Navigation Menu



Fahamu aina ya penicillin ambayo ufanya kazi kwa mda mrefu

Post hii inahusu zaidi aina mojawapo ya dawa ya penicillin ambayo ufanya kazi kwa mda mrefu, dawa hii kwa kitaamu huiitwa procaine benzyl penicillin.

Fahamu kuhusu dawa ya procaine benzyl penicillin.

1. Ni aina mojawapo ya dawa ya penicillin ambayo ufanya kazi kwa mda mrefu, kwa sababu yenyewe udili na bakteria ambao ushambulia mwili na kusababisha madhara ya mda mrefu na kwa hiyo ikiingia mwili inawezekana kukaa kwa masaa Ili kuweza kudili na bakteria ambao wameleta madhara ya mda mrefu.

 

2. Kwa kawaida dawa hii utumika kutibu maambukizi mbalimbali ya bakteria ambayo ujitokeza kwenye mwili wa binadamu na pia utumika kwa watu wazima na watoto kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya na pia kwenye kundi hili Kuna dawa nyingine ambayo Kwa kitaamu huiitwa fortified procaine penicillin nayo ufanya kazi kama procaine benzyl penicillin.

 

3. Dawa hii kwa kawaida huwa kwenye mfumo wa unga na huwa kwenye ki chupa Fulani hivi na pia uchanganywa na maji maalumu kwa ajili ya dawa ambayo Kwa kitaamu huiitwa sterile water,na uchanganywa kwa pamoja , yaani dawa na maji na pia utikiswa kumhakikishia kuwa unga umachanganyika kabisa na maji .

 

4. Dose kwa mgonjwa utegemea mtoto na mtu mzima,uzito na umri wa mtu,na pia dawa hii inaweza kutolewa kwa kupigwa sindano kwenye mapaja au Tako, na kwa wakati mwingine uweza kupitia kwenye damu, kwa hiyo mchanganyiko wa kupitia kwenye paja au Tako ni tofauti na ule mchanganyiko wa kupitia kwenye mishipa ya damu.

 

5.  Dawa hii pia utumiwa na watu mbalimbali ila kwa wale wote wenye aleji na dawa ya penicillin hawapaswi kutumia dawa hii, kwa hiyo watatumia dawa nyingine kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya.

 

6. Pia dawa hii Ina maudhi madogo madogo baada ya kuitumia, maudhi yenyewe ni kama maumivu kwenye jointi, unaweza kupata upungufu wa damu ukiitumia kwa mda mrefu, kwa hiyo wenye tatizo la upungufu wa damu wanapaswa kuitumia kwa taahadhari,pia dawa hazipaswi kutumiwa kiholela Bali ni kwa ushauri wa wataalamu wa afya.

 

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 761


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Fahamu kuhusu dawa ya kaoline
Post hii inahusu dawa ya kaoline katika kutibu au kuzuia kuharisha ni dawa ambayo imependekezwa kutumiwa hasa kwa wale walioshindwa kutumia dawa ya loperamide. Soma Zaidi...

Ifahamu dawa ya furosemide.
Post hii inahusu zaidi dawa ya furosemide ni mojawapo ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la diuretics na kwa jina linguine huitwa lasix Soma Zaidi...

Dawa ya Panadol au paracetamol katika kutuliza maumivu
Posti hii inahusu zaidi kazi ya paracetamol katika kutuliza maumivu, ni Aina ya dawa ambayo utumiwa sana katika kutuliza maumivu kwa wagonjwa. Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya kutibu kikohozi inayoitwa expectorant
Post hii inahusu zaidi dawa aina ya expectorant katika matibabu ya kikohozi,ni dawa ambayo usaidia au uzuia kikohozi kuendelea kutokea. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya Nystatin
Post hii inahusu zaidi dawa ya Nystatin ni mojawapo ya dawa ambayo utumika kwenye ngozi. Soma Zaidi...

Miungurumo haiishi tumboni nikishika upande wa kushoto wa tumbo kuna maumivu kwa mbali je mm nitumie dawa gan kuondoa tatizo hilo
Kukawa na gesi tumboni kunaweza kuwa ni dalili ya shida kwenye afya, hasa katika mfumo wa chakula. Hali itakuwa sio nzuri endapo utakosea hamu ya kula na kuhisivkushiba muda wowote. Soma Zaidi...

Fahamu dawa za cyclophosphamide na mustargen.
Post hii inahusu zaidi dawa za cyclophosphamide na mustargen katika kupambana na ugonjwa wa Kansa. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya ALU au kwa lugha nyingine ni dawa ya mseto
Post hii inahusu zaidi dawa ya ALU ila kwa jina jingine huitwa dawa ya mseto,ni aina ya dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria ya kawaida. Soma Zaidi...

Fahamu dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya cardiac glycoside katika matibabu ya magonjwa ya moyo,dawa maalum ambayo imo kwenye kundi hili la cardiac glycoside ni digoxin, ni dawa muhimu ambayo utumika kwenye mfumo wa vidonge mara nyingi. Soma Zaidi...

Fahamu Dawa itwayo Diazepam
Diazepam ni nini? Diazepam ni Dawa ambayo Huathiri kemikali kwenye ubongo ambazo zinaweza kukosa uwiano na kusababisha wasiwasi. Diazepam hutumiwa kutibu matatizo ya wasiwasi, dalili za kuacha pombe, au misuli. Diazepam wakati mwingine hutumiwa pamoja n Soma Zaidi...