Hoja za kudhibiti uzazi hivi leoTumekwishaona kihistoria mambo yaliyopelekea kuibuka kwa kampeni hii. Lakini hoja kubwa inayofanya kampeni hii iendeshwe kote duniani hivi leo ni ya uwiano kati ya idadi ya watu na maendeleo ya kiuchumi. Na ni kwa sababu hiyo ndiyo maana serikali nyingi hivi sasa zimeamua kuipigia zumari kampeni hii. Hoja yenyewe siyo ngumu kuielewa:


Watu kuongezeka kwa kasi zaidi kuliko ongezeko Ia pato Ia nchi kiuchumi. Matokeo yake ni kuwa taifa litashindwa kutoa huduma kuinua hali za wananchi. Hoja hii ni dhaifu sana. Lakini kabla hatujaonesha udhaifu wake tungependa kwanza kuielezea kwa ufasaha zaidi. Na tutanukuu hoja zilizotolewa na mtetezi mashuhuri sana wa udhibiti wa uzazi (birth control) Bwana Leanard Barnes.Bwana Barnes katika kitabu chake (African Renaissance - sura ya 7) anatoa hoja ya kwanza kuwa nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania zina kundi kubwa Ia watu ambao hawana Elimu wala mafundisho yoyote. Kundi ambalo halina manufaa yoyote kiuzalishaji mali na kwa hakika ni mzigo kwa taifa. Anasema kundi hili Ia watu kwa hakika halipaswi kuwepo. Kwa kufuata msingi wa aliyefika mwanzo, ahudumiwe kwanza, watu hawa wana haki ya kuitaka jamii iwape kipaumbele kabla ya kuwafikiria wale ambao hawajazaliwa.Hoja ya pili ni kuwa kilicho muhimu kwa taifa, kama ilivyo katika kiwanda, siyo uwingi bali ubora wa watu. Kwa sababu hiyo ndiyo maana viwanda siku zote huweka ukomo katika idadi ya wafanyakazi wake kulingana na mahitaji ya kudumisha ufanisi wa kazi. Kama ambavyo hayo ni muhimu katika mpango wa kiwanda kimoja kimoja hayo ni muhimu pia kwa taifa kwa ujumla.Katika kuisisitiza hoja hii Bwana Barnes anasema kama ambavyo serikali zote zimeweka idara za uhamiaji ili kudhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini, serikali za Kiafrika zimekawia mno kuzindukana kuwa ipo haja pia ya kudhibiti wageni wanaoingia nchini kwa njia ya kuzaana. Anasema: "Iwepo sheria ya uhamiaji wa mimba za binaadamu". Leanard Banees anaendelea kwa kusema:"Katika bara Ia Afrika mmomonyoko wa udongo unaosababishwa na mbinu duni za ukulima unaoana na mmomonyoko wa watu unaosabaishwa na mbinu duni za kuzaana. Ongezeko Ia watoto ni kubwa mno kiasi ambacho makazi, afya, shule na ajira haviwezi kudhibiti mtiririko wake, watu hao wanahitaji kuhifadhiwa kwa kuchukua hatua kama zile zinazochukuliwa katika kuhifadhi ardhi."Akitoa mfano wa nchi ya Tanzania, bwana Barnes anasema baada ya kila miezi 18 idadi ya watoto wanaozaliwa huwa sawa na idadi ya watu wanaofanya kazi za ajira. Na kama uwiano uliopo sasa kati ya wafanyakazi na wakulima hautabadilika, basi watoto wapatao 10,000 kwa mwaka watazaliwa katika nyumba za watu wa mijini na watoto 190,000 watazaliwa vijijini.Kwa kutumia takwimu zilizotolewa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano, Bwana Barnes anasema, "watoto 66,000 (karibu theluthi moja ya watoto wote waliozaliwa) watakufa kabla yakufikia umri wa kuweza kulipa gharama ya malezi yao. Na wale wanaonusurika huishi katika tishio Ia maradhi na utapia mlo".Hoja ya tatu ya Bwana Barnes imejengwa juu ya habi hiyo duni inayowakabibi watoto wa Kitanzania na wengine Afrika. Anasema nchi za Kiafrika zibipopigania uhuru zibifanya hivyo ibi kujenga utu wa kurejesha heshima yao na kujibetea maendebeo ya baadaye. Kizazi hicho kitajihisi vipi juu ya utu na heshima yao kitakapogundua kuwa thebuthi moja miongoni mwao wanatakiwa wafe kabba ya kufikia babeghe? Watahisi vipi juu ya uhuru wa kujibetea maendebeo yao ya baadaye iwapo nusu yao hawawezi hata kupata Ebimu ya msingi katika shube duni? (bkumbukwe kuwa, Bwana Barnes abiandika kitabu chake 1969). Kutokana na hayo Bwana Barnes anaubiza:Je, hatutakuwa tunawahurumia na kuwafanyia hisani ya kwebi watoto hao iwapo tutawaomba waakhirishe kuja kwao duniani kwa muda, wakati kizazi cha sasa kikijitahidi kuondosha umasikini, maradhi na kujenga mfumo wa Ebimu ambao angabau ni wa afadhabi?Kwa muhtasari hoja ya tatu ya Barnes ni kuwa ni kitendo cha ukatili kuwaleta watoto duniani halafu kuwatesa kwa njaa na maradhi. Si bora kuwazuia wasije? Bwana Barnes anasema kikwazo kikubwa kabisa cha maendebeo ya Afrika ni uongezekaji kihobeba na idadi ya watu. Hata kama matatizo yote mengine yatatatubiwa, bakini maadamu tatizo Ia uongezekaji wa watu habijapatiwa ufumbuzi, basi hakutakuwa na maendebeo Afrika. Bwana Barnes anawabaumu sana wale wataalamu wa uchumi wanaosema kuwa ongezeko Ia watu katika Afrika kwa asilimia 3 kwa mwaka si tatizo maadamu ongezeko Ia uchumi litakuwa asilimia 5 kwa mwaka. Watu kama hao anasema wanapotosha hakika ya mambo


yalivyo.Watu watakaoisaidia sana Afrika ni wale ambao watatambua umuhimu wa suala Ia idadi ya watu katika masuala yote ya maendeleo ya jamii na hasa kasi na namna ambayo kizazi kimoja huchukua nafasi ya kizazi kingine. Watu wanaojua umuhimu wa ubora na sio uwingi wa watu.
Sera kama hiyo Bwana Barnes anasema itawawezesha wapangaji wa mipango 'kuanza kwa kujiuliza kazi zipi ambazo jamii inataka zifanyike, na halafu izalishe na kuwafundisha watu wa kufanya kazi hizo.Bwana Barnes anamalizia kwa kusema kuwa ukatili wanaofanyiwa watoto wachanga ni matokeo ya huruma. Ni matokeo ya maendeleo ya sayansi ya tiba. Sayansi ya tiba (medical science) kwa kung'ang'ania kuokoa maisha ya watu bila kujali ubora wa maisha wanayoishi ndio imeleta matunda haya machungu. Na kwa hiyo sayansi ya tiba ifikiriwe kuleta ufumbuzi wa ongezeko Ia watu.Maandishi haya ya Bwana Leanard Barnes yanawakilisha hoja za wale wanaoiunga mkono kampeni hii ya kudhibiti ongezeko Ia watu. Sasa hebu tuangalie udhaifu wa hoja hizi.