picha

Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 17: Hadithi ya Mtume Muhammad ﷺ kukutana na Bahira akiwa na miaka 12

Katikasomo hili utakwenda kujifunza stori maarufu ya Bahira kuhusu kukutana na Mtume Muhammad ﷺ na kumtambuwa utume wake.

KUKUTANA NA BAHIRA MWANAZUONI WA KIYAHUDI:

kuna historia stori maarufu ambayo inamuhusu Mtume Muhammad wakati ni mdogo. Hata hivyo wanahistria na baadhi ya maulamaa wamedhoofisha masimulizi haya na kusema kuwa ni stori za kutungwa kwani hazina ushahidi wa kutosheleza juu ya kutokea kwake. Stori yenyewe ni hiyo hapo chini:- 


Mzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Sikumoja wakati Mtume alipokuwa na umri wa miaka kumna mbili (12) alitoka yeye na kijana wake kuelekea Sham (Syria) kwa ajili ya kufanya biashra. Basi walipofika sehemu inayoitwa Busra walikutana na kuhani mmoja wa kiyahudi aliyeitwa Bahira na inasemekana jina lake halisi ni George (Joji kwa matamshi ya kiswahili). Mtu huyu aliwaonesha ukaribu mkubwa sana, a katu hajawahi kuonesha ukarimu huu kwao watu hawa kwani walikuwa ni wageni kwake.



Bahira aliushika mkono wa Mtume na akasema “huyu ndiye kiongozi wa watu wote, Allah atamtuma kwa kumpa ujumbe ambao utakuwa ni rehma kwa viumbe wote” hapa mzee Abu Talib akamuuliza “umejuaje jambo hili” Mzee huyu akajibu kwa kumwambia “mlipokuwa mnakuja alipotokea upade wa Aqabah niliona miti na majabali vyote vinamsujudia (yaani vinampa heshima) na huwa vitu hivi havifanyi hivi ila kwa mitume tu. Pia naweza kumjuwa kwa kuwa ana mhuri wa mitume chini ya bega lake kama tunda la tofaha (epo) yote haya tumeyasoma kwenye vitabu vya dini yetu”



Baada ya mazungumzo Bahira akamwambia mzee Abu Talib amrudishe kijana Makkah kwani Bahira alihofia kuwa watu wa huko wendako huenda wakamgunduwa kuwa huyu atakujakuwa mtume wa mwisho hivyo wakamfanyia hasadi na kumuua. Kwani Mayahudi walikuwa wakihubiri kuhusu Mtume wa Mwisho lakini walitarajia kuwa atatokea miongoni mwa kabila lao hivyo wakitambua kuwa Mtume wa Mwisho ni Muarabu wanaweza kumuuwa kama walivyowauwa mitume wao huko nyuma. Basi mzee Abu talib alitii na kumrudisha kijana wake Makkah. 



Wanazuoni wa sirah wanazungumza maelezo mengi kuhusu habari hii ya Bahirah na Kijana Muhammad. Wapo wanaoeleza kuwa Bahira baada ya kutamka maneno ya kuwa huyu kijana atakujakuwa ni mtume alitaka kujiridhisha zaidi hivyo akaanza mazungumzo na kijana ili aweze kubaini mengi zaidi. Basi katika mazungumzo yake Bahira alisema “Nakuapia kwa Mungu Lata na Uzza” bahira alitambuwa kuwa Lata na Uzza ni miungu wa washirikina wa Makkah hivyo Mtume hatavumilia maneno haya. Basi kijana Muhammad aliposikia maneno yake akamwambia “Usitaje Lata na Uza mbele yangu, ninawachukia” Kufika hapa Bahira akawa amejiridhisha kabisa kuwa huyu ndiye Mtume wa Mwisho.



Katika masimulizi mengine ni kuwa Bahira alikaribisha msafara mmoja wa kibiashara kwenye tafrija yake. Msafara huu ndio ulikuwa msafara wa Abu Talib na wenzie. Basi bahira akawaambia watu wote waingie ndani kwenye tafrija isipokuwa hyuy mtoto (Muhammad) abakie nje ili kulinda mizigo. Basi wakati tafrija inaendelea bahira akaanza kuona miujiza kama Kusujudi kwa mitu (kutoa heshima) na kufunikwa na mawingu wakati kwa ajili ya kivuli. Hapo ndipo Bahira akatambua kuwa huyu ni Mtume.



Na hapo ndipo alipomsahuri mzee Abu talib kuwa kijana huyu asiendenae huko Syria kwani mayahudi wakimjuwa watamuua. Mzee abu Talib alitii ushauri huu hivyo akauza bidhaa zake paleple kwa bei iliyo nafuu ili aweze kurudi zake Makkah. Abu Talib safari yake ya biashara ikaishia palepale bila ya kufika Syria.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-07-28 21:31:27 Topic: Historia ya Mtume Muhammad (s.a.w) Main: Masomo File: Download PDF Views 992

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 web hosting     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 ai web app     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 40: Historia fupi ya Walib Ibn Al-Mughira

Katika somo hili utajifunza kuhusu mmoja katika maadui wakubwa wa Mtume Muhammad wakati akilingania watu.

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad (s.a.w) somo la 21: Ndoa ya Mtume Muhammad na Bi khadija

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu ndoa ya Mtume Muhammad ﷺ na Bi Khadija

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 65: Safari ya Israa na Miraj

Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu historia ya safari ya sira na miraji na yanayopatikana katika safari hiyo

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 36: Historia fupi ya Abu Lahab

Katika somo hili utakwenda kujifunza historia fupi ya Abu Lahab

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 10: Kufa kwa mama yake Mtume ﷺ

Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu habari ya kifo cha Bi Amina ambaye ni mama yake Mtume MUhammad ﷺ

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Muhammad ﷺ somo la 29: Amri za kwanza alizopewa Mtume Muhammad ﷺ

Katika somo hili utajifunza amri ambazo alipewa Mtume Muhammad ﷺ mwanzoni kabisa mwa kazi yake ya Kulingania dini

Soma Zaidi...