FANGASI

Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi ni hatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakili kama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathiri mwili wa binadamu.

 

Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina za fangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Fangasi wanaweza kuathiri makwapa, vidole, sehemu za siri kwenye tumbo na maeneo mengine.

 

Fangasi wa sehemu za siri husababishwa na fangasi waitwao candida. Hawa wanaweza kuathiri sehemu za siri kuzungukia uume ama uke. Kunatafiti zinaonesha kuwa fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi. Japo tafiti zaidi zinahitajika ili kuthibitisha hili.

 

FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI DALILI ZAO KWA WANAUME

  1. Kuvimba kwa kichwa cha uume
  2. Kuwasha kwa sehemu za siri, hususan kichwa cha uume
  3. Uume kuwa mwekundu kwa kuchubuka ama kuvumba ama kwa mashambulizi ya fangasi hawa.
  4. Kuota kwa mapele na maruturutu kwenye uume
  5. Kuwasha uume ama kuungua moto kwa uume.
  6. Kutokwa na majimaji meupe kwenye uume, majimaji haya huwa na harufu mbaya.
  7. Maumivu wakati wa kukojoa na kufanya tendo la ndoa.

DALILI ZA FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE

  1. Maumivu na miwasho kwenye mashavu ya uke na sehemu ya juu ya uke
  2. Maumivu wakati wa kukojoa ama kufanya tendo la ndoa
  3. Uuke kuwaka moto kwa ndani
  4. Kuvimba kwa mashavu ya uke na kuwa mekundu
  5. Kuot mapele na maruturutu kwenye uke
  6. Kutokwa na majimaji kwenye uke
  7. Kutokwa na majimaji mazito meupe na yenye harufu mbaya kwenye uke.

 

WATU WALIO HATARINI KUPATA FANGASI HAWA

  1. Wachafu
  2. Kuwa na mikunjomikunjo kwenye ngozi kama kitambi
  3. Wenye kisukari
  4. Wenye HIV
  5. Wenye saratani
  6. Wenye kutumia baadhi ya madawa ya kuzuia mimba
  7. Wajawazito

 

NJIA ZA KUPAMBANA NA FANGASI HAWA

  1. Kuwacha kutumia madawa ya kusafishia ama kuunga uke
  2. Kutokuvaa nguo mbichi
  3. Kutokuvaa nguo za kubana hususani za mpira
  4. Kuwa msafi muda wowote
  5. Kuosha kichwa cha uume na ngozi ya govi mara kwa mara
  6. Kuosha uke mara kwa mara
  7. Kutumia pedi zilizo kavua na safi na kubadilisha mara kwa mara