Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao

Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s.w).


Kwa mfano, maquraishi walipomjia Mtume (s.a.w) na rai ya kuchanganya haki na batili katika ibada, Mtume (s.a.w) aliamuriwa na Mola wake awape msimamo wa Uislamu kama ifuatavyo:


“Sema: Enyi m akafiri, siabudu mnachoabudu.Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.


Wala sintaabudu mnachoabudu. Wala nyinyi hamtamuabdudu ninayemuabudu. Nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu ” (109:6)