picha

Ni nini maana ya ndoa?

Ni nini maana ya ndoa?

Maana ya Ndoa



Ndoa, kwa ujumla, ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii. Kwa mfano, hapa Tanzania mume na mke watatambulika kuwa wameoana kisheria, pale watakapokuwa wamefunga mkataba wa kuishi pamoja mbele ya Mkuu wa wilaya au mbele ya walii na mashahidi wawili (ndoa ya kiislamu)au mbele ya Padri (Kanisani).



Ndoa ya Kiislamu ni mkataba wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa kuzingatia masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislamu. Ndoa yoyote iliyofungwa kinyume na masharti na taratibu za Kiislamu, haikubaliki kwa Waislamu.



Umuhimu wa Ndoa kwa Mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:



Katika Hadithi iliyopokelewa na Imamu Bukhari Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwa ndoa ni katika sunnah yake na akaongeza kusema: "Yeyote anayekataa sunna yangu sipamoja nami ".



Anas (r.a) amesema kuwa Mtume wa Allah amesema, 'Mtu anapooa huwa amekamilisha nusu ya dini, kisha amche Allah ili akamilishe nusu iliyobakia." (Bukhari).



Ndoa inasisitizwa kutokana na umuhimu wake katika kuijenga na kuiendeleza jamii kwa:
(i)Kuihifadhi jamii na zinaa.
(ii)Kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri.
(iii)Kujenga mapenzi na huruma katika familia.
(iv)Kukuza uhusiano na Udugu katika jamii.
(v)Kukilea kizazi katika maadili mema.
(vi)Kuwafanya watu wawajibike ipasavyo.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 4842

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Kiwango cha mahari katika uislamu

Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari?

Soma Zaidi...
swala za tahiyatu al masjid, qabliya na baadiya

Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid.

Soma Zaidi...
NAFASI YA SUNNAH KATIKA UISLAMU

Nafasi ya Sunnah katika UislamuMtume Muhammad (s.

Soma Zaidi...
Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?

Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?

Soma Zaidi...