Posti hii inahusu zaidi njia za maambukizi ya Homa ya inni, Homa ya inni usababishwa na virusi viitwavyo Hepatitis B, huwapata watu wote hasa wale wenye umri chini ya miaka mitano.
Njia za maambukizi ya Virusi vya Hepatitis B.
1. Njia ambazo virusi vya Hepatitis B uenea ni kama zinafanana na njia za virus vya Ukimwi kwa hiyo tujitahidi kujua namna Homa ya inni inavyoambukizwa tunaweza pia kuepuka ugonjwa huu na kuweza kuishi kawaida pasipo Ugonjwa huu .
Kwa hiyo Tunapaswa kushika masharti katika kupambana na Homa ya inni hasahasa kupata chanjo ya Homa ya inni kwa sababu unatolewa bure kwa watoto Ila watu waziy ni malipo. Kwa hiyo tunapaswa kujua njia za maambukizi kama vile.
2. Kumwongezea mtu damu, kutoka kwa mwenye virusi vya ugonjwa huu kwenda kwa yule ambaye Hana.
Kwa hiyo kabla ya kumwongezea mtu damu kitu Cha kwanza anapaswa kupima Ili kuangalia kama Kuna maambukizi kwenye damu, baada ya kuona kama kuna maambukizi kwenye damu , mtu hasipewa damu hiyo,
3. Mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua au mtoto akiwa tumboni kwa mama.
Ugonjwa huu wa inni unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia kwa Mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua au wakati mtoto akiwa tumboni kwa mama kwa hiyo mama akiwa anna mimba anashauliwa kupima ugonjwa wa inni Ili kuhakikisha afya yake na kuepuka hali Ile ya kumwambikiza mtoto.
Pia na wakunga wanapaswa kuwa macho wakati wa kumzalisha Mama Ili kuepuka kuendelea kuleta madhara kwa Mtoto na jamii kwa ujumla.
4. Maambukizi ya Homa ya inni yanaweza kupitia kwenye sehemu za uwazi kama vile kwenye vidonda,michubuko na Kuna wengine wanaweza kupata kupitia kwa jasho la mwilini kama likigusana na sehemu ya uwazi.
5. Kufanya ngono zembe.
Pengine ugonjwa huu unaweza kupitia kwenye ngono zembe kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa kupitia kujamiiana kwa hiyo watu wanapaswa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana Ili kuepuka hali ya kusambaa kwa ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, na pia elimu inabidi kutolewa kwa jamii Ili kuepuka madhara makubwa zaidi ya kuenea kwa ugonjwa wa Homa ya inni.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowPosti hii inazungumzia kuhusiana na was Uharibifu wa seli nyekundu za damu ambapo hujulikana Kama Ugonjwa wa Hemolytic uremic (HUS) ni hali inayotokana na uharibifu usio wa kawaida wa seli nyekundu za damu mapema. Mara tu mchakato huu unapoanza, seli nye
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za maumivu ya jino
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa na tatizo la kukosa nguvu, kuchoka ama kuhisi viungi vinelegea. Endelea na post hii.
Soma Zaidi...Post hii inaenda kuzungumzia zaidi kuhusiana na mimba zinazoharibika . mimba huweza kuaribika au kutoka anzia miezi 3 na kuendelea .
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kwa mtu ambaye ana tatizo kwenye mishipa ya retina,ni tatizo ambalo uwakumba wafu wengi wenye matatizo ya kisukari.
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza maana ya homa ya ini. Pia utajifunza chanzo kinachosababisha homa ya ini. Makala hii itakuwa endelevu hivyo usikose muendelezo wake.
Soma Zaidi...