Post hii inahusu zaidi dalili za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ingawa sio watu wote wenye dalili kama hizi Wana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo Ila zikitokea mtu anapaswa
1. Maumivu makali wakati wa kujamiiana.
Kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo bakteria tayari wameshambulia sehemu mbalimbali kwenye kibofu Cha mkojo na sehemu zinazozunguka kama vile via vya uzazi kwa hiyo wakati wa kujamiiana mtu anapata maumivu hali hii uwatokea hasa watu wale ambao maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo yanapokuwa yamesambaa sana na yamekaa mda mrefu.kwa hiyo tunapaswa kuhakikisha kuwa tunaangalia afya zetu mara kwa mara Ili kuepusha matatizo makubwa yanayoweza kujitokeza.
2.Mtu mwenye uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo anasikia maumivu wakati wa kukojoa.
Hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa bakteria ambao uingia kwenye kibofu Cha mkojo na kusababisha maambukizi na pengine kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe na uharibifu wowote ambao umeshafanyika kwenye kibofu Cha mkojo kwa hiyo wakati wa kukojoa mkojo ugusa sehemu ya majeraha na kusababisha maumivu wakati wa kukojoa kwa hiyo basi baada ya kujua hayo yote tunapaswa kutumia madawa ambayo yanatibu ugonjwa huu kwa sababu yapo na wengi wamepona na tusiyameze bila ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.
3. Kuwepo kwa damu kwenye mkojo.
Hali hii utokea kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo na Maambukizi hayo yamekuwa makubwa zaidi na kusababisha kuvuja damu kwenye sehemu mbalimbali za kibofu Cha mkojo ndio maana mkojo utoka n damu au uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo inakuwa unavuja damu ndo maana mkojo utoka pamoja na damu, hali hii sio nzuri inaweza kuleta madhara makubwa zaidi kwa hiyo mgonjwa anapaswa kuwaona wataalamu wa afya kwa msaada zaidi kwa sababu magonjwa haya yanatibika na dawa zipo hospitalini.
4. Maumivu makali kwenye Tumbo la chini.
Kwa wakati mwingine Kunakuwepo na maumivu kwenye sehemu ya tumbo la chini , hali hii usababishwa na Maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo ambapo kibofu Cha mkojo kinakuwa kimeshambuliwa na bakteria ambapo maumivu huwa mengi kwenye tumbo la chini.
5. Mkojo kutoa harufu mbaya.
Watu wenye matatizo ya uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, mkojo wao utoa harufu mbaya hali hii ni kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo ambayo usababisha harufu ya mkojo kubadilika na kuwa mbaya kwa hiyo pengine mkojo unaweza kuwa na usaha ambao usababisha mkojo kutoa harufu mbaya. Kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi mgonjwa inabidi kwenda hospitalini kwa matibabu zaidi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowPosti hii inahusu zaidi dalili za fangasi uken, hizi ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la fangasi uken.
Soma Zaidi...Watoto wachanga ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano, watoto hawa hushambulia na maginjwa mara kwa mara na kusababisha ukuaji wao kuwa dunk,
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kufunga kwa ulimi (Tongue-tie) kuanzia Mtoto anavyo zalia mpaka navyokua ni hali inayotokea wakati wa kuzaliwa ambayo kitaalamu hujulikana kama ankyloglossia.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya koo, ni ugonjwa unaoshambulia sana sehemu ya koo la hewa, na na huwa na dalili zake kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi kwenye mfupa ambao kitaalamu hujulikana Kama
Soma Zaidi...Kuzama hufafanuliwa kama mchakato unaosababisha upungufu mkubwa wa kupumua kutokana na kuzamishwa kwenye chombo cha kuogelea (kioevu). Kuzama hurejelea tukio ambalo njia ya hewa ya mtoto huzamishwa kwenye kioevu, na kusababisha kuharibika kwa kupumua.
Soma Zaidi...Hii ni huduma ya kwanza kwa aliyeshambuliwa na pumu katika mazingira ambayo ni mbali na kituo cha afya, na hakuna dawa.
Soma Zaidi...Minyoo ni katika viume wanyonyaji, wanaoishi katika miili ya viumbe hai na kujipatia chakula humo. Minyoo wanaweza kuishi kwenye maeneo yenye majimaji kama kwenye maji, ndani ya viumembe hai kama mtu, ngombe, ngure na paka. Minyoo pia wanaweza kuishi kwen
Soma Zaidi...Zipo aina nyingi za fantasy ambazo ni rahisi kuathiri binadamu. Wipe ambao haiathiri mdomo, nyayo, shemu za siri na kwenye ngozi.
Soma Zaidi...