haki na wajibu kwa wakubwa
Wajibu wa Wakubwa kwa wadogo na wa Wadogo kwa Wakubwa
Katika utamaduni wa Kiislamu wakubwa kwa umri au kwa Maarifa au kwa mamlaka ya (uongozi), wanawajibika kuwahurumia, kuwapenda, kuwaongoza, kuwaelekeza, kuwashauri na kuwaasa wadogo zao kiumri au kimaarifa au mamlaka. Wakubwa wanawajibika kuwamrisha wadogo zao kufanya mema na wanawajibika kukataza maovu wenyewe wakiwa ni viigizo nyema. Kwa kutumia uzoefu wao wanawajibika kuwaelekeza na kuwaongoza katika njia iliyonyooka, wale walio chini yao kiumri na kimamlaka.
Kwa upande mwingine, wadogo kiumri au kimamlaka wanawajibika kuwatii na kuwaheshimu wale walio juu yao kama tunavyoamrishwa:
"Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu, walio miongoni mwenu.Na kama mkikhitilafiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamwamini Mwenyezi na siku ya Mwisho. Hiyo ndiyo kheri nayo ma matokeo bora kabisa." (4:59).
Kutokana na aya hii tunawajibika kuwatii wakubwa zetu na wale wenye mamlaka juu yetu, baada ya kumtii Allah (s.w) na Mtume (s.a.w).
Lakini hatuwajibiki kuwatii wakubwa zetu na wenye mamlaka juu yetu kinyume na kumtii Allah (s.w) na Mtume (s.a.w).. Wale wenye mamlaka juu yetu wakituamrisha kumuasi Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w), tuwakatalie kwa heshima huku tukiwarejesha kwa mafundisho ya Qur-an na sunnah kuwa: "Hapana utii kwa kiumbe katika kumuasi Muumba."
Msisitizo wa kuwatii na kuwaheshimu wakubwa zetu kiumri na kimamlaka pia tunaupata katika Hadith zifuatazo:
Ibn Abbas (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Si katika sisi (si muumini) yule asiyewahurumia wadogo zetu na kuwaheshimu wakubwa zetu wala haamrishi mema na kukataza mabaya ". (Tirmidh)
Anas (r.a) anaeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Kama kijana atamuheshimu mtu mzima kutokana na umri wake, naye Allah atajaalia mtu atakayemheshimu katika uzee wake." (Tirmidh)
Pamoja na msisitizo wa kuwaheshimu wakubwa zetu, hatunabudi kuzingatia mipaka ya Uislamu katika kufanya hivyo. Wakati mwingine kuwaheshimu na kuwatii wakubwa kupita kiasi, hutupelekea kwenye shirk. Kwa kuchelea hili, Mtume (s.a.w) aliwakataza Waislamu kumsifu kupita kiasi kama wakristo walivyofanya kwa mwana wa Maryamu (Issa (a.s) na kumfanya mwana wa Mungu. Hivyo Mtume (s.a.w) ametuelekeza tumsifu kwa kumwita "Mja na Mtume wa Allah".
Pia kwa kuchelea shirk, Mtume (s.a.w) aliwakataza Waislamu wasimsimamie wakati akiingia kwenye mkutano au akipita njiani kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
Anas (r.a) ameeleza: "Hapana mtu tuliyempenda kuliko Mtume wa Allah.Hatukuwa tunamsimamia kwa sababu alikuwa hapendi kusimamiwa." (Tirmidh)
Muawiyah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yeyote yule anayependa watu wamuheshimu kwa kumsimamia, atarajie kuwa mkazi wa motoni." (Tirmidh, Abu Daud)
Tunajifunza kutokana na Hadithi hizi kuwa "heshima" isipelekee kuwafanya wengine kuwa wanyonge na dhalili na wengine kuwa watukufu na bora. Tunapo heshimu au kuheshimiwa, hatunabudi kuiweka mbele yetu aya ifuatayo:
Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja; Adamu) na (yule yule) mwanamke (mmoja; Hawa). Na tumekufanyeni matafa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu basi siyo mkejeliane).Hakika ahishimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye habari (za mambo yote). (49:13)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina ๐2 Dua za Mitume na Manabii ๐3 ai web app ๐4 web hosting ๐5 kitabu cha Simulizi ๐6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Jinsi ya kutekeleza funga za sunnah
Hapa utajifunza muda wa kutia jia katika funga za sunnah. Pia utajifunza kuhusu uhuru ulio nao
Soma Zaidi...Tarstibu za kulipa swaumu ya Ramadhani
Hapa utajifunza namna ambayo utatakiwa kulipa funga ya Ramadhani kwa siku ambazo hukufunga
Soma Zaidi...Funga za Sunnah na umuhimu wake
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Taratibu za mirathi katika zama za ujahilia
Kabla ya kuhubiriwa uislamu watu wa Maka walikuwa na tarayibu zenye dhuluma ndani yake katika ugawaji wa mirathi.
Soma Zaidi...Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada
Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudiย kumfanya Mtume (s.
Soma Zaidi...