SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Yaani karibia robo ya mimba zinazopatikana hutoka. Kitendo hiki cha kutoka kitaalamu huitwa misscarriage. Hiki ni kitendo cha kupotea kwa ujauzito kabla ya wiki ya 20.
Sababu za kutoka kwa mimba:
- Sababu za kurithi (genetics): hutokea mwanamke akarithi hizi sabau kutoka kwenye familia yake. Sababu hizi huenda zikapelekea matatizo ambayo baadaye huchangia mimba kutoka. Matatizo haya ni kama
- Mtoto kutokuendelea kukuwa tumboni
- Kiini tete (embriyo) kutokutengenezwa
- Placenta kuwa kubwa zaidi tofauti na kawaida.
- Afya ya mama; hutokea mwanamke mjamzito afya yake ikawa ni sababu ya ujauzito wake kutoka. Mwanamke akiwa na maradhi yafuatayo ujauzito wake unaweza kuwa hatarini:
- Kisukari
- Maradhi ya moyo
- Presha ya kupanda (hypertension)
- Maradhi ya figo
- Maambukizi; mwanamke mjamzito anweza kuweka ujauzito wake hatarini kama atakuwa na maambukizi ama mashambulizi ya maradhi kama:
- Chlamydia
- Gonoria
- Syphilis
- Malaria
- Ukimwi
- Udhaifu wa cervix; cervics ni mlango wa nyumba ya mimba.
- PCOS (Polycystic Ovary Syndrome). hii hupelekea ovary kuwa kubwa tofauti na kawaida. Ovary ndio sehemu ambayo mayai ya mwanamke hutengenezwa.