Navigation Menu



image

Maisha ya Mitume

Maisha ya Mitume

Maisha ya Mitume




Ukiyachunguza maisha ya mitume mbalimbali kama yalivyoelezwa katika Qur-an utabaini kuwa wao kweli walikuwa ni wajumbe wa Allah (s.w). Tunayoyaona katika maisha ya Mitume ambayo yanatuhakikishia kuwepo kwa Allah (s.w) ni pamoja na:



(i)Kuwepo kwao na kujieleza kwa watu wao kuwa niMitume wa Mwenyezi Mungu (s.w)



(ii)Msimamo wao katika kujieleza kwa jamii zao kuwa wao ni Mitume wa Allah (s.w)



(iii)Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na (mazingira) jamii



(iv)Miujiza waliyoionesha katika kuthibitisha utume wa o



(v)Kuhimili kwao mateso na kujitoa kwao muhanga kwa ajili ya Allah (s.w)



(vi)Ujasiri wao katika kuwakabili viongozi wa jamii zao.



(vii)Ushindi wao dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu



(viii)Mitume kutohitaji malipo yoyote kwa ajili ya kaziyao.



(i) Kuwepo kwao na kujieleza kwa watu wao kuwa ni Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w)
Mitume walijieleza kwa uwazi kuwa wao ni mitume wa Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika mifano ifuatayo:“Tulimtuma Nuhu kwa watu wake naye akasema: ‘Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakuhofieni adhabu ya siku iliyo Kuu. (7:59).


Wakuu wa watu wake wakasema: “Sisi tunakuona uko katika upotofu uliodhahiri.(7:60).Akasema (Nuhu):“Enyi kaumu yangu mimi simo katika upotofu lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola wa walimwengu wote. (7: 61).Na kw a Adi (tulimpeleka) ndugu yao Hudi akasema: “Ewe kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu nyinyi hamna Mungu ila Yeye Hamuogopi? (7:65)Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake:“Sisi tunakuona umo katika upumbavu na tunakuona u miongoni mwa waongo”. (7:66)


Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mimi sina upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola wa walimwengu.(7:67)
Pamoja na Mitume kujieleza kuwa wanatoka kwa Allah (s.w) mwenyewe Allah (s.w) anatufahamisha kuwa ametuma 83Na bila shaka tulimpeleka Mtume katika kila umma ya kwamba, “muadubuni Mwenyezi Mungu na mwepukeni muovu (twaaghuut)… (16:36)


Bila shaka Sisi tumekutuma (tumekuleta) kwa haki ili ubashirie na uonye. Na hakuna taifa lolote ila alipita humo muonyaji (Mtume kuwaonya). (35:24Na kwa yakini tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukusimulia na haikuwa kwa Mtume yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na itakapokuja hukumu ya Mwenyezi Mungu kutahukumiwa kwa haki, na wafanyao mambo ya batili watapata hasara wakati huo. (40:78).


Hivyo, kuwepo kwa Mitume kunatuthibitishia kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.a.w) kwa namna mbili, kwanza, kama Mwenyezi Mungu (s.w) asingelikuwepo asingelileta Mitume kwa wanaadamu. Pili, Mitume wote waliotokea katika nyakati mbali mbali za historia wasingelitoa dai moja linalofanana kwa wote kuwa wao ni Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) kama Mwenyezi Mungu hayupo.



(ii) Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na jam ii
Mitume wote takriban walizaliwa na kulelewa katika jamii za kijahili zilizozama katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w) na miungu chungu nzima.


lakini jambo la ajabu na kushangaza ni kwamba, Mitume wote tangu utotoni waliepukana na tabia za kijahili na walijiepusha mbali na kumshirikisha Mwenyezi Mungu (s.w).


Walikuwa na mwenendo wa kiutu (wa Kiislamu) uliowavutia watu wote wa jamii zao na walikuwa ni nyota katika jamii. Kwa mfano, Nabii Ibrahim (a.s) alizaliwa na kuhani Mkuu.


Yaani baba yake Nabii Ibrahim alikuwa ni kiongozi au msimamizi wa ibada ya masanamu. Lakini Nabii Ibrahim kamwe hakuvutiwa na ibada hiyo ya masanamu bali akiwa angali kijana mdogo aliona kuwa ni kinyume kabisa na akili ya mwanaadamu kuwaabudu miungu wengine kinyume na kumuabudu Allah (s.w) aliye mpweke.



Mfano wa pili ni ule wa Nabii, Musa (a.s) aliyelelewa katika nyumba ya Firaun aliyetakabari na kujiita mungu. Malezi hayo ya kifalme kamwe hayakumuathiri Nabii Musa (a.s). Aliinukia kuwa na mwenendo mwema wa kumpwekesha Allah (s.w).Mfano mwingine ni ule wa Mtume Muhammad (s.a.w) ambaye alizaliwa katika jamii ya Maquraysh iliyobobea katika ujahili na iliyozama katika ushirikina kiasi kwamba kila kitu kwao kiliweza kufanywa mungu na kuabudiwa. Katika wakati huo masanamu ya watu, ndege na wanyama yaliuzwa sokoni kama miungu wa kuabudiwa na hata tende zilifinyangwa na kuabudiwa.


Lakini tunavyojifunza katika historia, Mtume (s.a.w) tangu utotoni mwake hakuathiriwa kamwe na ibada za masanamu na mwendo wa ujahili. Bali tunajifunza kuwa aliinukia katika kumtambua na kumpwekesha Allah (s.w) na aliwazidi watu wote kwa tabia njema kiasi kwamba watu wake walimtegemea sana kwa ushauri na kuwatunzia amana zao na walimwita “mkweli”, “mwaminifu”na majina mengine kama haya yaliyodhihirisha tabia yake njema katikati ya jamii ya kijahili.


Ni kitu gani kilichowafanya Mitume kuwa tofauti na watu wa jamii zao? Je, hakuna aliyewatayarisha na kuwalea katika mwenendo huo ili wawe viigizo vyema katika jamii zao? Bila shaka Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye aliwewaleta Mitume ili wafikishe ujumbe wake na wawe viigizo vyema katika kuutekeleza Uislam kama inavyobainishwa katika Qur-an:Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na tukaviteremsha Vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. (57:25)




(iii) Dalili (miujiza) za kuthibitisha Utume wao
Mitume wameletwa pamoja na alama mbali mbali za kuwathibitisha Utume wao kwa watu wao.“Kwa hakika tumewapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi…” (57:25).
Kila Mtume alipewa dalili za kuwathibitishia watu wake kuwa yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Alama za Utume wa Nabii Musa (a.s) ni fimbo yake kugeuka kuwa nyoka wa kweli na mkono wake kutoa mwanga mkali kama tunavyojifunza katika Qur-an.


(Rejea 28:29-32)
Dalili za Utume wa Nabii Issa (a.s) zilikuwa ni kuwafufua wafu, kuwaponyesha vipofu na wenye mbaranga, kulifanya sanamu la ndege kuwa ndege wa kweli kama inavyobainishwa katika Qur-an (5:110).
Dalili aliyopewa Mtume Muhammad (s.a.w) ya kuthibitisha kuwa yeye ni Mtume wa Allah (s.w) ambayo itabakia mpaka mwisho wa ulimwengu ni Qur-an. Qur-an tofauti na vitabu vingine vya Allah (s.w) imehifadhiwa na uharibifu wa aina yoyote. Qur-an yenyewe inatukumbusha:Haw a izin ga tii n in i, h ii Qur-an? Na kam a ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila shaka w angeliku ta ndani yake kh itilafu ny ingi. (4:82).



(iv) Kuhimili mateso na kujitoa kwao muhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w)
Jambo jingine linalopatikana katika historia ya Mitume ni uvumilivu waliokuwa nao dhidi ya mateso mbali mbali waliyofanyiwa na watu wao na bado wakaendelea kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu bila ya kukata tama. Tukirejea katika Qur’an tunapata mifano mbali mbali ya mateso waliyofanyiwa na jamaa zao.


Kwa mfano tunajifunza katika Qur-an kuwa ilikuwa ni tabia ya Wayahudi (kizazi cha Israil) kuwauwa Mitume yao pasina haki:Wale (Mayahudi) wanaozikataa Aya za Mwenyezi Mungu, na wakawaua manabii pasina haki, na wakaua watu wanaoamrisha kusimamisha haki, wapashe habari ya adhabu kali.


(3:21)
Nabii Yahya (a.s) (Yohana mbatizaji) ni miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu waliochinjwa na Mayahudi, kwa sababu tu eti walisimama kidete kufikisha neno la Mwenyezi Mungu, kwa watu wao ili wasimamishe haki katika jamii kwa kufanya mema na kuacha maovu.


Pia Mayahudi walikula njama za kumuua Nabii Isa (a.s). Lakini Mwenyezi Mungu (s.w) alimuokoa na kumnyakuwa kwake kama tunavyojifunza katika Qur-an:Na kwa (ajili ya) kusema kwao: “Sisi tumemuua Masihi Isa, mwana wa Maryam Mtume wa Mungu”, hali hhawaku muua wala hawaku msulubu, bali walibadilishiwa (mtu mwingine wakamdhani Nabii Issa). Na kwa hakika wale waliokhitilafiana katika (hakika) hiyo (ya kumuua Nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo la kusema kauawa). Wao(kabisa) hawana yakini juu ya (jambo) hili (la kuwa kweli wamemua Nabii (Isa). Isipokuwa wanafuata dhana tu. Na kwa yakini hawakumua.(4:157)


Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake, na Mw enyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikim a. (4:158)Naye Nabii Ibrahim alitupwa motoni na jamaa zake, Mwenyezi Mungu (s.w) aliuamrisha moto kuwa baridi na salama kwake:“Tukasema: ‘Ewe moto! Kuwa baridi na salama juu ya Ibrahim”. (21:69)
Mitume pia walitiwa vifungoni na vizuizini (kutengwa na jamii) kama ilivyokuwa kwa Nabii Yusufu (a.s) na Nabii Muhammad (s.a.w). Baadhi ya Mitume na wafuasi wao walifukuzwa nchini mwao na kuhamia ugenini kama ilivyokuwa kwa Mtume (s.a.w) na Muhajirina:



“(Basi) wapewe (mali hayo) mafakiri wa Kimuhajiri ambao walifukuzwa katika nyumba zao na mali zao; (wakakhiari kuyaacha hayo) kwa ajili ya (kutafuta) fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi (yake) na kuinusuru (dini ya) Mw enyezi Mungu na Mtume wake. Basi hao ndio waislamu wa kweli. (59:8).
Mitume pia walinyanyaswa kwa matusi na kejeli. Kwa mfano Mtume Muhammad (s.a.w) aliitwa mwendawazimu, mchawi, mtunga mashairi, abtair (mkiwa) na matusi mengineyo.



Pamoja na kufanyiwa madhila yote hayo, bado Mitume walisimama kidete kuufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa watu wao na wala hawakukata tamaa. Ni nguvu gani iliyowapa Mitume ustahimilivu kiasi hicho? Je, kuna malipo yoyote ya hapa duniani waliyoyapata ndiyo yakawafanya kuwa wastahamilivu kiasi hicho? Je, Mitume hawakuwa na tegemeo la kulipwa na mwenye uwezo juu ya kila kitu anayestahiki kutegemewa na kuogopwa kuliko yeyote yule? Bila shaka uvumilivu na subira ya hali ya juu waliyokuwa nayo Mitume ni alama kuwa yuko mwenye nguvu na uwezo juu ya kila kitu waliyekuwa wakimtegemea na kutaraji ujira mkubwa kutoka kwake.



(v) Ujasiri wa Mitume mbele ya Viongozi wa jamii ya kishirikina
Mitume hawakumchelea yeyote katika kuwafikishia watu ujumbe waliotumwa kuufikisha.Hawakufikisha ujumbe wao kwa watu wa kawaida tu bali waliwaendea Wafalme na watawala wa jamii waliokuwa wapinzani wakubwa wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w). Mitume waliwaelekea wakuu hao wa jamii pamojana takaburi zao na vitisho vingi walivyovitoa dhidi yao. Kwa mfano Nabii Ibrahiim hakumchelea baba yake katika kumfikishia ujumbe wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:(Wakumbushe) alipomwambia baba yake: “Ewe baba yangu! Kwanini unaabudu visivyosikia na visivyoona na visivyo kufaa chochote?”


“Ewe baba yangu! Kwa yakini imenijia ilimu isiyokujia. Basi nifuate nitakuongoza njia iliyosawa ”.“Ewe baba yangu! Usimuabudu shetani, hakika shetani ni mwenye kumuasi (Mwenyezi Mungu) Mw ingi w a rehm a ”.“Ewe baba yangu! Hakika naogopa kukupata adhabu inayotoka kwa Mwingi wa Rehma (Mwenyezi Mungu), ukifanya hivyo) utakuwa mwenziwe shetani”.Akasema (yule baba yake):“Je, unaichukia miungu yangu, ewe Ibahimu? Kama huachi (haya unayoyasema) lazima nitakupiga mawe. Na niondokelee mbali, kwa muda mchache (huu)”. (19:42-4 6)
Nabii Ibrahim hakuishia kuufikisha ujumbe kwa baba yake tu, bali aliufikisha pia kwa vitendo kwa jamii nzima kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


“Na wallahi (kwa haki ya Mungu) nitayafanyia mabaya masanamu yenu haya baada ya kunipa mgongo mkenda zenu. ” Basi akayavunja (masanamu yote yale) vipande vipande isipokuwa lile kubwa lao (aliliacha), ili wao (hao makafiri) walirudie.


Wakasema: “Nani aliyeifanya hivi miungu yetu? Hakika huyo yu miongoni mwa madhalimu (wakubwa).” Wakasema: “Tulimsikia kijana mmoja akiwataja anayeitwa Ibrahim ”.


Wakasema: “Basi mleteni mbele ya macho ya watu, wamshuhudie (kwa ubaya wake huyo)” Wakasema: “Je! Wewe umeifanya hivi miungu yetu, Ee Ibrahim?” Akasema: “Siyo, bali amefanya (hayo) huyu mkubw a wao, basi (muulizeni na) waulizeni (pia hao waliovunjwa) kama wanaweza kusema!


Basi wakajirudi nafsi zao, (wakafikiri udhalilifu wa waungu hao walio nao, wasioweza kujipigania) na wakasema: “Hakika nyinyi mlikuwa madhalimu (wa nafsi zenu kwenda kuwaabudu wasiokuwa na maana). ” Kisha wakainamishwa vichwa vyao, (wakarejea ujingani, ukafirini, wakasema): “Hakika umekwishajua ya kwamba hawasemi, (kwa nini unatucheza shere?)”.


Akasema: “Je! Mnaabudu badala ya Mw enyezi Mungu (miungu) isiyokufaeni chochote (mnapowaabudu) wala kukudhuruni (chochote mnapoacha kuwaabudu?” Kefule (udhalilifu) yenu na ya hivyo mnavyoviabudu kinyume na Mwenyezi Mungu. Je! hamfikiri? (21:57-67)
Pia Nabii Ibrahim (a.s) alimkabili mfalme na kuhojiana naye. - Rejea Qur-an (2:25 8)



(vi) Ushindi wa Mitume dhidi ya maadui
Jambo jingine tunalojifunza katika historia ya Mtime ambalo ni miongoni mwa dalili kubwa za kuonyesha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ushindi waliokuwa wakiupata Mitume na wafuasi wao wachache dhidi ya maadui zao. Mara zote walikuwa wapinzani wakubwa wa ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w) walikuwa watawala wa walioshikilia dola na matajiri waliokuwa na wafuasi wengi na majeshi yenye nguvu kubwa.



Kwa upande mwingine, katika jamii zote, walioamini Mitume walikuwa wachache na wengi wao wakiwa wanyonge wa jamii. Pamoja na hivyo Mitume na waumini wachache wanyonge waliwashinda maadui zao walikuwa na nguvu kwa kiasi kikubwa.


Hebu turejee mifano michache ifuatayo:Nabii Nuhu (a.s) aliwalingania watu wa jamii yake kwa miaka 950. Lakini watu wake pamoja na kutishia kumuua, walimtaka awaletee kutoka kwa Mola wake hiyo adhabu aliyokuwa akiwatahadharisha kwayo ikiwa anasema kweli kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.w). Mwishowe adhabu kweli ililetwa na wakawa ni wenye kugharikishwa kama tunavyojifunza katika Qur-an:


Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa motoni wala hawakuwapata wa kuw anusuru mbele ya Mw enyezi Mungu (s.w). (71 :25)
Nabii Hud (a.s) alitumwa kwa watu wa Ad na kuwafikishia ujumbe wa Mwenyezi Mungu (s .w). Lakini wengi wao wakiongozwa na watawala na matajiri walitakabari na kukataa na kuwa dhidi yake na wafuasi wachache walioamini pamoja naye. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w) alimnusuru Mtume wake na walioamini pamoja naye kutokana na madhalimu kama tunavyojifunza katika Qur-an:



Basi tukamuokoa yeye na waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata mizizi ya wale waliozikadhibisha aya zetu, na (ambao) hawakuwa wenye kuamini. (7:72).
Nabii Musa (a.s) na wana wa Israil waliokolewa kutokana na makucha ya dhalimu Firaun na majeshi yake kama tunavyojifunza katika Qur-an:


Basi (watu wa Firaun na mwenyewe nafsi yake Firaun) wakawafuata (Nabii Mussa na watu wake) lilipotua jua. Na yalipoonana majeshi mawili (haya, watu wa Nabii Musa wanakimbia, na Firauni na watu wake wanawafuatia). Watu wa Musa walisema: “Hakika tutakamatwa ”.


(Musa) akasema: “La, kwa yakini Mola wangu yu pamoja nami, bila shaka ataniongoza (tuokoke sote)”. Mara tulimpelekea Wahyi Musa (tukamwambia): “Piga bahari kwa fimbo yako”. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama jabali kubwa.



Na tukawaleta hapo wale wengine (nao ni firauni na watu wake). Na tukamuokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye wote.


Kisha tukaw agharikisha hao w engine. Hakika katika hayo muna mazingatio: lakini wengi katika wao si wenye kuamini.


Na kwa yakini Mola wako ndiye Mwenye Nguvu, mwenye Rehema. (26:60-68)
Mfano wa mwisho ni ule unaopatikana katika historia ya Mtume Muhammad (s.a.w) na wafuasi wake. Vita vya kwanza vikubwa alivyopigana Mtume (s.a.w) na wafuasi wake dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu ni vita vya Badr. Katika vita hivyo jeshi la makafiri wa Kiquraish lililojizatiti barabara lilikuwa na watu 1000 ambapo jeshi la Waislamu lisilojiandaa vizuri kivita lilikuwa na wanajeshi 300 tu hivi. Pamoja na udogo na uduni wa jeshi, Waislamu walipata ushindi mkubwa kwa msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:



(Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mola wenu, naye akakujibuni kuwa:“Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa malaika elfu moja watakaofuatana mfululizo (wanaongezeka tu)”.


Na mwenyezi Mungu hakufanya haya ila iwe bishara (habari ya furaha) na ili nyoyo zenu zituwe kwayo. Na hakuna msaada (wa kufaa) ila utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima. (8:9-10).
Ushindi wa Mitume na wafuasi wao haukupatikana ila kwa msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).



(vii) Mitume kutohitajia malipo kutoka kwa watu wao:
Mitume, tofauti na viongozi wengine waliojitokeza katika jamii mbalimbali, hawakuifanya kazi yao ya kuwaongoza watu katika njia ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kutarajia maslahi yoyote si ya hali wala ya mali, kutoka kwa watu wao. Waliifanya kazi hiyo kama watumishi wa Mwenyezi Mungu (s.w) na ni yeye pekee waliyemtegemea awalipe kwa kazi hiyo.


Daima walikuwa wakiwakumbusha watu wao jambo hili kama tunavyorejea katika Qur-an:
“Wala sikutakini juu yake ujira, ujira wangu hauko ila kw a (Mw enyezi Mungu) Mola w a w alimw engu w ote ”. (26:127)
Mitume wasingelikuwa wajumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w) wenye uhakika wa kupata ujira mkubwa kwake kwa kazi yao, kitu gani kingeliwazuia wasitake malipo kutoka kwa watu wao,kama viongozi wa kawaida wa jamii za wanaadamu wanavyotaka malipo kutoka kwa watu wao?




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1013


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Nguzo za imani
Zifuatazo Ni nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

zijue Nguzo za uislamu, imani, ihsani pamoja na dalili za qiyama
عَنْ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَيْضًا قَالَ: " بَيْنَمَا نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم ذَاتَ يَوْمٍ، إذْ ?... Soma Zaidi...

Mazingatio kabla ya kuosha maiti
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kujiepusha na kuua nafsi bila ya Haki
Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo. Soma Zaidi...

Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab
Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa Soma Zaidi...

Kwa nini Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa
Kwa nini uislamu ndio dini pekee ya haki ambayo watu wanatakiwa waifuate. Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...

Historia ya Mwanadamu
Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
2. Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Neema Alizotunukiwa Nabii Daudi(a.s)
Soma Zaidi...

Maisha ya Mitume
Soma Zaidi...