picha

benki za kiislamu na njia zake za kuingiza kipato

Benki za KiislamuBenki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sio ule wa riba.

benki za kiislamu na njia zake za kuingiza kipato

Benki za Kiislamu
Benki za Kiislamu ambazo hutoa huduma kama benki nyingine zinaendeshwa katika msingi wa biashara na sio ule wa riba. Benki za Kiislamu badala ya kukopesha kwa riba, hutumia rasilimali zake kwa zenyewe kujihusisha katika uzalishaji kwa kufuata misingi inayokubalika katika Uislamu. Miongoni mwa misingi inayokubalika kwa Muislamu au Benki ya Kiislamu kuingiza fedha zake katika miradi ya biashara au uzalishaji ni hii ifuatayo:


(i)Mudharabah
Mudharabah ni makubaliano kati ya watu wawili au zaidi ambapo mmoja au zaidi kati ya hao anatoa mtaji na mwingine hushiriki kwa ukamilifu katika kuendesha na kuongoza mradi wa uchumi. Faida itakayopatikana katika mradi huo itagawanywa kulingana na makubaliano yao. Hasara itakayotokana na mradi huo itakuwa ni ya mwenye kutoa mtaji. Wengine hawatoi chochote kusaidia hasara kwa sababu wameshatoa mchango wao wa hasara hiyo kwa jasho walilolitoa katika shughuli ambayo haikuzaa matunda bali hasara.



Benki za Kiislamu zinaingiza fedha zake katika miradi ya uchumi kwa njia hii ya Mudharabah ambapo benki hutoa mtaji kwa ajili ya miradi mbali mbali ya uchumi kwa mapatano ya kupata kiasi (asilimia) fulani cha faida itakayopatikana na kuwa tayari kulipa hasara itakayopatikan a.


(ii)Musharikah
Musharikah ni ushiriki kati ya watu wawili ambapo, tofauti na Mudharabah wote wawili wanachangia mtaji na kushiriki katika uendeshaji wa shughuli ya kiuchumi, lakini si lazima watoe hisa sawa sawa, kwa makubaliano ya kugawana faida na hasara kulingana na kiasi cha hisa alichotoa kila mmoja wao. Kwa mtindo huu wa “Musharikah” Benki ya Kiislamu inaingia katika kuchangia mtaji, kuendesha na kusimamia mradi wa uchumi na watagawana (faida au hasara) kulingana na kiasi cha mtaji kila mmoja alichotoa.



(iii)Ijara-Uara wa Iktina
Huu ni utaratibu mwingine unaokubalika kisheria ambapo mtu au benki inatumia fedha zake katika kukodi vitu kama vile magari, majumba, ardhi, na kadhalika, ambavyo vikifanyiwa kazi huzalisha mali na kutoa faida. Benki za Kiislamu hujipatia faida kubwa kutokana na mtindo huu.



(iv)Murabah
Huu ni utaratibu unaotumiwa katika kununua bidhaa kwa wingi kwa ajili ya kuwauzia wafanya biashara ambao waliofikiana kuwa bidhaa hizo zinunuliwe kwa ajili yao. Benki kutokana na uwezo wake inapanga na wafanya biashara kuwa inunue bidhaa nyingi kutoka ndani na nje ya nchi kwa jina lake kisha iwauzie wafanyabiashara hao kwa bei itakayoipatia benki faida. Pia benki kwa mtindo huu inaweza kununua mazao ya wakulima na kuyauza kwa walaji kwa faida.



(v)Muqaradha
Mtindo huu wa Muqaradha humruhusu mtu au benki kununua “share” au “bonds” katika kampuni ya uzalishaji kwa mapatano ya kugawana faida au hasara kulingana na kiasi cha “share”.



Kwa kufuata mitindo hii katika kuingiza fedha zake katika miradi ya uchumi, Benki za Kiislamu hupata faida kubwa hata zaidi ya kipato cha riba kinachopatikana katika benki za riba. Benki za Kiislamu nazo hugawa faida inayopatikana kwa wateja wake walioweka fedha zao kwenye benki.



Uzuri wa benki za Kiislamu
Pamoja na benki za Kiislamu kutoa huduma zinazotolewa na kila benki kama tulivyoziorodhesha huko nyuma, kuna faida za ziada zinazopatikana kutokana na benki hizi kama ifuatavyo:



Kwanza benki za Kiislamu huiokoa jamii na uchumi wake na madhara yote yanayosababishwa na riba.


Pili, Benki za Kiislamu huwaingiza katika uchumi na kuwainua hata wale ambao hawana hata rasilimali yoyote kwa mtindo wa Mudharabah. Hivyo ni kwamba, benki zinazoendeshwa kwa mikopo ya riba, haziwezi kukopesha fedha zake kwa mtu yeyote asiye na rasilimali yenye thamani sawa au zaidi ya mkopo ili atakaposhindwa kulipa ifilisiwe rasilimali hiyo. Kwa mtindo huu wa mikopo ya riba, ni matajiri tu wanaopata mikopo ya benki na masikini wasio na rasilimali yoyote huachwa hivyo hivyo na umasikini wao bila ya msaada kutoka benki wa kuwainua kiuchumi.



Tatu, benki za Kiislamu huinua uchumi wa jamii, kutokana na umakini na tahadhari kubwa zinazochukua katika kuchagua na kuendesha miradi mbali mbali ya uchumi. Kwa kuwa benki zenyewe zinajiingiza katika uchumi, zinahakikisha kuwa miradi zitakazoichagua ni ile yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha faida kubwa na yenye uwezekano mdogo wa kusababisha hasara.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1657

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Ni nini maana ya swala

Post hii inakwenda kukugundisha kuhusu maana halisi ya ibada ya swala.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa

Post hii itakufundisha taratibu za kuzika maiti wa kiislamu hatuwa kwa hatuwa.

Soma Zaidi...
Uzuri wa Benki za kiislamu

Kwa nini benki za kiislamu ni bora kuliko benki nyingine?

Soma Zaidi...
Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu

kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah.

Soma Zaidi...
Faida na umuhimu wa ndoa katika jamii

Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi

Soma Zaidi...
Zijuwe funga za kafara na jinsi ya kuzigunga

Post hii itakufundisha kuhusu funga za kafara, zinavyotokea na na jinsi ya kuzifunga.

Soma Zaidi...
Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga.

Soma Zaidi...
Twahara na umuhimu wake katika uislamu

Katika post hii utajifunza maana ya twahara kiligha na kishria. Pia utajifunza umuhimu wake

Soma Zaidi...