Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:โKwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukavitere..
Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:โKwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na Uadilifu (mizani) pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. (57:25)โYeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na kw a dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia.โ (9:33, 61:9)
Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.w) ni wale wenye tabia ifuatayo:
1. Kuwatii Mitume ipasavyo kwa kufanya yale yote waliyoamrisha na kuacha yale yote waliyoyakataza kama Qurโan inavyosisitiza:โ... Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho...โ (59:7)Sem a: โIkiw a nyinyi mnampenda Mw enyezi Mungu, basi nifuateni;(hapo)Mw enyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu.Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, mwenye rehema.Sema: โMtiini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na kama mkikengeuka, (Mw enyezi Mungu atakutieni adabu), kw ani Mw enyezi Mungu haw apendi Makafiriโ (3 :31-32)
2.Kuwafanya Mitume vigezo vya maisha yao kibinafsi, kifamilia na kijamii kama inavyosisitizwa katika Qur-an:โBila shaka mnao mfano mwema (wa kuiga) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana โ. (33:21)
3.Kuwapenda Mitume kuliko nafsi zao kama Qur-an inavyosistiza:โSema โKama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali m lizozichum a na biashara mnazoogopa kuharibikiw a,na majumba mnayoyapenda; (ikiwa vitu hivi) ni vipenzi zaidi kw enu kuliko Mw enyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni mpaka Mw enyezi Mungu alete am ri yake; na Mw enyezi Mungu hawaongozi watu maasiโ (9:24)
Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume si jambo lingine zaidi ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa unyenyekevu na upendo. Muumini wa kweli hatakuwa tayari kuifurahisha nafsi yake au kumfurahisha yeyote awaye kinyume na kumfurahisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema:
โHatakuwa mmoja wenu ni Muumini wa kweli mpaka anipende zaidi kuliko chochote kile ikiwa ni pamoja na familia yake, mali yake na watu woteโ.(Sahihi Muslim)
โYeyote yule anayependa Sunnah yangu ananipenda, na yeyote yule anayenipenda atajikuta yuko ubavuni kw angu huko Peponi.โ (Tirm idh)
4. Kuwafanya Mitume kuwa Mahakimu wao pale wanapohitilafiana katika jambo lolote lile kama tunavyojifunza katika Qur-an:โNaapa kwa (haki ya) Mola wako (Ewe Muhammad); wao hawawi wenye kuamini mpaka wakufanye hakimu katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyopitisha, na wanyenyekee kabisa.โ (4:65)โHaiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiyari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotofu (upotevu) ulio wazi. โ (33:3 6)
5.Kuwa na yakini kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) ndiye Mtume wa mwisho kama Qur-an inavyosisitiza:โMuhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Mitume, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.โ (33:40)
6.Kumswalia Mtume(s.a.w) mara kwa mara katika swala na kila anapotajwa. Kumswalia Mtume(s.a.w) ni amri ya Allah(s.w) kama inavyotuelekeza ifuatavyo:Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume;na Malaika wake. Basi; Enyi mlioamini,
Umeionaje Makala hii.. ?
Faradhi kwa maiti ya muislamu (edk form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุฑูููุฑูุฉู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฃูููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ู ููู ููุงูู ููุคูู ููู ุจูุงููููููู ููุงููููููู ู...
Soma Zaidi...Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini.
Soma Zaidi...Hili ni swali kutoka katika maarifa ya elimu ya dini ya kiislamu kidato cha kwanza (EDK FORM 1)
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Waislamu wanakatazwa kufanya na kufuata mambo kwa kibubusa (kwa mkumbo) bila ya kuwa na ujuzi unaostahiki.
Soma Zaidi...