Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa

Utoaji wa zaka katika Dhahabu, fedha ama silva na pesa

(iii) Dhahabu (gold), fedha (silver) na fedha taslimu (cash)



Miongoni mwa vitu vinavyopendwa na wanaadam ni dhahabu na fedha. Ni vitu hivi walimwengu katika kipindi kirefu cha historia huvitumia kama kipimo cha thamani ya vitu mbali mbali, na ndio vimetumika kama kipimo cha utajiri. Kwa hiyo vimestahiki zaidi kutolewa Zakat:



β€œ... Na wale wakusanyao dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari ya adhabu iumizayo” (9:34).


Aya hii inatuthibitishia kuwa kutoa katika njia ya Allah kutokana na dhahabu na fedha (silver) ni lazima kwa Muislamu. Pia fedha taslimu (Bank money or cash) ziko katika mkumbo huu.



Nisaab ya dhahabu, fedha na fedha taslimu na viwango vya Zakat Nisaab ya dhahabu na fedha imeelezwa katika Hadith ifuatayo:



Ali (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana Zakat kutoka kwa Farasi au Punda. Kwa hiyo chukua Zakat ya fedha (silver), dirham moja kwa kila dirham arobaini (1/40). Hapana Zakat kwa dirham 190. Zinapofika dirham 200, basi kuna dirham 5 za Zakat” (Tirmidh, Abu Da ud).



Kutokana na Hadith, kiwango cha Zakat ya dhahabu, fedha (silver) ni Dirham moja. Dirham ni fedha zilizotumika katika baadhi ya nchi za kiarabu tangu wakati wa Mtume Muhammad (s.a.w) hadi hivi sasa. Pia katika Hadith hii tunafahamishwa kuwa Nisaab ya fedha (silver) ambayo ni sawa na nisaab ya dhahabu na fedha taslim ni dirham 200. Tukitumia kipimo cha uzito Nisaab ya fedha ni gram 577.5 au tola 52.5. Nisaab ya dhahabu ni gramu 82.5 au tola 7.5. Muda wa kutoa Zakat ya fedha, dhahabu na fedha taslim ni baada ya kupindukia mwaka mmoja. Kwa hiyo dhahabu, fedha na fedha taslim zitakapowekwa akiba kwa kipindi cha mwaka mzima zikiwa zimefikia thamani ya dirham 200 au zaidi zitatolewa Zakat kwa kiwango cha 1/40 au 2.5%.




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 611

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana: