HUDUMA YA KWANZA KWA MWENYE KIZUNGUZUNGU


Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa. Kizunguzungu kinaweza kuwa ni dalili ya tatizo flani kwenye afya ya mtu. Maradhi mengi yanahusiana na kizunguzungu, hivyo baada ya huduma ya kwanza na mgonjwa akawa hajambo ni vyema aende kituo cha afya akajuwe chanzo cha kizunguzungu:Mtu mwenye kizunguzungu anaweza kujipa huduma ya kwanza mwenyewe. Vinginevyo anaweza pia kupata maelekezo kutoka kwa mtu aliye karibu naye kwani siku zote mgonjwa anakosa uwezo wa kujimilikia\ hasa kujipa huduma ya kwanza.
1.Kwanza mwenye kizunguzungu anatakiwa akae chini


2.Kama alikuwa akitembea ama alikuwa akifanya shuhuli yeyote anatakiwa aache na akae chini kabisa na wala asichchumae.


3.Akaechini kipolepole na katu asiharakishe


4.Kama kukaa chini hakutoshi ni vyema alale, kama anaona kama dunia inazunguka asilale kichalichali.


5.Kama anakiu mpe maji ya kutosha anywe


6.Akae sehemu iliyotuia, isiyo na fujo wala mwanga mkali wa taa ama jua


7.Ni vyema kama atapata usingizi walau kidogo


8.Kizunguzungu kikiondoka kwanza akae chini kipolepole na anapotaka kusimama asimame kipolepole na katu asitumie kitu ili kimsaidie kusimama kama fimbo