Umuhimu wa ndoa na kuoa ama kuolwa katika jamii

Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki.

Umuhimu wa ndoa na kuoa ama kuolwa katika jamii

Kuhifadhi jamii na Zinaa



Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki. Wanyama pia wameumbwa na matamanio haya lakini yanatofautiana sana na yale yaliyopandikizwa kwa mwanaadamu. Matamanio ya jimai kwa wanyama yanakuja juu wakati maalum, wakati ule tu wanapokuwa tayari kupandikiza mbegu ya uzazi. Matamanio ya jimai kwa wanaadamu wa kawaida yako pale siku zote, mradi tu vipatikane vishawishi.



Kwa hali hii, endapo mwanaadamu ataachiwa huru atosheleze matamanio yake ya jimai apendavyo pasina kuwekewa mipaka, kwa vyovyote patatokea madhara makubwa kwake binafsi na kwa jamii nzima. Hivyo, Mwenyezi Mungu (s.w) aliyemuumba mwanaadamu kwa lengo maalum na anayelifahamu vyema umbile Ia mwanaadamu na matashi yake kuliko yoyote yule, amemuwekea utaratibu madhubuti wa kukidhi haja zake za kimaumbile pasina kuleta kero kwa yeyote katika jamii.



Mwenyezi Mungu (s.w) ameharamisha jimai nje ya ndoa ili kuikinga jamii na madhara makubwa ya zinaa ambayo huidunisha na kuivuruga kiasi kikubwa. Mwenyezi Mungu (s.w) amehalalisha ndoa na kuitilia mkazo kwa wale wenye uwezo kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:

Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) mighairi ya hawa. Muwatafute kwa mali zenu, kwa kuwaoa bila ya kufanya zinaa (4:24).


Na (mmehalalishiwa kuwaoa) wanawake wema wa Kiislamu na wanawake wema kailka wale waliopewa kitabu kabla yenu. (Ni halali kuwaoa) mtakapowapa mahari yao mkafanya nao ndoa bila ya kufanya uzinzi wala kuwaweka vimada (5:5)



Aya hizi zinatubainishia kuwa ndoa ni ngao ya kujikinga na kitendo kichafu cha zinaa. Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza ndoa kwa lengo hili hili Ia kujikinga na zinaa kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



Abdullah bin Mas 'ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: "Enyi kongamano ?a vj/ana! Na aoe yule aliye na uwezo miongoni mwenu, hakika kuoa kunainamisha macho na asiyeweza kuoa na afunge; hakika funga hukata matamanio" (Bukhari na Muslim).



Pia Mtume (s.a.w) amesema: Mmoja wenu atakapomuona mwanamke kisha akamtamani, hana budi kumuendea mkewe kwani ana idle idle alicho nacho huyo mwanamke aliyemtamani. (At-Tirmidh).



Hadithi hizi zimesisitiza ndoa na kuonesha umuhimu wake katika kuikinga jamii na zinaa. Uislamu kwa kusisitiza ndoa, umefunga njia zote zitakazo wapelekea wanaume na wanawake kutosheleza matamanio ya jimai nje ya ndoa. Uislamu umekataza uzinifu wa kila ama na umesisitiza ndoa iii kuwawezesha wanaume na wanawake baleghe, kukidhi matashi ya kimaumbile na wakati huo huo wawe na upendo na ushirikiano wa kudumu iii waweze kuwalea watoto watakapopatikana.



Kuendeleza Kizazi cha Mwanaadamu kwa Utaratibu mzuri



Lengo Ia ndoa haliishii kwenye kufurahia jimai tu bali kitendo hicho kinakusudiwa kiwe ndio sababu ya kupatikana watoto watakao endeleza kizazi cha mwanaadamu. Lengo hili Ia ndoa Iinabainishwa wazi katika aya ifuatayo:


(Yeye ndiye) Muumba wa mbingu na ardhi. Amekuumbieni wake (zenu) katika jinsi yenu; na wanyama nao (A kawaumbi a) wake (zao katika jinsi moja na wao);


anakuzidisheni kwa namna hii (ya kuchanganyika dume na jike). Hakuna chochote mfano wake; naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona. (42:11).
Katika aya hii tunafahamishwa kuwa Mwenyezi Mungu (s.w) amewaumba wanaadamu na wanyama katika dume na jike iii papatikane kizazi. Katika aya ifuatayo pia lengo hili Iinabainishwa:


Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka kwa wawili hao. (4:1). Wanaadamu wamewekewa utaratibu wa ndoa iii wasije wakazaana kiholela bila ya kuchukua jukumu Ia malezi.



Kujenga Mapenzi, Huruma na Ushirikiano katika Familia



Lengo jingine Ia ndoa ni kuleta utulivu wa moyo kati ya mume na mke na kupandikiza mapenzi, huruma na ushirikiano kati yao na kuendeleza maadili hayo kwa watoto wao. Lengo hili Iimebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:


Na katika ishara Zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu iii mpate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika hayo zimo ishara kwa watu wanaofikiri." (30:21)."... Wao ni nguo kwenu na nyinyi ni nguo kwao..." (2:187).


Pamoja na lengo Ia kuzaa watoto, aya hizi zinatupa lengo Ia hali ya juu Ia ndoa ambalo halipatikani kwa wanyama. Lengo Ia jimai kwa wanyama ni kuzaana tu kwa kiasi kwamba, baada tu ya kitendo hicho uhusiano wa dume na jike hukatika. Kwa wanaadamu, mahusiano ya mume na mke hayapaswi kuishia tu kwenye jimai bali yanatarajiwa yalete utulivu wa nyoyo na fikra kwa wawili hao na kuwa chimbuko Ia mapenzi, huruma na ushirikiano kati yao. Mume na mke waliofungamana katika misingi ya ndoa, wanatarajiwa kushirikiana kwa mapenzi kiasi cha kuchangia furaha zao na huzuni zao. Ushirikiano kati yao uliofungamana na huruma na mapenzi umepandikizwa iii waweze kulea kizazi kipya kwa maadili yanayotakikana iii kujenga jamii ya makhalifa wa Mwenyezi Mungu.



Kukuza Uhusiano na Udugu katika Jamii



Uhusiano na mshikamano wa kidamu wa familia moja hutanuka pale watoto wa familia moja watakapooana na watoto wa familia nyingine. Hivyo, mapenzi, huruma na ushirikiano wa udugu hutanuka kutoka kwenye familia moja, kisha kwenye ukoo, kisha kwenye kabila hadi kufikia taifa na mataifa. Sisi sote tu familia ya Adamu na Hawa, hivyo tunapaswa tupendane, tushirikiane na tuhurumiane kama tunavyokumbushwa katika Qur-an:


Naye Ndiye aliyemuumba mwanaadamu kwa maji kisha akamfanyia nasaba (ya damu) na ujamaa wa ndoa. Na Mola wako ni Mwenye uweza (/uu ya kilajambo). (25:54)


Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kutokana na mwanamume (Adam) na mwanamke (Hawwa) na tumekufanyeni matafa na makabila (mbali mbali) iii mjuane... (49:13)


Aya hizi zinatudhihirishia wazi kuwa mahusiano ya ndoa kati ya mume na mke ndio msingi wa jamii ya mwanaadamu. Wanaadamu wangalijenga familia zao kwa kufuata utaratibu aliouweka Mwenyezi Mungu (s.w) ulimwengu huu ungalikuwa ni uwanja wa furaha na amani kwani watu wangalihurumiana na kushirikiana kwa mapenzi. Endapo wanaume na wanawake katika jamii hawatoishi maisha ya ndoa na kuamua kutosheleza matashi ya jimai nje ya ndoa, itakuwa ndio chanzo cha vurugu na kuparaganyika kwa jamii. Inatosha kusema kuwa miongoni mwa vurugu na mparaganyiko wa jamii hivi leo inatokana na uzinzi na kubeza maisha ya ndoa.



Kukilea Kizazi katika Maadili



Upendo kwa watoto hauishii tu kwenye kuwapa watoto chakula bali ni lazima uambatane na malezi yao yote. Malezi ya watoto ni pamoja na kuwaelimisha katika nyanja mbali mbali zinazohusu maisha yao, kuwafunza tabia njema na utaratibu wa maisha anaouridhia Mwenyezi Mungu (s.w). Malezi ya watoto katika familia ni kazi tosha na ya kudumu na mama anatakiwa awe nyumbani kwa kazi hii. Hakuna mtu au taasisi yoyote inayoweza kuifanya kazi hii vizuri badala ya familia. Watoto waliokosa malezi ya kifamilia hata kama watapelekwa kwenye shule za malezi hawawezi kuwa sawa kitabia - upendo, huruma na mwenendo mwema na wale waliopata malezi ya familia.



Kumuendeleza Mwanaadamu Kiuchumi



Ndoa ni changamoto kwa waangalizi wa familia, hasa baba. Katika kuilea familia wazazi huwa macho sana katika kutekeleza majukumu yao ili kukidhi mahitaji muhimu ya familia. Mahitaji muhimu ya familia ni pamoja na chakula, mavazi, makazi na gharama za kuwaelimisha watoto. Baba ambaye ndiye mkuu wa familia hulazimika kufanya kazi kwa juhudi kubwa na Maarifa. Pia wazazi, kwa kuzingatia jukumu Ia malezi linalo wakabili, huwa macho katika kutumia kile walicho kichuma kwa kuhakikisha kuwa wanatumia mali yao katika mambo ya lazima kwa familia. Ni kwa msingi huu Mwenyezi Mungu (s.w) anatufahamisha katika Qur-an kuwa watoto hawaleti ufakiri kwani kila mtoto amepangiwa riziki yake ambayo hupitia mikononi mwa wazazi kwa njia ya uchumi. Tunajifunza hili katika aya ifuat




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 205

Post zifazofanana:-

Namna ya kuhiji, hatua kwa hatua
Soma Zaidi...

Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo
Kuamini Mwenyezi Mungu sio suala la Kibubusa au Kufuata Mkumbo. Soma Zaidi...

Rangi za majimaji yanayotoka kwenye uke na maana yake kiafya
Je unajuwa kuwa majimaji yanayotoka ukeni yanatueleza mengi kuhusu afya yako, rangi za majimaji ya ukeni na damu ya hedhi Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

Haki ya kumiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA, HABARI NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

ALIF LELA U LELA KITABU CHA PILI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KITABU CHA PILI HADITHI ZA ALIF LELA U LELA UFUPISHO WA ALIF LELA U LELA KITABU CHA KWANZA. Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA KWIKWI
Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo. Soma Zaidi...

FYA YA UZAZI, ULEZI, BABA, MAMA NA MTOTO PAMOJA NA MAHUSIANO
Soma Zaidi...

Maana na taratibu za kiuchumi katika uislamu
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 08
20. Soma Zaidi...

UGONJWA WA MALARIA NA TAKWIMU ZA ATHARI YAKE KIDUNIA
Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles. Soma Zaidi...