Dawa ya fangasi kwenye mdomo na ulimi

Utajifunza dalili za fangasi mdomoni na ulimini, sababu za fangasi wa mdomoni na ulimini, matibabu yeke na njia za kukabiliana nao

Dawa ya fangasi kwenye mdomo na ulimi

Dawa ya fangasi kwenye mdomo na ulimi
Fangasi wanaweza kuathiri sehemu yeyote kwenye ngozi ya mtu. Kuanzia vidole, kichwa, kwapa, sehemu za siri na mapajani. Hutokea fangasi wakaathiri mdomo na ulimi. Hapa hali inaweza kuwa mbaya pale mtu akishindwa kula. Bila shaka ni maumivu, lakini leo nitakwenda kukutajia tiba yake.Nini sababu ya fangasi wa mdomo na ulimi?
Fangasi hawa husababishwa na aina ya fangasi inayoitwa Candida albicans (C.albicans). hawa fangasi ni kawaida kupatikana kwenye mdomo. Kwa mtu ambaye kinga yake ipo imara hakuna shida yeyote anaweza kuipata kwa kuwa na fangasi hawa. Ila endapo watazidi kupitiliza ndipo inaweza kuleta shida.Dalili za fangasi kwenye mdomo na ulimi
1.Vijidoma vyeupe au njano kwenye shavu kwa ndani, finzi, midomo na kwenye ulimi
2.Kuvuja kwa damu wa finzi
3.Vidonda kwenye mdomo
4.Kuhisi kama kuna pamba kwenye mdomo (vinyuzinyizi)
5.Ukavu wa kona za mdomo pamoja na mipasuko
6.Taabu katika kumeza
7.Mdomo kuwa na ladha mbaya
8.Kupotesa ladha ya unachokila.Fangasi wa mdomoni wanaweza kuambukiza?
Yes wanaweza kuambukizwa kwa mfano ukimkisi (denda) mtu anaweza kupata fangasi hawa kama na wewe unao.Dawa ya fanasi kwenye mdomo na ulimi
1.Fluconazole hiini ya kumeza
2.Clotrimazole (Mycelex Troche) ni kidonge pia cha kumumunyikia mdomoni
3.Nystatin (Nystop, Nyasta) ni ya kuosha mdomo
4.Itraconazole (Sporanox) ni ya kumeza, hupewa wale wenye usugu ama wenye HIV
5.Amphotericin B (AmBisome, Fungizone) hutumika kutibu hali mbaya zaidi ya fangasi wa mdomoni.Nini ufanye ukiwa unatumia dawa hizi
1.Piga mswaki kwa mswaki ulio mlaini
2.Badili mswaki baada ya kumaliza dozi
3.Usitumie dawa za kuosha mdomo mpaka daktari akuambie.
4.Osha mdomo kwa maji ya chumvi
5.Changanya maji na juisi ya limao kisha knywa

                   

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2226


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-