Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo UKIMWI hutokea
SASA UKIMWI UNATOKEAJE?
Seli ndio matofali yaliyojengea miili yetu. Ndani ya miili yetu kuna aina nyingi za seli, na seli za damu. Ndani ya damu pekee kuna aina zisizopunguwa tatu za seli. Kuna seli hai nyekundu, nyeupe na seli sahani. Kila seli kati ya hizi ina kazi zake. Sasa hii seli hai nyeupe yenyewe ndio inakazi ya kupigana na vijidudu vya maradhi vinapoingia katika miili yetu. Vijidudu hivyo vinaweza kuwa bakteria, virusi ama fangasi. Seli hizi ndizo ambazo ambazo huitwa CD4.
Sasa virusi vya VVU vinapoingia mwilini vinaanza kuharibi hizi seli ambazo zinalinda mwili. Kawaida mtu anaweza kuwa na seli hizi 500 mapa 1500 katika kipimo kimoja. Sasa VVU vinaanza kuziharibu hizi na kupunguza idadi yake. Na kila seli hizi zikipunguwa ndipo mfumo wa kinga unavyoendelea kuharibika na ndivyo maradhi yanapozidi kupata nafasi ya kuingia mwilini.
Sasa endapo zimeharibiwa na kufika idadi ya 200 katika kipimo kimoja hapa mtu huyu ataambiwa ana Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI. Katika hatuwa hii mtu atakuwa akinyemelewa na maradhi nyemelezi kama fangasi, kifuwa kikuu, na mengineyo.
Endapo mgonjwa atatumia ARV mapema anaweza kukaa miaka mimngi sana bila ya kufikia hatuwa hii. Kuna umuhimu wa kutumia ARV mapema, sababu hizo ni kama:-
1.Kupungua maambukizi ya VVU
2.Kulinda afya ya mtu
3.Kupunguza uharibifu wa seli
4.Kulinda mwili dhidi ya maradhi nyemelezi
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu presha ya kushuka/ hypotension
Soma Zaidi...Posti hii inahusu sana kuhusu ugonjwa wa ebora. Ugonjwa huu usababishwa na virusi.Virusi hivyo husababisha kutokwa na damu nyingi mwilini kutokana na kupasuka kwa mishipa ya damu
Soma Zaidi...maambukizi ya kawaida ya zinaa (STI), Hujulikana Kama Chlamydia. Huenda usijue una Ugonjwa huu kwa sababu watu wengi hawapati dalili au ishara, kama vile maumivu ya sehemu za siri na kutokwa na uchafu kutoka kwa uke au uume. Maambukizi haya huathiri
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na kisukari
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili na ishara za shambulio la moyo. Shambulio la moyo huzuia damu yenye oksijeni kufika kwenye moyo hivyo hupelekea tishu kufa. Na Ugonjwa huu mtu akicheleweshewa matibabu huweza kupata mshtuko wa moyo mpaka kifo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu na kwa kitaalamu huitwa retention of urine.
Soma Zaidi...post hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa utando wa pua unaoonyeshwa na mchanganyiko wa dalili zifuatazo: Kupiga chafya Msongamano wa pua Muwasho wa kiwambo cha sikio Kuwasha kwa pua na koromeo Uvimbe huu hutokea ikiwa mashambulizi ya kupiga chafya,
Soma Zaidi...