Fahamu kuhusu dawa ya fluoroquinolones/quinolones

Post hii inahusu dawa ya kupambana na bakteria, hili kundi la fluoroquinolones lina dawa kuu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin.

Fahamu kuhusu dawa ya fluoroquinolones .

1. Hii ni mojawapo ya dawa za kupambana dhidi ya maambukizi ya bakteria dawa hii kama tulivyoona hapo mwanzoni Ina dawa muhimu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin na kundi hili pamoja na kutibu magonjwa mengine ni maarufu katika matibabu ya maambukizi kwenye mfumo wa hewa, maambukizi kwenye ngozi ambayo uambatana na viupele pamoja na miwasho, maambukizi ya kaswende na kisonono au kwa lugha ya kitaamu huiitwa sexual transmission diseases and sexual transmission infection.

 

2. Dawa hizi ufanya kazi mwili kwa kuharibu kabisa kazi ya bakteria kwa kuingilia DNA ya bakteria na kuzuia bakteria kuendelea kuzaliana hatimaye kufa, dawa hizi kwa kawaida utumiwa kwenye mdomo kama vidonge na pia uweza kuingia kwenye mmengenyo wa chakula na kuelekea kwenye mzunguko wa damu ambapo usambaza sehemu mbalimbali kama vile kwenye sehemu zozote za mwili zenye maambukizi na kuharibu kabisa kazi ya bakteria kwa kuingilia DNA ya bakteria.

 

3. Pamoja na magonjwa ambayo utibiwa na dawa hizi Kuna magonjwa mengine kama hays kuharisha na kutapika, maambukizi kwenye kibofu cha mkojo, kwenye joint na kweye magoti, kwenye tumbo na pia maambukizi kwenye via nya uzazi kama Kuna bakteria ameshambulia huko.

 

4. Ambao hawapaswi kutumia dawa hii ni wale wenye aleji na dawa hii pamoja na watoto chini ya miaka kumi na minane pamoja na wanawake wenye mimba.pia utumika kwa uangalizi kwa wenye magonjwa ya Figo na inii.

 

5. Maudhi madogo madogo ya dawa hii ni pamoja na kizunguzungu, maumivu ya kichwa, maumivu ya tumbo, kichefuchefu na kutapika, kuharibu na pengine kupandisha sukari.

 

6. Kwa hiyo dawa hii haiitumiki kiholela mpaka kuwepo kwa maagizo ya wataalamu wa afya kwa sababu dawa hii Ina maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kuleta shida ikiwa mgonjwa yupo nyumbani ila kama yupo hospital ni rahisi kumpatia huduma ya kwanza.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/22/Thursday - 09:19:17 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 681


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-