UMBILE LA MBINGU NA ARDHI


“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.w) kwa wenye akili.” (3:190).


Mungu, Muumba wa kila kitu ndiye mmiliki pekee wa viumbe vyote. Ni Yeye anayebadili mielekeo ya upepo,anayekusanya mawingu, anayewasha jua na kuiangazia dunia na kudhibiti sayari zizunguuke katika mihimili yao.Kudai maisha haya ya dunia na ulimwengu mzima yanatokana na bahati nasibu ni kutokitumia kipawa cha busara alichotunukiwa kila mwanaadamu mwenye akili timamu. Mpango bora wa dunia na ulimwengu kwa ujumla unapinga uwezekano wa kutokea kwa bahati nasibu tu, na kinyume chake ni ishara ya wazi ya uwezo wa Allah(s.w)usio na kikomo unaodhihirisha kuwepo kwake.Wakati ambapo ni muhali hata kwa kitu chepesi kufanya mzunguko wa moja kwa moja katika njia yake bila kwenda kombo, dunia pamoja na ukubwa wake yenye mkusanyiko wa vitu visivyo na idadi hufanya hivyo.


Na imekuwa ikifanya hivyo kwa miaka dahari, na dahari, tangu dunia kuumbwa na kuanza mzunguko wake. Allah anasema Yeye ndiye mfanyaji wa mahesabu ya mzunguko huo.
Hakika Mw enyezi Mungu am ekw is ha kiw ekea kila kitu kipimo chake. (65:3)Utaratibu huo bora wa ulimwengu unaendeshwa kwa mfumo wa ajabu unaokwenda kwa kutegemea mihimili isiyo na mashiko.Wengine hudhani kuwa baada ya kuumba, Allah(s.w)amekiacha kila kitu kijiendeshe chenyewe tu. La hasha kila tukio litokealo mahala popote pale ulimwenguni hutokea kwa idhini ya Allah(s.w) na chini ya udhibiti wake. Qur’an inatufahamisha:


Je! Hujui ya kwamba Mwenyezi Mungu anajua yaliyoko mbinguni na ardhini? Bila shaka yote yamo kitabuni mwake. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni sahali. (22:70)


Kwa ujumla, umbile la mbingu na ardhi pamoja na vyote vilivyomo - jua, mwezi, nyota, sayari mbali mbali, milima na mabonde, maji ya mvua, bahari, mito na maziwa, mimea ya kila namna, wanyama wa kila namna na kadhalika ni hoja kubwa ya kuthibitisha kuwepo Allah (s.w) na utukufu wake kwa kila mwenye kutumia akili yake vizuri. Kila mtu atakavyobobea katika taaluma zinazohusiana na maumbile ya mbingu na ardhi kama vile Jeografia, Elimu ya anga (Astronomy), Elimu ya mimea (Botany), Elimu ya wanyama (Zoology), n.k. ndivyo Imani yake ya kuwepo Allah (s.w) itakavyopea.Kwa hakika wanaomuogopa Allah (s.w) miongoni mwa waja wake ni wale wataalam...” (35:28)