image

Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana

Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana

Umaharimu



Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana kutokana na ukaribu wa nasaba kama ilivyobainishwa katika Qur-an na Sunnah. Wanaume wa Kiislamu wameharamishiwa kuwaoa wanawake wanaobainishwa katika aya zifuatazo:


Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu; isipokuwa yale yaliyokwishapita. Bila shaka jambo hili ni uovu na chukizo na ni njia mbaya (kabisa). Mmeharamishiwa (kuoa) mama zenu, watoto wenu, dada zenu, shangazi zenu, ndugu za mama zenu, watoto wa ndugu zenu, watoto wa dada zenu, na mama zenu waliowanyonyesheni, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, walio zaliwa na wake zenu mliowaingilia. Lakini kama nyinyi hamjawaingilia basi si vibaya kwenu (kuwaoa). Na mmeharamishiwa wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na (mmeharamishiwa) kuwaoa madada wawili wakati mmoja, isipokuwa yale yaliyokwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kurehemu na Mwenye kusamehe. (4:22-23)


"Na pia mmeharamishiwa wanawake wenye (waume zao) isipokuwa wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume. Ndiyo Sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalalishiwa (kuoa wanawake) minghairiya hawa..." (4:-24)



Aya hizi zinabainisha wanawake walioharamishwa kuwaoa kuwa ni hawa wafuatao:
1.Mwanamke aliyepata kuolewa na baba yako, (babu yako, baba wa baba yako - wa kuumeni na kikeni).
2.Mama aliyekuzaa (babu aliyezaa waliokuzaa, mama wa bibi aliyezaa aliokuzaa...).
3.Binti yako uliyemzaa (au binti aliyezaliwa na uliyemzaa...). Pia binti wa kunyonya na mwanao (na kikazi chake...).
4.Dada yako khalisa au wa kwa baba au wa kwa mama.
5.Shangazi yako- dada wa baba yako,(na dada wa babu yako...).
6.Mama mdogo; ndugu wa mama yako (au ndugu wa bibi yako...).
7.Binti wa ndugu yako mwanamume, khalisa au wa kwa baba au kwa mama (na kila aliyezaliwa naye).
8.Binti wa dada yako khalisa au wa kwa baba au kwa mama
9.Mama wa kukunyonyesha (na mama zake wa kumzaa au wa kumnyonyesha).
1O.Dada yako wa kunyonya naye (aliyenyonyeshwa na aliyekunyonyesha).
11 .Mama yake mkeo wa kumzaa au wa kumnyonyesha (na bibi yake pia wa kumzaa mama yake au wa kumnyonyesha Ama ndugu yake mama yake mkeo yaani mama mdogo wake au shangazi yake wa kuzaliwa au kunyonya; unaweza kumuoa akifa mkeo au utakapomuacha na eda ikaisha.
12.Binti wa mkeo uliyemuingilia (na mjukuu wake...).
13.Mke aliyeolewa na mwanao wa kumzaa au wa kunyonyeshwa na mkeo (na kizazi chake); si mke wa mtoto wa kupanga au mtoto wa kulea.
14.Mtu na ndugu yake pamoja (au) mtu na shangazi yake au mtu na mama yake mdogo pamoja. Akifa mke au ukimuacha na eda ikaisha unaweza kumuoa dada yake, au shangazi yake, au mama yake mdogo.
15.Mke wa mtu, bado mwenyewe hajafa wala hajamuacha ni Haram kumuoa. Wanawake hao wameharamishwa kuolewa na wanaume wanaofanana na hawa kwa upande wa kiumeni.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 444


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-