picha

Hstora ya Nabii Ilyasa

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Ilyasa

HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)

 

Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Alitumwa kwa watu ambao walitupa mafundisho ya Mitume waliotangulia na badala yake wakawa wanaabudu Mungu- jua waliyemuita - Baal. Mtume Ilyasa(a.s) aliwaita watu wake wamwabudu Mungu Mmoja, Allah(s.w); lakini walimkadhibisha. Kwa ajili hiyo ya kukataa mafundisho ya Mtume wao, wakawa katika kundi la watakaoingia katika adhabu ya Allah(s.w). Isipokuwa kwa wale waliorejea kwa Mola wao wakajitakasa. Kwa muhtasari ujumbe wa Mtume Ilyasa(a.s) unapatikana katika aya zifuatazo:

 


"Na hakika Ilyas alikuwa miongoni mwa Mitume. (Wakumbushe) Alipowaambia watu wake: "Oh! Hamuogopi?" "Mnamuomba (na kumuabudu) Baal na mnamuacha aliye Mbora wa waumbaji (na ndiye Muumbaji peke yake)." "Mwenyezi Mungu, Mola wenu na Mola wa wazee wenu wa mwanzo!" Wakamkadhibisha. Basi bila shaka watarudishwa (adhabuni). Isipokuwa waja wa

 

Mwenyezi Mungu waliosafishwa (na Mwenyezi Mungu). Na tumemuachia (sifa nzuri) kwa (watu wote) Amani kwa Ilyas" (37:123-130).

 

Katika historia

 

Alyasa katika Uislamu

Alyasa (Kiarabu: اليسع, Alyasaʿ) ni nabii wa Mungu aliyepelekwa kuwaongoza Wana wa Israeli. Katika Quran, Alyasa anatajwa mara mbili kama nabii mwenye heshima na mara zote akiwa pamoja na manabii wenzake. Anaheshimiwa kama mrithi wa kinabii wa Ilyas (Elia).

 

Kutajwa katika Quran

Jina la Alyasa limetajwa mara mbili katika Al-An'am 6:86 na Sad 38:48. Aya hizo zinamtaja kuwa "amepewa neema" na "miongoni mwa wateule":

"Na Ismail na Alyasa na Yunus, na Lut; na kila mmoja tulimneemesha juu ya walimwengu." — Al-An'am 6:86

"Na kumbuka watumishi wetu Ismail, Alyasa, na Dhul-Kifl, kila mmoja wao ni wema wa kweli." — Sad 38:48

 

Makaburi Yanayodaiwa

Baadhi ya Waislamu wanaamini kaburi la Alyasa lipo Al-Awjam, Saudi Arabia, lakini liliondolewa na Serikali ya Saudi kwa sababu heshima hiyo haikubaliani na vuguvugu la Wahhabi. Kaburi lingine linadaiwa kuwa lipo katika wilaya ya Eğil, Mkoa wa Diyarbakir, Uturuki. Kituo hicho kilihamishwa usiku kabla ya eneo hilo kufurika mwaka 1994 na mwili wa nabii huyo ulihamishiwa kwenye kilima kinachoangalia tambarare iliyojaa maji.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-06-27 16:32:38 Topic: visa vya Mitume Main: Masomo File: Download PDF Views 1509

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 web hosting     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zinazofanana:

Histora ya Nabi Zakariya

Katika somo hili utakwenda ujfunza kuhusu hslistoria ya Nabi Zakariya

Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Ismail katika quran

KKatika somohili utakwenda kujifunzahistoriaya Mtume Ismail Mtoto wa Nabii Ibrahim

Soma Zaidi...
Historiaya Nabii Isa

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Historia ya Nabii Isa

Soma Zaidi...
Hstora ya Nabii Yahya

Katika somo hili uatkwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Yahya

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Lut

Katika somo hili utakwenda kujifunza historia yaMtume Lut kutoka katika Quran

Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Idrisa

Katika somohili utakwenda kujifunza historia ya Nabii Idrisa (amani iwe juu yake)

Soma Zaidi...