الحديث الثامن والثلاثون
"من عادى لي وليا فقد آذنته بالحرب"
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال: قال رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : ((إنَّ الله تَعالَى قَال : مَنْ عَادَى لي وَلِيّاً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُهُ عَلَيْهِ، وَلا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إلَيَّ بِالنَّوَافِلٍ حَتَّى أُحِبَّهُ، فإذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بهِ، وَيَدَهُ الّتي يَبْطِشُ بهَا، وَرِجْلَهُ الّتي يَمْشي بِهَا، وَلَئِنْ سَأَلِني لأعْطِيَنَّهُ، ولَئِن اسْتَعَاذَنِي لأُعِيذَنَّهُ ))
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 38 ANAYEONYESHA UADUI KWA RAFIKI YANGU MTIIFU NINATANGAZA VITA DHIDI YAKE
Kutoka kwa Abu Hurayra رضي الله عنه ambaye amesema kuwa Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: Allaah سبحانه وتعالى kasema: Anayeonyesha uadui kwa Walii Wangu (rafiki wa karibu, yaani mja mtiifu aliye karibu naye) , nitatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote ninachokipenda zaidi kama zile amali nilizomuwajibisha, na mja Wangu anazidi kukaribia Kwangu kwa amali njema zisizokuwa wajibu ili nimpende. Ninapompenda, Ninakuwa masikio yake anayosikilizia (yaani Allah atamjaalia asikie mazuri kama Qur’an, Dhikr, Mawaidha n.k. Na sio Muziki, Masengenyo, na Machafu mengine), macho yake anayoonea (yaani Allah atamfanya macho yake yawe yanatazama yale ya kheri), mikono yake ambayo anakamatia (Allah atafanya mikono yake ikamate vile vya halali na kufanya yale yanayomridhisha Allah), miguu yake anayoendea (na Allah ataifanya miguu yake isitembee kuyaendea ila yale mema, ya kheri na Atakayoridhika nayo Yeye Allah). Anaponiomba (kitu) bila shaka Ninampa, na anaponiomba ulinzi bila shaka Nitamlinda.
Imesimuliwa na Al-Bukhari
Umeionaje Makala hii.. ?
DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu “LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha adabu zinazotakikana kwa mwenye kuomba dua.
Soma Zaidi...Hii ni historia ya uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina. Yaani wafuasi wa wale wafuasi wa Masahaba
Soma Zaidi...Kwenye Quran kuna duaambazo Allah ametufundisha tuziombe kwa ajili ya wazazi, familia na kwa ajili yetu wenyewe.
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صل?...
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha dua ambazo ni muhimu kuzisoma wakayi wa shida na taabu.
Soma Zaidi...