4.SURATUL-MASAD
Sura hii pia ni katika sura za kushuka Maka. Wanaeleza Maulamaa kuwa sababu ya kushuka sura hii ni kuwa mtume (s.a.w) alipopewa amri ya kulingania bila ya siri aliwaita watu wa Maka ili awalinganie na hapo baba yake mdogo Mtume (s.a.w) aitwaye Abdul a€?Uzza ambaye Qurani imemuita Abuu Lahabi yaani baba wa moto alitowa maneno ya upumbavyu na upuuzi juu ya ujumbe wa Allah na hapo Allah akateremksha sura hii.
Huyu Abu Lahab jina lake hasa ni Abdul Uzza, naye alikuwa baba mdogo wa Mtume s.a.w. Neno Abuu Lahab - baba wa miali ya moto - ni jina ambalo hutumika kwa ajili ya mtu ambaye hali yake n nya asili ni ya moto na ya uasi, na pia hutumika kwa ajili ya mtu ambaye anawachochea wengine. Hivyo bwana huyu amepangwa jina hili na Qur'an kwa sababu ya uadui wake kwa Mtume s.a.w.
Siku ya kwanza Mtume alipowaita Wakureishi ili kuwaeleza habari za ujumbe wake, huyu Abu Lahab, alimkaripia akasema, "Uangamizwe, je umetuitia maneno haya!" (Bukhari). Na ilikuwa desturi yake kila mara kumfuata Mtume aendako na kuwaambia watu wasimsikilize, akisema, Mtume ni jamaa yake na ni mwehu. Kadhalika mkewe Abu Lahab aliyeitwa Ummi Jamil bint Harb, dada wa Abu Sufiyan, alikuwa mwanamke mbaya sana aliyekuwa anamwudhi sana Mtume na kumsumbua na hata kumsingizia-singizia mambo ya upuuzi. Na kwa sababu ya masingizio yake ameitwa mchukuzi wa kuni (Bukhari), ambazo kwazo amejikokea moto wa Jahanamu, (Razi).
FADHILA ZA SURAT HII
fadhila za sura hii ni kama za sura nyingine kuwa utapata thawabu. Hakuna hadithi sahihi iliyonukuliwa kueleza fadhila za surahii kama zinavyotajwa sura nyingine. zipo baadhi ya nukuu zinanukuliwa kuwa Mtume (s.a.w) amesema "mwenye kusoma sura hii, hatakuwa makazi sawa na Abuu lahab". Haikunukuliwa hadithi hii katika vitabu vikuu va hadith, na sikuweza kupata ushahidi juu ya usahihi wa hadithi hii.