DALILI ZA KUTOKA KWA MIMBA

Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Yaani karibia robo ya mimba zinazopatikana hutoka. Kitendo hiki cha kutoka kitaalamu huitwa misscarriage. Hiki ni kitendo cha kupotea kwa ujauzito kabla ya wiki ya 20. karibia mimba nyingi hutoka ndani ya miezi mitatu ya mwanzo. Mimba iliyotoka inakuwa na dalili kadhaa. Pia wakati mwingine dalili hizi huashiria kuwa ujauzito upo hatarini.

 

Dalili hizi ni kama;

  1. Kutokwa na damu nyingi ukeni. Mjamzito anaweza kuona damu ikitoka ikiwa chache yaani matone kadhaa ama madoa hii ni kawaida. Lakini ikiwa nyingi huashiria hatari kwa ujauzito.
  2. Kupungua uzito kwa ghafla. Bila ya kujuwa sababu yeyote mjamzito anapungua uzito wake kwa ghafla sana.
  3. Kutokwa na uteute wa rangi ya pink iliyo pauka kwenye uke
  4. Kuondoka kwa dalili za ujauzito kwa ghafla
  5. Kutokwa na tishu yaani kama vipande vya nyama vinatoka ukeni
  6. Maumivu makali ya mgongo ama tumbo