Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu historia ya Amina mama wa Mtume Muhammad ﷺ
Amina bint Wahb ibn Abd Manaf al-Zuhriyya
Amina bint Wahb ibn Abd Manaf al-Zuhriyya (Kiarabu: آمِنَة بِنْت وَهْب, kwa kilatini: ʾĀmina bint Wahb, takriban 549–577) alikuwa mama wa Mtume wa Kiislamu Muhammad. Alitoka katika kabila la Banu Zuhra.
Maisha ya Awali na Ndoa:
Aminah alizaliwa kwa Wahb ibn Abd Manaf na Barrah bint 'Abd al-'Uzzā ibn 'Uthmān ibn 'Abd al-Dār huko Maka. Kabila lake, Quraysh, linasemekana kuwa wazao wa Ibrahim (Abraham) kupitia mwanawe Isma'il (Ishmael). Mwana wao Zuhrah alikuwa kaka mkubwa wa Qusayy ibn Kilab, babu wa Abdullah ibn Abdul-Muttalib, na msimamizi wa kwanza wa Qurayshi wa Kaaba. Abd al-Muttalib alipendekeza ndoa ya mtoto wake mdogo Abdullah na Aminah. Vyanzo vingine vinasema kuwa baba wa Aminah alikubali pendekezo (posa) hilo; vingine vinasema kuwa alikuwa ni mjomba wa Aminah, Wuhaib, ambaye alikuwa mlezi wake. Wawili hao walifunga ndoa muda mfupi baadaye. Abdullah alitumia muda mwingi wa ujauzito wa Aminah akiwa mbali nyumbani kama sehemu ya msafara wa wafanyabiashara na alikufa kwa ugonjwa kabla ya kuzaliwa kwa mwanawe huko Medina.
Kuzaliwa kwa Muhammad na Miaka ya Baadaye:
Miezi mitatu baada ya kifo cha Abdullah, mwaka 570–571 BK, Muhammad alizaliwa. Kama ilivyokuwa desturi miongoni mwa familia zote kubwa wakati huo kutafuta wanyonyeshaji na waleaji wa watoto wao kutoka mashambani, ili wapate kujuwa lugha kwa ufasaha, waepuke na magonjwa yanayozuka mijini, wawe na ukakamavu, na wajifunze tabia njema. Aminah Hivyo Muhammad alichukuliwa na Halima kwa ajili ya kulelewa. Imani ilikuwa kwamba jangwani, mtu angejifunza nidhamu binafsi, heshima, na uhuru. Wakati huu, Muhammad alinyonyeshwa na Halimah bint Abi Dhuayb, mwanamke maskini wa Bedouin kutoka kabila la Banu Sa'ad, tawi la Hawāzin.
Muhammad alipokuwa na umri wa miaka sita, alikutanishwa tena na Aminah, ambaye alimpeleka kumtembelea jamaa zake huko Yathrib (baadaye Medina). Waliporudi Maka mwezi mmoja baadaye, wakiwa na mtumishi wake, Umm Ayman, Aminah aliugua. Alikufa karibu mwaka 577 au 578, na alizikwa katika kijiji cha Al-Abwa'. Kaburi lake lilivunjwa mwaka 1998. Sababu ya kuvunjwa kwa makaburi mengi ni imani ya kuwa kuna watu walikuwa wanafanya ibada kwenye makaburi haya ama wengine walikuwa wakiyaomba. Hivyo fatuwa iliyotolewa na wanazuoni wa Sudia ni kuwa haya yote yanayofanywa ni bidaa na ni shirk. Hivyo makaburi mengi yalivunjwa na kuwa katika hali ya kawaida. Muhammad alichukuliwa kwanza na babu yake wa upande wa baba, Abd al-Muttalib, mwaka 577, na baadaye na baba yake mkubwa Abu Talib ibn Abd al-Muttalib.
Hatima katika Akhera:
Wanazuini wengi wa kiislamu bado wana hitilafu juu ya kuwa wazazi wa Mtume ni watu wa peponi ama wa motoni. Kuna hadithi nyingi zinanukuliwa hata hivyo wachambuwa wa hadithi wamedhoofisha nyingi katika hadithi hizo. na Nyinine zimepewa sifa ya kuwa ni za uwongo kabisa. Hivyo basi jambo hili tumuachie Allah.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Hatimaye Mtume Muhammad ﷺ anarejea Makkah na kuendelea na kazi yake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu kusimama kwa Wahyi kuja kwa Mtume Muhammad ﷺ
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kwa ufupi historia ya mmoja katika maadui wakubwa wa Uislamu wakati Mtume alipokuwa analingania dini.
Soma Zaidi...Baadhi ya matukio mengine yaliyoteokea kweye safari hii ya Tfai
Soma Zaidi...Hii ni historia fupi ya makataba wa pili wa aqaba ambao ulifanywa kati ya Mtume wa Allah na waislamu wa Madina kutoka katika makbila ya aws na Khazraj
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Nasaba ya Mtume Muhammad ﷺ toka kwa wazazi wake Mpaka kwa Nabii Ibrahim
Soma Zaidi...katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Mazazi ya Mtume MUhammad ﷺ na kupewa jina.
Soma Zaidi...Mwaka wa 10 toka kupata utume, Mtume Muhammad (S.A.W) anaanza kulingania dini nje ya Mji wa Makkah
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu miaka mitatu ya kulingania dini kwa siri na mambo yaliyojitokeza.
Soma Zaidi...Hii ni historia fupi ya kuslimu kwa Umar na kuanza kwa taswira mpya ya waislamu na uislamu katika mji wa makkah
Soma Zaidi...