Fahamu kuhusu dawa ya Theophylline katika kutibi mfumo wa upumuaji

Post hii inahusu zaidi dawa ya theophylline ni dawa inayofanya kazi kwenye mfumo wa upumuaji.

Fahamu dawa ya Theophylline katika kusaidia kwenye mfumo wa upumuaji 

1. Dawa ya Theophylline ni mojawapo ya dawa ambayo ufanya kazi kwenye mfumo wa upumuaji hasa kwa wagonjwa ambao wanabanwa , kwa hiyo dawa hii usaidia hasa kwa watu wenye asthma, ufanya kazi hiyo kwa kulegeza sehemu za mfumo wa upumuaji na hewaa uweza kupitia kwa urahisi na  mgonjwa uweza kuendelea vizuri na afya njema.

 

2. Dawa hii kwa kawaida huwa kwenye mfumo wa vidonge na nyingine upitia kwenye mishipa ya damu na ikipitia kwenye damu inapaswa kwenda pole kwa mda walau wa dakika ishilini na pia inawezekana kupitia kwenye matako au kwenye paja ila ikitolewa kwa mtindo huo usababisha kuwepo kwa viupele sehemu hizo ndio maana mara nyingi utolewa kama vidonge na kupitia kwenye damu .

 

3. Pia dawa hii kwenye matumizi huwa na maudhi madogo madogo kama vile kutapika na kichefuchefu, kizunguzungu, maumivu makali ya kichwa, mapigo ya moyo kwenda mbio, maumivu kwenye misuli, pia sukari inawezekana kupanda.

 

4. Dawa hii huwa na milligrams kuanzia mia Moja mpaka mia tatu na dozi utolewa kulingana na umri na uzito hii ni dozi ya mfumo wa vidonge. Na pia milligrams huwa tofauti kwa wale wanaotumia dawa kupitia kwenye mishipa ya damu, dozi uanzia milligrams mia mbili hamsini mpaka miatano kwa watu wazima na kwa watoto uanzia mia ishilini na tano mpaka mia mbili hamsini na Tano.

 

5. Kwa hiyo dawa hii inapaswa kutumiwa kulingana na wataalamu wa afya na isitumiwe kiholela au kwa mazoea kwa sababu inawezekana kuwepo kwa matatizo kwa baadhi ya watumiaji.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/23/Friday - 03:09:37 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 690


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-