SURAT AL-QURAYSH Sura hii ina majina mawili.
SURAT AL-QURAYSH
Sura hii ina majina mawili. Inaitwa Qureish na pia inaitwa Li ii laafi. Ibni Abbas anasimulia ya kuwa ilishuka Makka. Qureish ni jina la kabila lililotoka kwa Nadhir bin Kinana (Razi). Wengine wanasema neno Qureish limetoka katika neno Qarsh ambalo ni jina la samaki mkubwa wa bahari anayekula samaki lakini yeye haliwi. Hivyo kwa ukubwa wa kabila lao na kwa kuheshimiwa na watu wote nao wakaitwa Kureish. Makureish walikuwa watu wa Makka na walinzi wa Kaaba, na kwa sababu ya kuilinda Kaaba waliheshimiwa sana.
Sura hii imeshuka kwa maqurayshi kama alivyosema Mtume (s.a.w) βAllah amewapa neema Maquraysh ambayo hajampa yeyote kabla yao na hatampa yeyote baada yao: Ukhalifa umepewa mtu katika wao, uangalizi wa nyumba tukufu ya Allah umepewa mtu miongoni mwao, kazi ya kuwapa maji mahujaji imepewa mtu katika wao, utume umepewa mtu katika wao, wamepewa ushindi dhidi ya jeshi la tembo, walimuabudu Allah kwa miaka saba ambapo hakuna yeyote aliyekuwa akimuabudu Allah, na sura kwenye quran imeshushwa kwa ajili yao na hakuna yeyote aliyetajwa kwenye surahiyo ila wao (kwa kupewa jina la al-quraysh)
Umeionaje Makala hii.. ?
Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa alam nasharah yaani Surat Ash sharh.
Soma Zaidi...(i)Mtume Muhammad (s.
Soma Zaidi...Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani?
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kanuni za tajwid katika kusoma bismillah au basmalah.
Soma Zaidi...Ikh-fau ni moja ya hukumu za nun sakina na tanwin kwenye hukumu za Quran tajwid
Soma Zaidi...