Katika somo hili uatwkeda kujifunza zaidi kuhusu widget, maana yake, aia zake na kazi zake kwneye flutter.
Widget ni nini?
Widget ni kipengele muhimu katika Flutter ambacho kinaunda sehemu ya interface ya mtumiaji yaani uso wa matumizii kwenye app yako.. Kimsingi, kila kitu ambacho unaona kwenye programu ya Flutter, kama vile vichupo, vitufe, maandishi, na zaidi, vyote ni widget. Widgets zinaweza kuwa vitu vya msingi kama vile vitufe na maandishi, au zinaweza kuwa muundo wa kina zaidi kama vile orodha au gridi.
Katika Flutter, kuna aina mbili za widgets: StatefulWidget na StatelessWidget.
StatelessWidget: Hii ni widget ambayo haitoi uwezo wa kubadilisha hali yake mara baada ya kujengwa. Kwa mfano, maandishi ambayo hayabadiliki baada ya kuundwa ni StatelessWidget. Kama tulivyoona hapo somo lililopita neno Bongoclass
Hapa kuna mifano kumi ya StatelessWidget katika Flutter:
Hizi ni baadhi ya mifano ya StatelessWidget ambayo inaweza kutumika kujenga interface ya mtumiaji katika programu za Flutter.
StatefulWidget: Hii ni widget ambayo inaweza kubadilika au kubadilishwa baada ya kujengwa. Kwa mfano, kipengele ambacho kinaweza kubadili rangi au maudhui yake baada ya tukio fulani, kama vile kubofya kifungo, ni StatefulWidget. Mfano katika somo la pili tuliona app ambayo ukibofya batani namba zinajiongeza.
Hapa kuna mifano kumi ya StatefulWidget katika Flutter:
Hizi ni baadhi ya mifano ya StatefulWidget ambayo inaweza kutumika kujenga interface ya mtumiaji yenye utendaji mzuri katika programu za Flutter.
Jinsi ya kuandika widget:
child: Container(
height: 50.0,
),
child: Container(
height,
),
child: Container(
height: 50.0,
),
Hapo child ni property ambapo Container ni widget, pia widget container ni value ya property child. Na height ni property ya widget container ambapo 5.0 ni value ya property widget.
Hapo chini nimekuletea mfano wa widget,ambazo zipo katika aina zote mbili. Pia nimekuwekea widget zenye children. Tutakuja kujifunza zaidi tutakapokuwa tunasoma hizi widget moja moja.
Mfano wa app:
Hapa nakuletea app ambayo ina aina zote mbili za widget.
import 'package:flutter/material.dart';
void main() {
runApp(
MaterialApp(
home: Scaffold(
appBar: AppBar(
title: Text('Bongoclass'),
backgroundColor: Colors.blue,
),
body: Center(
child: Text("Mafunzo ya flutter"),
),
drawer: Drawer(),
floatingActionButton: FloatingActionButton(
onPressed: () {},
child: Icon(Icons.add),
),
),
),
);
}
Kuelewa na kutumia Widgets ni muhimu sana katika maendeleo ya programu za Flutter, kwani husaidia kujenga interface ya mtumiaji iliyoboreshwa na yenye utendaji mzuri.
Statefull na stateless widget kwenye app moja:
App inaweza kuwa na statefullwidget na statelesswidget. Sasa inatakiwa useme wakati unapotengeneza class za hizo widget. Useme kuwa widget hizo ni stateless ama statefull.
Mfano:1
import 'package:flutter/material.dart';
void main() {
runApp(
MaterialApp(
home: Scaffold(
backgroundColor: Colors.blue,
),
),
);
}
Code hizo zitaprint app ambayo ina ukrasa m">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tutakwend akuyaona baadhi ya maeneo muhimu ya kuanzia kuyajuwa kwa ajili ya course ya flutter kwneye android studio.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili app icon kwenye app ya Android na iphone kwenye flutter.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya AppBar. Hata tutaona inavyofanya kazi na baadhi ya property zake.
Soma Zaidi...Katika Flutter, Text Widget ni kipengele kinachotumiwa kuonyesha maandishi kwenye programu. Kwa kawaida, hutumiwa kama sehemu ya muundo wa UI ya programu za Flutter.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jisni ya kuweka drawer menu kwenye app ya flutter.
Soma Zaidi...Somo hili litakufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya ku sign app ya android kwenye flutter
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jisni ya kubadili package name ama app id kwenye Android app na Bundle Identifier kwenye iOS app na taarifa nyinginezo.
Soma Zaidi...Katika somo hili uatakwenda kujifunz ajinsi ya kutumia batani na kuweka maumbo mbalimbali ya batani.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia icon yaani kuweka icon kwenye App ya flutter.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunzajinsi ya kubadilisha, jinala App yaani App name.
Soma Zaidi...