الحديث الخامس والعشرون
"ذهب أهل الدثور بالأجور "
عن أبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ ناساً من أَصْحابِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالوا لِلنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: يا رسولَ اللهِ، ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ، يُصَلُّونَ كما نُصَلِّي، ويَصُومُونَ كما نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ. قَالَ: ((أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ ؟ إنَّ بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَةً)). قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ:
((أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abu Dharr رضي الله عنه ambaye amesema:
Baadhi ya Maswahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم walimuambia Mtume صلى الله عليه وسلم : Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, wenye mali wameondoka na fungu (jaza) kubwa, wanaswali kama sisi, wanafunga kama sisi, na wanatoa sadaka ya ziyada ya mali zao. Mtume صلى الله عليه وسلم akasema: Mwenyeezi Mungu hajakufanyieni vitu kwa ajili yenu kutoa sadaka? (Basi jueni) Hakika kila Tasbihi (Subhana Allah) ni sadaka, kila Takbiri (Allahu Akbar) ni sadaka, kila Tahmidi (AlhamduliLlah) ni sadaka, na kila Tahlili (Laa ilaaha illa Allaah) ni sadaka, na kulingania jambo jema ni sadaka, na kukataza mabaya ni sadaka na katika kujamii (wake zenu) kila mmoja katika nyinyi ni sadaka. Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtumeصلى الله عليه وسل mtu anapojitosheleza shahawa yake atapata malipo kwa ajili yake? Akasema صلى الله عليه وسلم : Mnadhani ingekuwa anajitosheleza kwa njia ya haramu angelipata dhambi? Na hivyo ikiwa kafanya kwa njia ya halali basi atapata thawabu.
Imesimuliwa na Muslim
Umeionaje Makala hii.. ?
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.
Soma Zaidi...Download kitabu hiki na upate kusoma zaidi ya dua 120, pamoja na darsa mbalimbali za dini ya kiislamu.
Soma Zaidi...Katika hadithi hii utakwenda kujifunza hekma ya kuangalia watu walio chini yako na sio walio juu yako
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 1.
Soma Zaidi...Nini kilichangia ongezeko la uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba.
Soma Zaidi...