Imani ya Kiislamu na ni nani muumini?
Sura ya Tatu
IMANI YA KIISLAMU
Maana ya imani
Imani: ni neno la Kiarabu lenye maana ya kuwa na yakini au kuwa na uhakika moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana machoni lakini kuna dalili za kuthibisha kuwepo kwake
. Hivyo ili mtu awe na imani juu ya jambo lolote lile asiloweza kuliona, hanabudi kuwa na ujuzi wa kina utakaompa hoja au dalili za kutosha zitakazomkinaisha moyoni juu ya kuwepo jambo hilo.
Nani Muumini?
Imani ni kitu cha moyoni kisichoonekana lakini dalili za Muumini huonekana kwenye matendo. Katika Uislamu mtu hatakuwa Muumini kwa kudai tu bali uumini wake utaonekana katika matendo yake.
Katika Qur-an tunafahamishwa kuwa:
“Na katika watu wako wasemao, ‘tumemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.”(2:8).
Si wenye kuamini kwa sababu hawajaingiza imani yao katika matendo bali wamebakia kwenye kudai tu kuwa wao ni waumini pengine kwa kujiita majina au kuchagua kufanya vitendo fulani fulani tu.
Muumini wa kweli ni yule atakayethibitisha imani yake katika mwenendo na matendo yake ya kila siku.
“Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa hofu, na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.(8:2).
Ambao husimamisha swala na wanatoa katika yale tu liy ow apa. (8:3).
Hao ndio wanaoamini kweli kweli, wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora kabisa”. (8:4).
“Wenye kuamini kweli kweli ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kisha wakawa si wenye shaka na wanaopigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kw eli kweli” (49:15)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waumini wa kweli ni wale wenye sifa zifuatazo:
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
UMBILE LA MBINGU NA ARDHI
“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)
Soma Zaidi...Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake
Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu.
Soma Zaidi...Jifunze ni kwa namna gani Malaika waliweza kuwasiliana ana manabii Malimbali
Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.
Soma Zaidi...