Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.
VYAKULA VYA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME
Ugumba si kwa wanawake tu, wapo hata wanaume wanatatizo hili. Lakini kutokubebesha mimba ama kubeba mimba pekee haimaanishi kuwa wewe ni mgumba. Mwanaume kumbebesha mimba mwanamke kunategemea mambo mengi kutoka kwa mwanaume mwenyewe na kwa mwanamke mwenyewe. Katika makala hii nitazungumzia kipengele kimoja tu nacho ni tatizo la kutokuwa na mbegu bora za kiume.
Mwnaume anapokojoa bao moja anatoa mbegu zaidi ya milioni 300. katika mbegu hizo ni moja tu ndiyo intakayofanikiwa kitungisha mimba. Mamimioni ya mbegu haya yanakufa bila hata ya kulifikia yai, kutokana na udhaifu wao, kutoweza kuogelea vyema, ukali wa tindikali katika tumbo la mwanamke n.k. sasa ili mwanaume aweze kubebesha ujauzito anatakiwa atoe mbegu bora na imara zinazoweza kuishi ndani ya tumbo la mimba kwa muda mrefu.
Inatokea baadhi ya wanaume mbegu zao zinakuwa sio imara kutosheleza. Hii inakuwa ni ngumu kubebesha ujauzito. Lakini kumbuka kama mambo mengine yakiwa sawa hata mwenye mbegu dhaifu inaweza kubebesha mimba endapo itakuwa ni siku sahihi ya kukutana na yai, hazitachukuwa muda kukutana na yai ama zilitolewa nyingi.
Sasa ikiwa tatizo ni hili la mbegu ni dhaifu, je nitawezaje kuboresha mbegu zangu? Yes ni swali zuri sana, na inapasa hasa kulijuwa jibu lake. Mbegu utaweza kuziporesha kwa kubadilisha mlo ama kutumia dawa ama njia nyinginezo. Miongoni mwa njia hizo ni:-
Njia za kuboresha mbegu za kiume.
1.Badili mlo wako.
Muonekano wako leo ni sawa na chakula unachokila. Ladha na ubora wa manii na mbegu za kiume pia hutegemeana na unachokila. Kama unataka kuboresha mbegu za kiume kwanza anza na kubadili mlo wako. Jitahidi kula vyakula vifuatavyo:-
A.Vitamini B-12
Vitamini hivi unaweza kuvipata kwenye nyama, samaki na maziwa. Vitamini hivi husaidia sana katika afya ya mbegu za kiume.
B.Vitamini C
Hivi unaweza kuvipata kwenye machungwa, viaz mbatatai, nyanya, apinach na kwenye matunda yenye uchachu na mapapai na mananasi. Vitamini C pia ni muhumu kwa afya ya mfumo wa kinga
C.Kula vyakula jamii ya korosho na karanga
D.Kula vyakula vyenye lycopene. Vyakula hivi kuwa na rangi nyekundu kama tikiti na nyanya
E.Kula vyakula vyenye madini ya zinc kwa wingi. Unaweza kupata madini haya kwenye nyama, samaki wa baharini kwenye magobeta jamii ya kaa, mimea jamii ya kunde, kula mbegu kama mbegu za maboga na nyingine, maziwa, mayai, jamii ya korosho, baadhi ya mboga za majani kama maharagwe ya kijani na nafaka nzima.
2.Fanya mazoezi ya mara kwa mara.
Mazoezi si kwa ajuli ya hili tu bali pia ni kwa ajili ya kuboresha afya kwa ujumla. Si lazima ufanye mazoezi mareefu, hapana kwa uchache pia inatosha.
3.Punguza kuvaa nguo za ndani zenye joto.
Afya ya mbegu za kiume inategemea pia joto la mwili wako. Hakikisha korodani unazipa hewa ya kutosha. Usivae nguo za kubana nyingi kama chupi, si salama kwa wanaume. Boxa kama haibani sana inatosha.
4.Punguza unywaji wa pombe, na soda kama unakunywa kwa kiasi kikubwa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia Malaria kwa wajawazito na watoto wao wakiwa bado tumboni, tunajuwa wazi kuwa wajawazito wakipata Malaria inaweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyo ili kuzuia tatizo hili zifuatazo ni njia zilizowekwa ili kuz
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa Mama mjamzito, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama mjamzito, hizi Dalili zisipofanyiwa kazi mapema zinaweza kuleta shida kwa Mama kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua Dalili hizi na kuchukua hatua endapo zitajio
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo mbalimbali yanayodhoofisha afya za wanaume, kwa wakati mwingine wanaume ukosa kujiamini kwa sababu ya mambo ambayo yanaadhiri afya za wanaume.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na hatua za kujikinga na Maambukizi ya Uvimbe kwenye ovari na kwenye mirija ya uzazi
Soma Zaidi...Posti inahusu nzaidi kufunga kwa mishipa ya machozi ya mtoto kwa kawaida mishipa ya mtoto inapaswa kufunguka baada ya mwaka mmoja lakini kwa wengine ubaki imefungwa hata baada ya mwaka mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kwa mtoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia ugumba, ni njia ambazo utumiwa na wapenzi ambao wameshindwa kupata watoto hasa kwa wale ambao wamezaliwa wakiwa na uwezo wa kupata watoto lakini kwa sababu tofauti tofauti wanashindwa kupata watoto kwa hiyo njia zifu
Soma Zaidi...Kuna watoto wengine huanza kucheza mapema kuliko watoto wengine. Tunapozungumzia kucheza kwa mtoto aliye tumboni yaani mimba hapa inatubidi tuangalie kwa undani zaidi, je ni muda gani mtoto ataanza kucheza?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kugundua tatizo lake na kutoa msaada pale penye uhitaji.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa Ugonjwa wa fangasi,ni sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha fangasi.
Soma Zaidi...