KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)


Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Semeni nyinyi (Waislamu kuwaambia Mayahudi na Wakristo kuw a): “Tumemw amini Mw enyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu, na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutafautishi baina ya yoyote katika hao.


(Wote tunawaamini), na sisi tumenyenyekea kwake.” (2:136)Kuamini baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuwakanusha wengine kama walivyo fanya mayahudi na Wakristo ni Ukafiri kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Hakika wale wanaomkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume yake, na wanataka kutenga baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume yake, kwa kusema: “Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa, ” na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (si ya Kiis lam u kh as a w ala y a Kikafiri).


Hao ndio Makafiri kweli.Na tumewaandalia makafiri adhabu idhalilishayo.(4:150-151).


Na waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake wala wasimfarikishe yoyote katika wao (bali wamewaamini wote), hao atawapa ujira wao. Na Mw enyezi Mungu ni Mw ingi w a kusamehe (na) Mw ingi wa kurehemu.” (4 :152).


“Na kwa yakini tuliwatuma mitume kabla yako (Muhammad). Wengine katika hao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia...” (40:78)