TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO
KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.
KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO
Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito. Kitaalamu hali hii hutambulika kama odema. Wakati mwingine si miguu tu ndio huvimba bali mikono, nyayo na uso huweza kuvimba. Ijapouwa huku kukuvimba kwa ghafla kwa uso na mikono ni dalili ya maradhi mengine kama preeclampsia.
Hali hii ya kuvimba kwa miguu huweza kuwapata wanawake katika kipindi chote cha ujauzito, iwe wajauzito ulio mchanga, ama kipindi cha katikati cha ujauzito ama kipindi cha mwisho cha ujauzito. Katika hali ya kawaida kuvimba kwa miguu kwa wajawazito sio jambo la kusumbua kiafya yaani kusema kuwa ni tatizo kubwa. Hapana hii ni kawaida kwa wajawazito.
Kuvimba huku kunaweza kuwa ni tatiko kama kutaweza kuambatana na baadhi ya matatizo mengine ya kiafya kama maumivu makali ya kicha, kizunguzungu, kutokwa na damu, kushinwa kuona kwa usahihi ama kushinwa kupumua ama kupumua kwa taabu, hali hizi kuweza kuashiria hatari. Ni vyema mjamzito awahi kituo cha afya kama ana hali hizi.
Sababu za kutokea kwa vimbe hizi ni mabadiliko ya mwilini yanayopatikana wakati wa ujauzito. Kuongezeka kwa damu mwilini na kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kuchangia zaidi hali hii. Halikadhalika ongezeko la homoni maalumu zinazotolewa wakati wa ujauzito. Haya yote kwa pamoja huchangia kutokea hali hizi za kuvimba.
Tofauti na sababu hizi pia zipo nyingine kama mabadiliko ya hali ya hewa. Hapa tunazungumzia joto, ambalo pia ni sababu ya kuvimba. Sababu nyingine ni kutokunywa maji ya kutosha, matatizo ya homoni yaani homone imbalance. Kukaachini kwa muda mrefu ukaaji wa kukalia miguu. Ama kusimama kwa muda mefu.
Kupunguza ama kuepuka hali hii ni vyema kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kukaa kivulini, kulalia upande kwa kushoto unapolala. Hakikisha unakula mlo kamili, hakikisha kuwa unakunywa maji ya kutoka kwa siku. Na hata ukizidisha ni faida kwako. Epuka kusimama kwa muda mrefu ama kukaa kwa kukalia mguu. Epuka kukaa kwa muda mrefu kwa staili moja. Kuna matatizo mengu ya kiafya yanayoambatana na ujauzito, ni vyema mjamzito akiwa makini.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 web hosting 👉3 ai web app 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Uchafu unaotoka ukeni na rangi zake.
Posti hii inahusu zaidi uchafu unaotoka ukeni na rangi zake, kwa kawaida ukeni utolewa uchafu, uchafu huo unaweza kuwa kawaida na unaweza kuwa na rangi mbalimbali kutokana na kuwepo kwa Maambukizi.
Soma Zaidi...anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu
Abali mkuu Nina mdogo wangu anawashwa Sana sehemu ya Siri mpaka anatoka vipele vingi kwenye mapaja korodani zake zimebadilika kuwa nyekundu na zenye kutisha uume wake nao umekuwa unakama mabaka umebabuka aisee nime angaika Sana kumtibia mpaka nakata tamaa
Soma Zaidi...Habari nilitaka kujua kuhusu ugonjwa wa fungusi kwenye uume
Je na wewe unasumbuliwa na fangasi wenye uume. Post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...je ute wa uzazi uanza kuonekana siku ya 14 tu au kabla ? Na je mimba ya siku tatu inaweza kucheza?
Miongoni mwa dalili zamwanzo za ujauzito ni maumivu ya tumbo ama kupatwa na damu kidogo. Mabadiliko ya ute ute sehemu za siri ni katika baadhi ya dalili. Endelea na makala hii utajifunza zaidi.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa kisukari wakati wa ujauzito.
Posti hii inaelezea ugonjwa wa kisukari wakati mama akiwa mjamzito.na yafuatayo ni Mambo hatari yanayotokea wakati Mama akiwa na ujauzito.
Soma Zaidi...