Historia ya uandishi wa Hadithi, na ni kwa nini wakati wa Mtunme hakukuwa na uandishibmkubwa wa hadithi

Hapa utakwendabkuijuwabhistoria ya uandishi wa hadithi. Pia utaijuwa sababu iliyopelekea uandishi wa hadithi kuwa mdogo .

Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.a.w)
Tofauti na Qur-an, ambayo iliandikwa mara tu baada ya kushushwa chini ya malekezo na usimamizi wa Mtume (s.a.w) mwenyewe, Hadith za Mtume (s.a.w) ambamo ndani yake ndio tunapata sunnah yake, zimeandikwa na watu kulingana na walivyomuona, au walivyomsikia. Historia ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.a.w) katika vitabu vya Hadith , imechukua takriban muda wa karne tatu. Kwa kurahisisha tutaigawa historia ya kuhifadhiwa Hadith katika maandishi katika hatua nne zifuatazo:  - Wakati wa Mtume (s.a.w).
- Wakati wa Maswahaba wa Mtume (s.a.w).
- Wakati wa Tabi'iina.
- Wakati wa Tabii Tabi'iina.

Wakati wa Mtume (s.a.w)
Wakati wa Mtume (s.a.w), hapakuwa na uandishi mkubwa wa Hadith kwa sababu:

Kwanza, Mtume mwenyewe alikuwepo, hivyo kilichokuwa muhimu kwa Masahaba ni kufuata mafundisho ya Mtume(s.a.w) na kuigiza mwenendo wake,kila walipokwama katika utendaji au kila walipotatizwa na tatizo lolote, walimwendea Mtume(s.a.w) na aliwakwamua au kuwatatulia tatizo lolote walilokuwa nalo.

Pili, Masahaba katika kipindi hiki walijishughulisha sana na kuandika, kusoma na kuhifadhi Qur-an moyoni na kuitekeleza katika maisha yao ya kila siku.

Tatu, kwa kuwa mwanzoni Mtume (s.a.w) aliwakataza Masahaba wake kuandika Hadith, walizoea kutoandika Hadith hata wakati waliporuhusiwa kuandika na walipendelea kutoandika kuliko kuandika Hadith.

Nne, katika wakati huu wa Mtume (s.a.w) Masahaba walishughulika sana katika harakati za kuuhami Uislamu ambao ulikuwa umesongwa sana na maadui wake ambao walipania sana kumuua Mtume, Uislamu na Waislamu.

Kutokana na sababu hizi nne na nyinginezo, uandishi wa Hadith haukupewa nafasi nzito katika kipindi hiki cha Mtume (s.a.w). Hivyo, Hadith nyingi zilibakia katika matendo na vifua vya Masahaba. Masahaba waliokuwa karibu sana na Mtume (s.a.w) kwa muda mrefu wa maisha yao, walihifadhi Hadith nyingi zaidi kuliko wale waliokaa mbali na Mtume (s.a.w). 

Miongoni mwa Masahaba waliofahamika kuwa mashuhuri kwa kuhifadhi Hadith nyingi ni Abu Hurairah, bibi Aysha (mkewe Mtume (s.a.w)) 'Abdullah bin 'Umar, 'Abdullah bin 'Abbas, na Abdullah bin 'Amr na Abdallah bin Masu'ud (r.a)


 



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2023/01/27/Friday - 09:24:18 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 519


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Fadhila za kusoma surat al Kahaf siku ya Ijumaa
Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili Soma Zaidi...

Uandishi wa hadithi wakati wa Matabii tabiina (tabiitabiina)
Hii ni historia ya uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina. Yaani wafuasi wa wale wafuasi wa Masahaba Soma Zaidi...

Nini maana ya Quran
Post hii inakwenda kukuambia maana ya Quran Soma Zaidi...

Historia ya uandishi wa Hadithi, na ni kwa nini wakati wa Mtunme hakukuwa na uandishibmkubwa wa hadithi
Hapa utakwendabkuijuwabhistoria ya uandishi wa hadithi. Pia utaijuwa sababu iliyopelekea uandishi wa hadithi kuwa mdogo . Soma Zaidi...

Maana ya sunnah (suna) na maana ya hadithi
Post hii itakufundisha maana ya neno sunnah katika Uislamu. Pia utajifunza maana ya neno hadithi katika uislamu Soma Zaidi...

Nafasi ya Sunnah (suna) katika Uislamu.
Hapa utajifunza nafasi ya kufuata suna katika Uislamu Soma Zaidi...

Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba
Nini kilichangia ongezeko la uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba. Soma Zaidi...