Je na wewe i katika wale ambaowanahitaji kujuwa kuhusu Vitamini A, kazi zake na vyakula vya vitamini A. post hii inakwenda kukujuza zaidi pamoja na historia ya vitamini A.
Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene. Vitamini A ni moja kati ya vitamini vingi. Vitamini vingine ni viamini b, C, D, E, K. unaweza kupata vitamini A sana kwenye mboga za majani za kijani, maini, mayai, maziwa, karoti na spinach. Katika makala hii tutakwenda kuona mengi kuhusu vitamini A, kazi zake, vyakula vya vitamini A pamoja na athari za upungufu wake mwilini:
Yaliyomo:
1.Maana ya vitamini A
2.Kazi za vitamini A
3.Vyakula vya vitamini A
4.Upungufu wa vitamini A
5.Athari za kuzidi kwa vitamini A
Maana ya vitamini A
Vitamini ni aina ya fat soluble vitamini ambayo ni kampaind ogania (organic compound) inayopatikana katika makundi kama retinol, retinal, retinoic acid na provitamin ambazo ni beta-carotene. Vitamini A ni muhimu katika ukuaji, uboreshwaji wa mfumo wa kinga na kuboresha afya ya macho.
Ugunduzi wa vitamini A umeanza toka miaya ya 1816 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Francois Magendie alipokuwa akimfanyia uchunguzi mbwa mgonjwa. Baada ya hapo tafiti mbalimbali zikafata mwaka 1912, 1913, 1918, 1920 na 1939 na 1947. vitamini A vimepewa jina hili katika tafiti za mwaka 1920.
Kazi za vitamini A
1.Husaidia katika afya ya macho yaani kuona
2.Husaidia katika ukuaji
3.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
4.Husaiia katika ukuaji wa mimba na mtoto aliye tumboni
5.Husaidia katika afya ya mifupa
6.Husaidia katika afya ya ngozi
7.Husaidia katika afya ya meno
8.Husaidia katika utengenezwaji wa uteute mwilini.
Vyakula vya vitamini A
1.Maini
2.Karoti
3.Viazi vitamu
4.Spinachi
5.Maboga
6.Pilipili
7.Maembe
8.Njegere
9.Maziwa
10.Mayai
11.Mboga za majani za rangi ya kijani
Upungufu wa vitamini A
Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini A huathiri watoto wanaokadiriwa kufikia 670,000 waliochini ya umri wa miaka mitano kila mwaka. Pia inakadiriwa kuwa watoto katika ya 250,000 na 500,000 wanakuwa vipofu katika nchi zinazoendelea kila mwaka. Tafiti zinathibitisha kuwa chanzo kikuu cha upofu kwa watoto ni upungufu wa vitamini A.
Athari za vitamini A kupitiliza
Endapo mtu atakuwa na vitamini A vingi ndani ya mwili hata vikapitiliza kiwango ambacho mwili unaweza kudhibiti, athari zifuatazo zinaweza kutokea:-
1.Mkusanyiko wa sumu mwilini
2.Kichefuchefu
3.Kuwshwa
4.Kukosa hamu ya kula
5.Kutapika
6.Kuona maluelue
7.Maumivu ya kichwa
8.Kupotea kwa nywele na misuli
9.Maumivu ya tumbo na uchovu
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kqa mgonjwa aliyeingiliwa na kitu au uchafu kwenye sikio.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi matokeo ya maambukizi kwenye milija na ovari, ni matokeo apatayo mtu mwenye maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina mbalimbali za vidonda kwenye mwili wa binadamu, ni vidonda ambavyo utokea kwenye mwili wa binadamu kwa Aina tofauti.
Soma Zaidi...Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya roghage
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za tumbo,tumbo ni sehemu ya mwili ambayo ushughilika na kutunza chakula,
Soma Zaidi...