Katika somo hili utakwenda kujifunza historia yaMtume Lut kutoka katika Quran
Mtume Lut(a.s) ni mpwawe Ibrahiim(a.s) waliohama pamoja yeye kutokea Iraq. Lut(a.s) alitumwa kuulingania Uislamu katika miji miwili ya Sodoma na Gomora katika nchi ya Transjodan.
Tabia ya Watu wa Miji ya Sodoma na Gomora
Jamii aliyoikuta Mtume Lut(a.s) ilikuwa imeanguka sana kimaadili. Walifikia hali ya kuwa waovu zaidi ya wanyama licha ya kuwa maumbile yao yalikuwa ya binaadamu. Walizama kwenye kufanya maovu matatu mazito kama yanavyotajwa katika Qur-an:
Na (wakumbushe Nabii) Lut; alipowaambia watu wake: “Bila shaka nyinyi mnafanya uovu (ambao) hakuna yoyote aliyekutangulieni kwa (uovu) huo katika walimwengu.(29:28)
“Je, mnawaendea wanaume, na mnawakatia njia (watu kwa kuwaua na kuwanyang’anya njiani) na mnafanya maovu katika mikusanyiko yenu?” basi halikuwa jawabu ya watu wake ila kusema: “Tuletee adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa umiongoni mwa wasemao kweli!” (29:29)”
Katika aya hizi tunafahamishwa kuwa watu wa jamii ya Lut (a.s) walikuwa wakifanya maovu mazito yafuatayo:
1) Walikuwa wakiwaendea wanaume wenzao katika kutosheleza matamanio yao ya ngono.
2) Walikuwa wakifanya uharamia na uporaji wa mali za watu.
3) Walikuwa wakifanya maovu haya hadharani na kwa ufahari.
Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu); wanahangaika ovyo. (15:72)
Je, jamii yetu hivi leo haifanyi haya na zaidi ya haya tena kwa ufahari. Hivi leo kuna mashindano ya U-miss ambayo wasichana vigoli hujitokeza jukwaani mbele ya hadhara ya watazamaji wanaume kwa wanawake wakiwa wamevaa viguo visivyo sitiri mwili. Hali ni hiyo hiyo kwenye kumbi za dansi, disko na hata kwenye sherehe za kiserikali. Na wengine wameenda mbele zaidi hata kufikia wanawake kusoma taarifa za habari katika television wakiwa uchi wa mnyama na kufikia wengine kucheza sinema za wanawake na wanaume wakifanya ngono hadharani.
Leo hii baadhi ya nchi za magharibi zimepitisha sheria yakuruhusu ndoa baina ya wanaume kwa wanaume wakifanya ushenzi ule ule wa mabaradhuli wa miji ya Sodoma na Gomora.
Nabii Lut(a.s), kama Mitume wengine walivyofanya aliwanasihi watu wake wamuamini Allah(s.w) na wamche ipasavyo na waogope adhabu yake ambayo ikimfika mtu hapana awezaye kuizuia au kuiondosha.
(Wakumbushe) alipowaambia ndugu yao, (Nabii) Lut: “Je, hamuogopi?” “Bila shaka mimi kwenu ni Mtume muaminifu.” “Basi Mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini.(26:161-163)
“Wala sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa (Mwenyezi Mungu) Mola wa walimwengu wote.” “Je, mnawaingilia wanaume katika viumbe (vyake Mwenyezi Mungu)!” “Na mnawacha alichokuumbieni Mola wenu katika wake zenu? Kweli nyinyi ni watu mnaoruka mipaka (mliyowekewa).”(26:164-166)
Na (wakumbushe) Lut alipowambia watu wake: “Je, mnaufanya uchafu, na hali mnaona?” Mnawaingilia wanaume kwa matamanio mabaya badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mfanyao ya ujinga kabisa. (27:54-55)
Pamoja na nasaha hizi nzuri zilizoambatana na hoja madhubuti, hawakumuamini Lut(a.s) ila watu wachache tu. Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu. (51:36)
Pamoja na Nabii Lut(a.s) kuwanasihi kwa maneno ya hekima na hoja zilizo wazi, watu wake hawakuwa tayari kabisa kuacha maovu yale.
Naapa kwa umri wako! Hakika wao walikuwa katika ulevi wao (wa maovu); wanahangaika ovyo. (15:72)
Walishakuwa walevi wa machafu hayo na walipania kumfukuza Nabii Lut na wale walioamini pamoja naye ambao huchukia ubaladhuli huo.
“Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila kusema: Wafukuzeni wafuasi wa Lut katika mji wenu, hao ni watu wanaojitakasa, (basi wasikae na sisi wachafu)” (27:56)
“Wakasema: Kama usipoacha, ee Lut (kutukataza haya), bila shaka utakuwa miongoni mwa wanaofukuzwa (katika nchi hii).” (26:167)
Watu wa Lut(a.s) walipokataa kabisa kuonyeka kwa nasaha na maonyo ya Nabii Lut(a.s) na badala yake wakazidi kushabikia machafu na kupania kuwafanyia ubaya waumini, Allah(s.w) alipitisha hukumu yake ya kuwanusuru waumini na kuwaangamiza makafiri.
(Wale wajumbe) wakasema: “Ewe Lut! Sisi ni wajumbe wa Mola wako (Malaika). Hawatakufikia (kwa baya lolote). Na ondoka pamoja na watu wako katika sehemu ya pingapinga la usiku.Wala yoyote miongoni mwenu asitazame nyuma. Isipokuwa mke wako (mwanamke mbaya huyo hatakufuata). Naye utampata msiba utakaowapata hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Jee, asubuhi si karibu tu? (Basi tuliza moyo wako. Umekwishafika wakatiwao wa kuangamizwa).(11:81)
Basi ilipofika amri yetu, tulifanya (ardhi hiyo iwe juu chini); juu yake kuwa chini yake, na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu (wa motoni uliyokamatana). (11:82) (Changarawe) zilizotiwa alama kwa Mola wako (kila moja kuwa ya mtu fulani). Na (adhabu) hii haiko mbali na madhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya). (11:83)
Jeshi la Allah lililotumika kuwaangamiza watu wa Lut(a.s) ni mvua ya changarawe kutokea motoni na kisha ardhi ikapinduliwa juu – chini.
Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. (48:7)
(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.s) na waumini aliokuwa nao.
(ii) Tusichelee watu katika kukemea maovu.
(iii) Kila mtu atahesabiwa na kulipwa kulingana na amali zake.
Hatafaidika mtu kwa amali njema za mwingine na wala hataadhibiwa mtu kwa matendo mabaya ya mwingine.
(iv) Tumuogope Allah(s.w), kwani adhabu yake ni kali na hakuna awezaye kujinusuru nayo inapokuja.
(v) Tujitahidi kusimamaisha Uislamu kwa mali na nafsi zetu bila ya kumchelea yeyote.
(vi) Hatma ya mapambano dhidi ya makafiri ni Waislamu kuibuka washindi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-06-26 09:56:54 Topic: visa vya Mitume Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 276
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Historia ya Mtume Al-yasa’a
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Mtume Al-yasa'a Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Musa
atika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Musa Soma Zaidi...
Hstora ya Nabii Ilyasa
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Ilyasa Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Swaleh (Salih)
Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Swalehe katikaQuran Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Lut
Katika somo hili utakwenda kujifunza historia yaMtume Lut kutoka katika Quran Soma Zaidi...
Histora ya Nabi Zakariya
Katika somo hili utakwenda ujfunza kuhusu hslistoria ya Nabi Zakariya Soma Zaidi...
Hstoria ya Nabii Yusuf
Katika makala hii utakwenda ujfunzakuhusu historiaya Nabii Yufuf katika Quran Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Idrisa
Katika somohili utakwenda kujifunza historia ya Nabii Idrisa (amani iwe juu yake) Soma Zaidi...
Hstora ya Nabii Yunus
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Yunus Soma Zaidi...
Historiaya Nabii Isa
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Historia ya Nabii Isa Soma Zaidi...
Hstora ya Nabii Yahya
Katika somo hili uatkwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Yahya Soma Zaidi...
Hstoria ya Nabi Daud
Katika somo hili utawenda ujifunza uhusu historia ya Mtume Daud Soma Zaidi...