Mali yenye kuchangiwa mtaji kwa hisa
Mtu akishaamua kuuza hisa (share) kwa watu wengine kwa ajili ya mali fulani katika sheria ya Kiislamu anapoteza umilikaji wa mali wa mtu mmoja. Kuuza hisa kwa wengine kwa maana nyingine ni kukaribisha watu wengine kushiriki katika umilikaji wa mali ile. Nafasi ya mtu katika kumiliki mali hiyo itategemea idadi ya hisa alizonazo katika mali ile. Wenye hisa inabidi washirikiane katika faida na hasara pamoja na gharama za uendeshaji.
Faida anazopata atakayekuwa mwenye kumiliki mali
Zipo faida kadhaa ambazo atakayekuwa mwenye kumiliki mali huzipata kwa kufuata ushirika katika biashara, mtaji na faida (Shared Equity and rental) badala ya kupata mikopo ya biashara yenye riba. Faida kubwa atakayopata ni fadhila za Allah (s.w.) kwa kule kuepuka kwake kutoa riba kwa mkopo atakaopata. Tunajifunza katika Hadithi za Mtume (s.a.w.) kuwa laana ya Allah (s.w.) huwafikia wote wanaohusika na riba (mtoaji, mpokeaji, shahidi). Hata hivyo kuna faida nyingine ambazo anaweza kuzipata:
(i) Atakayekuwa mwenye kumiliki mali kwa kutochukuwa mkopo wenye masharti ya riba hujiepusha kabisa na hatari ya kunyangβanywa mali yake (aliyoweka rahani) akishindwa kutimiza masharti yake.
(ii)Fedha ambayo angeitoa kama riba kwa ajili ya mkopo atabaki nayo na kutumia kwa shughuli nyingine kuendeshea maisha yake.
(iii)Atakuwa na uhakika wa kupata sehemu halali ya faida inayotokana na mali hiyo (kama ipo). Kadhalika kama ikitokea hasara haitamlazimu kubeba mzigo wote wa hasara kwani ushirika katika biashara huhusisha vile vile umuhimu wa kugawana hasara itokeapo.
Faida kwa wenye kununua hisa
Mwenye kununua hisa huchangia katika mtaji. Naye huepuka ghadhabu za Allah (s.w.) za utoaji mkopo kwa riba. Zaidi ya haya hupata faida zifuatazo:
(i) Hupata sehemu ya faida itokanayo na mali hiyo kulingana na mchango wake kwenye biashara (idadi ya hisa alizonazo).
(ii) Huwa na sauti kwenye mali kwani naye pia ni mwenye kumiliki mali ile mpaka atakapouza hisa zake. Isitoshe hutoa kiwango kidogo kujipatia haki ya kumiliki ukilinganisha na mtaji mzima.
Kwa ujumla jamii nzima itanufaika kwa kuacha mfumo wa mikopo kwa riba na kuhimiza watu kufanya ushirika katika biashara. Ilivyo waliokopeshana kwa riba hawawi katika uhusiano mzuri kiroho. Aliyekopeshwa ilimbidi kufanya hivyo kutokana na shida aliyokuwa nayo. Kutoa kwake riba anakufanya kwa kuwa anafahamu hatari za kutofanya hivyo (kupoteza mali yake) ingawa kitendo hicho kinamuuma sana rohoni. Hivyo urafiki kati ya mkopeshaji na mkopeshwaji huwa ni wa kinafiki. Jambo hili ni wazi sana katika jamii ya dunia ya sasa. Hebu fikiria athari za mikopo hii kwa nchi masikini duniani. Ni mara nyingi nchi masikini zimekuwa zikipiga kelele aidha kupunguziwa au kufutiwa kabisa baadhi ya madeni yao. Sehemu kubwa ya madeni hayo ni limbikizo la riba la miaka mingi.
Hivyo Uislamu unapiga vita riba kutokana na madhara yake kibinafsi, kitaifa na kimataifa. Aidha Uislamu unahimiza ushirikiano katika biashara kama ufumbuzi wa tatizo la riba.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 533
Sponsored links
π1 Kitau cha Fiqh
π2 Madrasa kiganjani
π3 Kitabu cha Afya
π4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π5 kitabu cha Simulizi
π6 Simulizi za Hadithi Audio
Sifa za imamu wa swala ya jamaa
Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii. Soma Zaidi...
Swala ya jamaa.
Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa. Soma Zaidi...
Siku ya idi al-fitir na namna ya kusherekea idi
Soma Zaidi...
Taratibu za ndoa ya kiislamu, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...
Twahara
FIQH 1. Soma Zaidi...
Suluhu na kupatanisha kati ya mke na mume
Soma Zaidi...
Sanda ya mtoto
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Maana ya Ndoa na Faida zake katika jamii
4. Soma Zaidi...
JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka. Soma Zaidi...
Ni kwa nini lengo la Funga na swaumu halifikiwi na wafungaji?
Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi? Soma Zaidi...
Mda wa mwisho wa kula daku mwezi wa ramadhani
Post hii fupi itakwenda kukujulisha utaratibu wa kula daku. Soma Zaidi...
Wanaowajibika kuhijji
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...