Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
NAMNA AMBAVYO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI
Tumeona huko juu kuhusu visababishi vya maradhi na namna ambavyo maradhi yanaweza kusambaa, sasa hapa tutaona namna ambavyo miili yetu unapambana na maradhi haya kwa ajili yetu. Mwili una njia nyingi tuu na namna ya kupambana na maradhi kama utakavyoona hapo chini
1.KA KUTUMIA KUTA ZUIZI (PHYSICAL BARRIERS
Itambulike kuwa ili mtu aumwe ni kwamba wadudu wa maradhi wanatakiwa waingie mwilini. Sasa mwili una vizuizi yaani kuna ukuta maalum ambao unakazi ya kuzuoa wadudu hawa wasipate njia ya kuingia ndani. Vizuizi hivyo ni;-
A).Ngozi:ngozi yenyewe ni ukuta wa kuzuia vijidudu hivi. Ngozi hutumia chemikali kama jasho na mafuta ili kuuwa vijidudu hivi.ngozi inatabia ya kujitibu kwa haraka zaidi kama itapata jeraha ili kuzuia wadudu wasiingie.
B).Utando wa utelezi: huu ni utando maalumu ambao unateleza na kunata. Utando huu unapatika na sehemu nyingi za mwili kama puani kwa ajili ya kunasa mavumbi na vijidudu hawa. Utando huu pia upo machoni kwa ajili ya kunasa vijidudu hivi na kuvitoa nje.
C)Vinyweleo: hivi ni njia nyingine ya kunasa wadudu wowote wanaoraka kuingia ndani. Kwa mfano ndani ya pua kuwa vinyweleo hivi kwa ajili ya kunasa wadudu na mavumbi kuingia ndani.
D)Kemikali: kwa mfano mwili huzalisha asidi ya hydrocloric ambayo husaidia kuuwa bakteria waliopo kwenye vyakula.
2.INFLAMATORY RESPONSE (YAANI KUVIMBA)
Inatokea wadudu hawa wanaingia mwilini kwa mfano mtu anpojikata. Hivyo inflammatory response hali ya mwili kupambana na ma majeraha ambapo sehemu husika huvimba, huwa njeundu na kuwa na maumivu. Kitendo hiki hufanya eneo hili liwe limoto na kusababisha vimishipa vidogo vinavyoleta damu vilete damu kwa wingi na hatimaye seli kutoka kwenye damu hupambana na wadudu walofanikiwa kuingia kwenye eneo lile.
3.IMMUNE SYATEM (MFUMO WA KINGA)
Njia zilizotajwa hapo juu pekee haziwezi kupambana na wadudu hawa. Hivyo kuna mfumo maalumu wa kuukinga mwili dhidi ya majambazi hawa (pathojens) mfumo huu huitwa immune system ambao unatengenezwa na seli hai nyeupe za damu na aina flani ya protin ambayo kitaalamu huitwa antibodies ambazo zipo kwenye mfumo wa lymph (lymphatic system).
Mfumo wa lymph huu umezunguka mwili mzima na unahusika katika kubeba majimaji mwilini. Katika kufanya hivi unafanya kazi ya kuwatowa bakteria na pathogen wengine nje ya mwili. Mfumo huu una seli hai nyeupe nyingi nna hizi ndizo ambazo zinapambana na pathogen na kuwauwa.
Seli nyeupe za damu, kazi yao kuu seli hizi ni kuulinda mwili dhidi ya wavamizi. Kuna aina fani ya seli hizi hutowa kemikali ziitwazo antibodies ambazo huwakamata pathogens na pitowa tahadhari kwa seli nyingine ili wawaue hawa pathogens. Pindi unapoumwa hutokea tezi za lymph zinauma kama mtoki ni kwa sababu seli hizi nyeupe zipo kwa wingi eneo lile kupambana na wadudu hawa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kutumia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda, ni njia muhimu ambazo ni lazima kuzipitia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuzuia kiungulia
Soma Zaidi...Huduma ya kwanza ni huduma anayopewa mgonjwa au mtu yeyote aliyepata ajali kabla ya kumpeleka hospitalini
Soma Zaidi...Natak kufaham kuwa binadam akiwa mweupe mikononi atakuwa na upungufu wa vitamin gani?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wanaweza kupata, huduma hii utolewa hasa kwa wale ambao wamejitokeza kupima afya zao na kujua wazi hali zao na kwa wale wanaofatilia huduma hii wanaweza kuishi vizu
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa mate mdomoni, mate ni majimaji ambayo hukaa mdomoni na husaidia katika kazi mbalimbali mdomoni.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza sababu za kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya Surua kwa watoto, ni Aina ya chanjo ambayo utolewa kwa watoto na kufanya kazi mbalimbali mwilini ambazo ni kumkinga mtoto asipatwe na magonjwa.
Soma Zaidi...