Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr.
Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr. Wakawa nao wanabuni miungu ya vitu vilivyo hai na visivyo hai. Moja ya miungu waliyoibuni ni ng'ombe mwenye sifa maalum. Asiye mzee sana wala mchanga, mwenye rangi ya dhahabu na asiyefanyishwa kazi. Kwa hiyo pamoja na kuwa baadhi ya Mayahudi walifuata sheria ya Musa(a.s), lakini bado athari ya ibada ya ng'ombe ikawa imesalia katika nafsi zao.
Katika mazingira hayo, Nabii Musa(a.s) alipewa amri na Mola wake awaamrishe wachinje ng'ombe. Huu ukiwa ni mtihani wa imani kwao kuthibitisha kwamba kweli wamemuamini Allah(s.w) au la. Mtihani huu ukawa mgumu sana kwao. Wakajaribu kuukwepa kwa kuleta maswali kadhaa ya udadisi. Lakini kila walivyozidi kudadisi juu ya ng'ombe waliyeambiwa wamchinje ndivyo walivyojiingiza mahali pagumu zaidi. Kwani majibu waliyokuwa wakiyapata yaliwataka wamchinje ng'ombe mwenye sifa sawa na yule wanayemuabudu. Basi hatima yake wakamchinja japo kwa shingo upande.
Fundisho lililokusudiwa lilipatikana kwani kile walichokidhania kitakatifu hata kukiabudu walikichinja kwa mikono yao wenyewe na wala hawakupata dhara lolote. Qur'an yabainisha tukio hili katika aya zifuatazo:
"Na Musa alipowaambia watu wake: "Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje ng'ombe". Wakasema: "Je! Unatufanyia mzaha?" Akasema "(La) Najikinga kwa Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa wajinga. Wakasema: "Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni (wa umri) gani (ng'ombe huyo)?" Akasema: "Hakika Yeye anasema kwamba ng'ombe huyo si mzee wala si mchanga, bali ni wa katikati baina ya hao. Basi fanyeni mnavyoarishwa". Wakasema: "Tuombee kwa Mola wako atupambanulie ni vipi hali yake, hakika ng'ombe wanafanana; (basi yupi)? Na kwa hakika kama Mungu akipenda (tutafuata) tuwe wenye kuongoka". Akasema: "Yeye anasema: Kuwa huyo si ng'ombe aliyetiwa kazini kulima ardhi wala kutilia maji mimea, safi kabisa rangi yake, hana kipaku ndani yake". Wakasema: "Sasa umeleta (maneno ya) haki". Basi wakamchinja, na walikuwa mbali na kufanya hayo". (2:67-71).
Pamoja na fundisho kuu tulilolitaja awali la kujenga hoja dhidi ya shirk; lakini pia aya zinatutanabahisha kuwa tusijaribu kuzikwepa amri za Allah(s.w) kwa kuleta maswali ya udadisi na visingizio. Maadhali jambo limethibiti kuwa ni amri ya Allah basi hatuna hiari bali ni kulitekeleza kwa moyo mkunjufu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii surat At-Takaathur ilishuka Makka, na hizi ndio sababu za kushuka kwa sura hii
Soma Zaidi...(i)Mtume Muhammad (s.
Soma Zaidi...Surat Al-Asri imeteremshwa Makka, na hapa utazujuwa sababu za kushuka kwa sura hii
Soma Zaidi...Qur-an inavyogawa MirathiMgawanyo wa mirathi umebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili.
Soma Zaidi...TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao.
Soma Zaidi...Zijuwe sababu kuu za kushuka surat Al-Humazah katika quran
Soma Zaidi...Maulamaa katika elimu ya Quran wametofautiana juu ya aya ya mwisho kushuka. Hata hivyo hapa nitakutajia ambayo imependekezwa zaidi
Soma Zaidi...surat Zalzalah ni sura ya 99 katika mpangilio wa Quran, na ina aya 8. Sura hii imeteremshwa Madina ila pia kuna kauli zinathibitisha kuwa ni ya Makkah. Katika hadithi iliyopewa daraja la hassan na Imam Tirmidh Mtume S.A.W amesema kuwa kusoa surat Zilzalah
Soma Zaidi...SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah.
Soma Zaidi...