image

kanunu na sheria za biashara katika islamu

kanunu na sheria za biashara katika islamu

Biashara haramu



Biashara inaweza kuwa haramu kwa namna mbili: kwanza kwa kutofuata misingi ya halali iliyowekwa na Allah (s.w). Pili, kuna biashara ambayo moja kwa moja imeharamishwa hata kama misingi ya halali itafuatwa. Kwa maana nyingine kuna biashara ambazo zimeharamishwa katika nafsi yake yenyewe. Katika kipengele hiki tutaorodhesha biashara ambazo zimeharamishwa moja kwa moja katika nafsi yake na Hadithi mbali mbali za Mtume (s.a.w).


(i)Muzabanah
Ni kunufaika kibiashara kutokana na matatizo ya watu wengine. Ni haramu kufaidi shida ya mwengine katika biashara. Uislamu unataka mwenye shida asaidiwe na wala asikandamizwe kutokana na shida yake. Biashara ya Muzabanah imeharamishwa kwa muuzaji na mnunuzi. Uislamu unasisitiza kuwa kinachouzwa na kinachobadilishwa nacho ni lazima kifahamike kwa mnunuzi na muuzaji.



(ii)Mu’awamah
Huu ni uuzaji wa matunda, nafaka, na mazao mengine ya shambani kabla ya kukomaa kiasi cha kufaa kuliwa; na ni haramu kama inavyosisitizwa katika Hadithi zifu atazo:
Abdullah bin Umar ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) ameharamisha kuuza matunda sham bani mpaka yaive. Ameharamisha kwa muuzaji na mnunuzi (wamekubaliana Bukhari na Muslim). Na katika maelezo ya Muslim: (Mtume) aliharamisha kuuza tende mpaka ziive na nafaka mpaka ziwe nyeupe na zisiwe zenye kudhuriwa tena na madhara mbali mbali.



Jabir ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharamisha kuuza (kwa matunda yangali mtini) kwa kipindi cha miaka, na ameamrisha kungojea kwanza yawe tayari (kiasi cha kutoweza kudhuriwa na chochote). (Muslim).



(iii)Hablul-Habalah
Kuuza kilichotumboni kabla hakijazaliwa. Kwa mfano kuuza mimba ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, ngamia, n.k ni haramu. Tunafahamishwa katika Hadithi ifuatayo: Ibn Umar ameeleza kuw a Mtume Mtukufu ameharam isha mauzo ya Habalul-Habalah; na ni uuzaji waliokuwa wakiufanya watu majahili. Mtu alikuwa akinunua ngamia mpaka ngamia jike lishike mimba na mpaka hicho nacho katika tumbo la uzazi kiwe na mimba. (Bukhari na Mus-lim).



Jambo linalosisitizwa katika Hadithi hii ni kwamba imeharamishwa kuuza mimba kwani ni jambo ambalo halina uhakika kabisa. Ajuaye na mwenye uhakika wa kuzaliwa au kutozaliwa kilichomo tumboni ni Allah (s.w) peke yake. Kwa hiyo uuzaji wa mimba ni uuzaji wa pata-potea (uuzaji hewa).



(iv)Uuzaji wa bidhaa kabla hazijamfikia mnunuzi ni h aram,
Ununuzi au uuzaji hauhusiki mpaka mnunuzi ashuhudie bidhaa anazouziwa. Hivyo ndivyo tunavyofahamishwa katika Hadithi ifu atayo:
Ibn Abbas ameeleza: “Katika mauzo aliyoyaharamisha Mtume (s.a.w) ni mauzo ya chakula mpaka yawe mikononi mwa mnunuzi…” (Bukhari na Muslim).
Msisitizo wa Hadithi hii ni kwamba mtu asiuze kitu ambacho hajakishuhudia machoni mwake au machoni mwa mwakilishi wake.



(v)Uuzaji wa bidhaa njiani kabla ya wauzaji kufikisha bidhaa sokoni.
Wakati mwingine wafanya biashara hufanya ujanja kwa kuteka nyara bidhaa njiani kabla hazijaingia sokoni ili kuwaghilibu na kuwapumbaza wauzaji ambao hawajajua bei halisi ya bidhaa ile sokoni. Ununuzi wa namna hii ni ulanguzi na umeharamishwa katika Uislamu kama inavyosisitizwa katika Hadithi zifu atazo:


Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Usimfuate mfanya biashara wa nafaka mkakutana naye njiani kabla (ya kuingia sokoni). Na endapo atanunua kutoka kwake-atakapoingia sokoni na kujua hali halisi ya soko ana haki ya kukataa mauziano ya awali. (Muslim, Bukhari).


Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Usikutane (usiteke nyara) bidhaa njiani mpaka zitakapofikishwa sokoni.” (Bukhari na Muslim)



Kununua bidhaa iliyonunuliwa na mwingine kwa kulipa bei kubwa zaidi au kwa sababu nyinginezo ni haramu kama inavyobainishwa katika Hadithi zifu atazo:
Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Hapana mapatano ya atakayenunua kitu yatayofanyika baada ya mwenzake kununua na hapana atakayemchumbia ambaye ameshachumbiwa na mwenzake (ndugu yake) mpaka apate ruhusa kutoka kwake (huyo) aliyeanza na kupatana bei au aliyeanza kuchumbia.” (Muslim).



Kinachosisitizwa katika Hadithi hii ni kwamba, Muislamu haruhusiwi kununua bidhaa iliyonunuliwa na mwingine. Mara nyingine kwa sababu ya husuda au uroho matajiri huweza kuwashawishi watu wenye uroho kama wao wakaamua kuvunja mkataba wa mauzo uliofanyika hapo awali ili apate bei kubwa kwa huyu mteja aliyejitokeza baada ya mauzo kwa yule mteja wa kwanza.



(vi) Kuuza maji au majani ambayo mtu hakuyagharamikia chochote imekatazwa katika Hadithi zifuatazo:
Jabir amesimulia kuwa Mtume wa Allah amekataza (ameharam isha) kuuza maji ya asili. (Muslim).


Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Majani ya asili hayatauzwa ili kununua malisho yaliyomo. (Bukhari na Muslim).



Hadithi hizi zinatufundisha kuwa mali asili kama maji, majani, miti ya porini (n.k.) ni haki ya kila mwanaadamu kwa hiyo hapana mwenye haki ya kuzuia mali ya asili na kuifanya yake na kuwauzia watu wengie. Bali kama mali asili imeshughulikiwa ndio ifae kutumika, itajuzu mwenye kuishughulikia awe na haki ya kudai arudishiwe gharama alizozitoa katika shughuli hiyo. Kama gharama za bomba, na mashine ya kusukumia maji na kadhalika.
Lakini kuyauza maji ya chemchem ya asili au mto ni ha ram u.



(vii)Uuzaji wa samaki aliyeko majini, uuzaji wa ndege anayeruka angani (ambaye hafugwi), uuzaji wa maziwa ambayo hayajakamuliwa na uuzaji wa manyoya ya mnyama yangali mwilini mwake ni uuzaji haramu. Ni wazi kuwa mauzo yote haya yameharamishwa kwa sababu bidhaa hizo hazina uhakika wa kuzipata. Ili pawe na haki kati ya muuzaji na mnunuzi bidhaa hizo hazina budi kupatikana kwanza mkononi ndio ziuzwe.



(viii)Uuzaji wa damu na uuzaji wa uhuru wa mtu (utumwa) uuzaji wa nywele na maziwa ya binaadamu ni biashara haramu. Vitu vyote hivi si haki ya mwanaadamu na havipatikani kutokana na jasho lake. Hivyo hana haki ya kuviuza na wala hana hata uwezo wa kukadiria thamani yake halisi. Kama hatuwezi kukadiria thamani ya mvuto mmoja wa hewa au thamani ya tone moja la maji, tunaweza kukadiria thamani ya damu, achilia mbali thamani ya maisha yetu?


(ix)Mauzo ya mbwa, nguruwe, pombe, damu na mzoga ni biashara haramu. Pia ni haramu kuuza picha na sanamu kama tunavyofahamishwa katika Hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah ameharamisha kipato kilichotokana na kuuza damu, mbwa, na kipato cha Malaya. Na amelaani mwenye kupokea na mwenye kutoa riba, na mwenye kuchora mwili kwa chale na mwenye kuchorwa mwili kwa chale na mchoraji wa picha (za wanyama) na watu. (Bukhari).
Jabir ameeleza kuw a amemsikia Mtume w a Allah akisema katika mwaka wa ushindi (wa kuiteka Makka) wakati alipokuwa Makka.Hakika Allah na Mtume wake wameharamisha mauzo ya pombe; mizoga, nguruwe na masanamu. (Bukhari na Muslim).



(x)Ulanguzi (Kuhodhi bidhaa)
Hili ni neno pana linalotumiwa kwa maana mbali mbali; lakini katika kipengele hiki tutalitumia neno hili kuwakilisha kitendo cha kuteka nyara bidhaa muhimu sokoni kwa kuinunua kwa wingi labda kwa bei ya juu kidogo kwa madhumuni ya kuilundika (kuihodhi) na kuifanya iwe adimu ili hapo baadaye itakapokosekana sokoni iuzwe kwa bei ya juu sana na kutoa faida kubwa sana.



Biashara ya namna hii ni biashara haram kama tunavyofahamishwa katika Hadithi kadhaa zifuatazo:
Umar amesimulia kutoka kwa Mtume wa Allah aliyesema: “Mwenye kuleta nafaka (mjini) anazidishiwa rizki na mkusanyaji na mfichaji wa bidhaa hizo amelaaniwa.” (Ibn Majah, Dirimi).


Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Anayelundika na kuzuia bidhaa za chakula kwa siku 4 kwa nia ya kupata bei kubwa zaidi, anajitenga na Allah na Allah anajitenga naye.” (Razin).



Hadithi zote hizi zimedhihirisha ubaya wa kuzuia bidhaa, hasa bidhaa muhimu kama vile chakula, na kuzifanya ziwe adimu ili kuuza kwa bei kubwa itakayotoa faida kubwa sana. Biashara ya namna hii ni biahara haramu na laana ya Allah iko juu ya walanguzi hawa:



Mu ’az amesimulia: Nimemsikia Mtume wa Allah akisema: “Mbaya ni yule anayelundika bidhaa na kuifanya iwe adimu. Kama Allah akifanya bidhaa kuwa rahisi, yeye anachukia na kama Allah akifanya kuwa ghali, anafurahi. (Razin, Baihaqi).



Hadithi hii inatueleza sura hasa ya mlanguzi. Ama mtu kuweka bidhaa alizozilima na alizotengeneza mwenyewe au kuuza bidhaa alizozinunua kutoka masafa ya mbali si haramu. Lililoharamishwa ni kule kununua bidhaa katika soko la kawaida na kuzificha ili baadaye aziuze kwa bei kubwa baada ya bidhaa hiyo kuwa adimu katika soko.
Pamoja na Uislamu kulaani ulanguzi, hauruhusu kumkangandamiza mfanyabiashara kwa kumuwekea bei ya bidhaa yake. Bei inatakiwa ijiweke yenyewe kulingana na hali halisi ya soko. Bidhaa zikiwa nyingi bei itakuwa chini na bidhaa zikiwa chache itakuwa juu. Tunajifunza kutokana na Hadithi ifuatayo:



Anas amesimulia kuwa wakati mmoja katika wakati wa Mtume wa Allah bei ya vitu ilikuwa ghali. Wakamuomba Mtume: Ewe Mtume wa Allah panga bei kwa nafuu yetu. Mtume wa Allah akajibu: Hakika Allah ndiye anayemiliki bidhaa, anapunguza, anatoa kwa wingi, anatoa rizki, na ananipendelea sana nikutane na Bwana wangu katika hali ambayo hapana yeyote kati yenu atakayenifanya niwe na dhima juu ya damu (iliyomwagika kwa sababu yangu) au mali (aliyopunjwa kwa sababu yangu)! (Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah).



Uislamu kama usivyoruhusu kukandamizwa na kudhulumiwa mnunuzi ndivyo hivyo hivyo usivyoruhusu kukandamizwa kwa mchuuzi au muuzaji. Mtume (s.a.w) akiwa kiongozi mkuu wa serikali ya Kiislamu, hakuthubutu kutumia madaraka hayo kuingilia haki za wafanyabiashara walizopewa na Allah (s.w). Jibu lake kwa namna nyingine lilikuwa “anayepanga bei ni Allah (s.w).



Kutokana na Hadithi hii hapana yeyote aliyojitokeza mwenye haki ya kukaa chini na kumpangia mfanyabiashara bei iliyo kinyume na ile iliyojitokeza yenyewe sokoni. Kinachotakiwa kifanywe na nguvu za dola ni kutokomeza njama zote za ulanguzi na vikwazo vyote vya uchumi. Kisha kuwaacha huru wafanyabiashara wauze bidhaa zao kwa bei halisi inayokubaliwa katika soko huru.



(xi) Kupunguza kipimo cha ujazo au kilo kwa kuharibu mizani au kugonga vipimo vya ujazo ni haramu. Allah (sw) anasema :


Maangamizo yatawathubutikia wapunjao (wenzao). Ambao wanapojipimia kwa watu hupokea (kipimo) kamili, lakini wanapowapimia kwa (kipimo cha) vibaba au mizani (au vinginevyo), wao hupunguza. (83:1-3) Na timizeni kipimo mpimapo; na pimeni kwa m izani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu na bora mwishoni (kwake). (1 7:3 5).



(xii) Kuficha ila (dosari) ya bidhaa inayouzwa ni haramu. Katika Hadithi iliyosimuliwa na Bukhari, Baihaq na Al-Hakim, Mtume (s.a.w) amesema: Muuzaji na mnunuzi kila mmoja lazima atimize makubaliano. Na muuzaji akitoa habari zote juu ya bidhaa anayoiuza pamoja na mfano, kama unauza maharage makavu mwambie mnunuzi mathalan, uzuri wa maharage haya ni kuwa hayajatoboka lakini yana ila moja ya kuchelewa sana kuiva. Mwache mnunuzi apime hiari ya kununua au kuwacha.



Kutokana na maelezo yote haya; juu ya vipengele mbali mbali vilivyo haramishwa katika biashara, tunaona kuwa biashara japo ni kazi halali yenye hadhi kubwa mbele ya Allah, haitamnufaisha mwanaadamu iwapo mipaka ya Al-lah (s.w) haitachungwa wakati wa kufanya shughuli hiyo.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1113


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kupanga uzazi na uzazi wa mpango katika uislamu
Soma Zaidi...

Swala ya jamaa.
Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa. Soma Zaidi...

Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu
Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake. Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi.
Njia hizi ni haramu katika kukuza uchumi wako. Soma Zaidi...

Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke katika jamii
Unadhani mwanamke kupewa mahari kitendo hiki kinaweza kushusha hadhi yake? Soma Zaidi...

Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...

Je manii ni twahara au najisi?
Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis Soma Zaidi...

Kwanini wengi wanaoswali hawafikii lengo la swala zao
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nafasi ya serikali katika ugawaji
Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi. Soma Zaidi...

Fadhila za kufunga mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Haki za nafsi
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...