Basi tambua haya;-

81..Kunywa maji mengi hakuna madhara yeyote, ila kutokunywa maji mengi kuna madhara mengi zaidi.

82.Ni rahisi kwa wanawake kupata UTI kulikowanaume. Ni kwa sababu wanawake mirija yao ya haja ndogo ni midogo, halikadhalika sehemu zao za haja ndogo na kubwa zipo karibu hivyo ni rahisi kwa vijidudu vya UTI kuingia njia ya haja ndogo kwa kutokea njia ya haja kubwa.

83..Inashauriwa kiafya kumwaga maji chooni kabla ya kufanya haja yako. Na hii hasa ni kwa wale ambao wanatumia vyoo vya kuchangia au vyoo vya kukaa.

84.supu ya samaki inashauriwa sana na wataalamu wa afya. Bila kusahau mafuta ya samaki ambayo yana uwezo wa kupambana na saratani na kufanya ukuaji wa mtot uwe salama.

85.Hakuan vyakula vilivyohakikiwa na wataalamu wa afya kuwa vinaongeza seli za CD4. Ila unaweza kuongeza uwezo wa mwili wako kupambana na maradhi kwa kula chakula bora na mlo kamili.

86.Juisi ya matunda asili kama karoti husaidia katika kulinda mwili na maradhi. Matunda mengine ni kama mananasi, mapensheni, mapalachichi na miwa.

87.Magonjwa mengi wanayougua leo watu duniani ni kutokana na mifumo mibaya ya vyakuyla.

88.Kama unatumia vidonge vya vitamini si vyema kula maini kwa wingi maana maini yana vitamini vingi hivyo unaweza kupata maradhi yahusuyo na zidi kwa vitamini

89.Ni vyema kula matunda japo mara moja kwa siku na samaki japo mara moja kwa wiki.

90.Inashauriwa kutafuna vizuri chakula kabla ya kukimeza. Na hii ni kusaidia mwili kumeng’enya chakula zaidi.

91.Ukiwa na mafua pendelea kunywa vinywaji vimoto kama chai imoto. Hii husaidia kupunguza athari za w adudu wa mafua kwani hawawezi kuvumilia joto.

92.Ni vyema unapokunywa maji unywe kipole pole.

93.Unapokunywa sumu wahi kunywa majiwa au ukikosa kunywa maji mengi sana. Fanya hivi pia kwa mtu alokunywa sumu au sabuni au kemikali yeyote. Hii ni kama huduma ya kwanza tuu kishwa wahi hospitali

94.Aliyekunywa sumu jitahidi kumtapisha kwa kutia vidole ama kwa namna ingine yeyote. Ila kama sumu ni kemikali zinazochubua wacha kufanya hivyo.

95.Ndani ya tomato kuna aina za carotenoid kama vile: lutein na lycopene. Hizi husaidia katika kuimarisha afya ya macho. Au kupunguza athari zinazotokana na mwanga zisidhuru macho. Tomato ni katika matunda ambayo yauwezo mkubwa wa kulinda mwili dhidi ya maradhi. Pia huweza kuuwa seli za saratani.

96.Tomato zina vitamini C kwa wingi. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vitamini hivi vina kazi kubwa ya kulinda mwili na maradhi mbalimbali. Pia vitamini hivi vinakazi ya kuzuia utengenezwaji wa seli bila ya mpangilio yaani seli za saratani.

97.Wtoto wanatakiwa wapewe vyakula vya proini kwawingi zaidi. Vyakula hivi ndio vinahusika katika ukuaji wa tishu na miili yao kiujumla.

98.Kuwa na uzito wa kupitiliza ni katika sabau zinazosababisha kupata kisukari. Sababu nyingine ni kama mazingira, vyakula na mfumo wa maisha kwa mfano kutokufanya mazoezi.

99.Saratani ni katika sababu zinazoongoza kwa vifo vya watu wengi duniani. Mwaka 2004 watu 7.4 milioni walikufa kwa saratani, na hii ni asilimia 13% ya vifo vyote. Inakadiriwa kufikia milioni 13 mpaka ifikapo mwaka 2030

100.Mgonjwa wa kisukari kama atafuata maelekezo anaweza kuishi kama watu wengine bila ya kuwa na matatizo. Kwa mfano karibia watu milioni 23 marekani wanaishi na ugonjwa wa kisukari.