Adhkari unazoweza kuomba kila siku

Adhkari unazoweza kuomba kila siku

Hapa nitakuletea baadhi tu ya adhkari ambazo ni muhimu kwa muislamu

ADHKARI MBALIMBALI NA DUA
Hapa tutajifunza dua mbalimbali ambazo ni adhkari. Tutajifunza pia na faida zake kama Mtume صلّي الله عليه وسلّم alivyozungumza na masahaba zake. 1.amesema Mtume"‏ أَفْضَلُ الذِّكْرِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ الْحَمْدُ لِلَّهِ ‏"‏ “bora ya dhikir ni kusema Lā ilāha illallāh na bora ya dua ni kusema Al-ḥamdulillāh” (amepokea Tirmidh).

2.Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ مَا مِنْ عَبْدٍ يَقُولُ فِي صَبَاحِ كُلِّ يَوْمٍ وَمَسَاءِ كُلِّ لَيْلَةٍ بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لاَ يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الأَرْضِ وَلاَ فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ فَيَضُرُّهُ شَيْءٌ ‏" “Mja yeyote atakayesema ‘Bismillāh, alladhi lā yaḍurru ma`a ismihi shai'un fil-arḍi wa lā fis-samā', wa huwas-Samī`ul `Alīm’ mara tatu kila asubuhi na jioni hatadhuriwa na kitu chochote” (Amepokea Tirmidh).

3.mtume amesema "‏ مَنْ قَالَ حِينَ يُمْسِي رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا وَبِالإِسْلاَمِ دِينًا وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُرْضِيَهُ ‏"‏ “Mwenye kusema jioni ‘Raḍītu billāhi rabban wabil-Islāmi dīnan wa bi-Muḥammadin nabiyyan’ itakuwa ni haki kwa Allah kumridhia” (Amepokea tirmidh).

4.Mtume alimwambia al-baraa IBN ‘Aazib kuwa “أَلاَ أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ تَقُولُهَا إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَإِنْ مُتَّ مِنْ لَيْلَتِكَ مُتَّ عَلَى الْفِطْرَةِ وَإِنْ أَصْبَحْتَ أَصْبَحْتَ وَقَدْ أَصَبْتَ خَيْرًا تَقُولُ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ لاَ مَلْجَأَ وَلاَ مَنْجَا مِنْكَ إِلاَّ إِلَيْكَ آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ وَبِنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ ‏"‏ ‏

“je nikufundishe maneno utakayoyasema pindi atakapoliendea tandiko lako (kulala) na kama utakufa utakufa katika fitrah (uislamu) na ukiamka asubhi utakuwa umepambaukiwa katika kheri? Utasema ‘'Allāhumma innī aslamtu nafsī ilaika wa wajjahtu wajhī ilaika, wa fawwaḍtu amrī ilaika, raghbatan wa rahbatan ilaika wa alja'tu ẓahrī ilaika, lā malja'a [wa lā manjā] minka illā ilaik. Āmantu bikitābikal-ladhī anzalta wa binabiyyikal-ladhī arsalt’ (Amepokea Tirmidh).

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views: 3008

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 ai web app     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Fadhila za udhu yaani faida za udhu

Katika makala hii utajifunza faida za kuwa na udhu

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba

Nini kilichangia ongezeko la uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba.

Soma Zaidi...
Dua za kumuomba Allah wakati wa shida na tabu ama matatizo

Post hii inakwenda kukufundisha dua ambazo ni muhimu kuzisoma wakayi wa shida na taabu.

Soma Zaidi...
Sura za kujikinga na Uchawi na mashetani

Post hii itakwenda kukufundisha sura katika Quran ambazo ni kinga dhidi ya Wachawi, uchawi na Masheitwani.

Soma Zaidi...