Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kushoto
MAUMIVU YA TUMBO KWA CHINI UPANDE WA KUSHOTO
Sehemu ya kushoto ya tumbo lako kwa chini hupatikana mwishilizo wa utumbo mkubwa. Pia kwa upande wa wanawake sehemu hii hupatikana ovari ya kushoto. Katika hali za kawaida maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto sio jambo la kuogopesha sana. Kwani maumivu haya yanaweza kuondoka yenyewe bila ya kuhitaji uangalizi wa kidaktari.
Je na wewe ni mmoja kati ya wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa shini upande wa kushoto? Je una muda gani na tatizo hili?. makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakwenda kukujuza sababu za maumivu ya tumbo sehemu ya chini upand wa kushoto.
Kama nilivyotangulia kukuijuza kuwa maumivu haya si jambo la kuogopesha. Basi ni vyema kwa haraka ukamuona daktari endapo utaona dalili zifuatazo:-A.HomaB.Sehemu husika kuwa na ugumu na maumivuC.Kuvimba kwa tumboD.Kuona damu kwenye kinyesiE.Kuendelea kuwa na kichefuchefu na kutapika kwa masik kadhaaF.Kupungua uzitoG.Ngozi kuwa na njano.
Sababu za maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto1.Kuwa na shida kwenye utumbo mkubwa.Hii hutikea pale kwenye utumbo mkubwa kunapoota kama vijifuko vijidogo. Hivi sio jambo la kuogopa sana kiafya maana mara nyingi havina madhara na hupotea vyenyewe. Hali hii huwapata sana wenye umri zaidi ya miaka 40. sasa ikitokea vijifuko hivi vimeshambuliwa na vijidudu huvimba na kuleta maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto. Dalili zake ni kama:-
A.HomaB.KichefuchefuC.KutapikaD.Tumbo kujaa na kuiwa gumuE.KuharishaF.Kukosa choo
2.Gesi tumboni.Sababu nyingine ni kujaa gesi tumboni. Gesi tumboni inaweza kusababishwa na:-A.Kumeza hewa sanaB.Kula kupitilizaC.Kuvuta sigaraD.Kutafuna bigjiiE.Chakula kutokumeng’enywa vyemaF.Kula vyakula vyenye gesiG.Kuwa na bakteria kwenye utumbo mkubwa.
3.Kuvimbiwa ama chakula kutokumeng’enywa vyema tumboni. Hali hii huplekea maumivu ya tumbo kwa juu. Maumivu haya wakati mwingine husambaa na kuathiri chini ya tumbo upande wa kushoto. Mtu pia ataona dalili kama:-A.KiunguliaB.Kuhisi kishiba na tumbo kujaaC.Kucheua gesiD.kichefuchefu
4.Ngiri henia; henia ina dalili kama:-A.Kuongezeka uvimbe maeneo ya tumboni (si kila henia)B.Maumivu kuongezekaC.Maumivu wakati unaponyanyua kituD.Kujihisi umeshiba5. kuwa na vijiwe kwenye figoVijiwe vya kwenye vigo vinatokana na mkusanyiko wa madini ya chumvi. Vijiwe hivi vinaweza kutokea kwenye figo, kibofu ama maeneo mengine kwenye mfumo wa mkojo. Vijijiwe hvi vinaweza kusababisha maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kushoto. Pia vinaweza kusababisha maumivu ya mgongo upande mmoja na nyuma pia na kwenye mbavu. Tofauti na dalili hizi pia mgonjwa anaweza kupata dalili zifuatazo:-
A.Mkojo wenye rangi ya kahawiya, nyekundu ama mawingu mawingu na haruu kaliB.Mkojo wenye maumivu makali unaotokea mra kwa maraC.KichefuchefuD.VomitingE.Homa
Maumivu ya tumbo kwa chini uapande wa kulia kwa wanawake, husababishwa na yafuatayo:-A.Tumbo la changoB.Kuota tishu za tumbo la uzazi maeneo mengineC.Kuwa na shida kwenye ovariD.Kuwa na ujauzito uliotungia njeE.Kuwa na ugonjwa wa PID
?
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dalili za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ingawa sio watu wote wenye dalili kama hizi Wana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo Ila zikitokea mtu anapaswa
Soma Zaidi...Mvurugiko katika mfumo wa chakula mwilinivunaweza kusababisha maumivu ya tumbo, kuharisha, kutapika na kuchoka pia. Lakini zipo sababu nyingine kama kuwana ujauzito. Nini ufanye endapo unasumbuliwana hali hii
Soma Zaidi...DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo.
Soma Zaidi...Kubana kwa kifuwa ni katika hali ambazo si naweza kuhatarisha maisha. Huwenda kuwa ni miongoni mwa dalili za magonjwa mengi. Je unadhani na HIv na UKIMWI ni moja ya magonjwa hayo?
Soma Zaidi...Malaria inaweza kumpata mtu yeyote bila ya kujali mri.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ni Maambukizi ambayo hutokea kwenye mifupa kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu dalili za figo.figo husawazisha maji mwilini pamoja na kuchuja mkojo.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu. Yafuatayo Ni madhara ya minyoo;
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi aina za ajali kwenye kifua,pamoja na kifua kuwa na sehemu mbalimbali na pia na ajali ambazo utokea Huwa za aina mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na kisukari
Soma Zaidi...