Navigation Menu



VIJUE VITAMINI, CHAZNO CHAKE, NA KAZI ZA VITAMINI MWILINI

VIJUE VITAMINI, CHAZNO CHAKE, NA KAZI ZA VITAMINI MWILINI

NINI VITAMINI NA NI ZIPI KAZI ZAKE MWILINI?

Bongoclass-afya

NINI VITAMINI NA NI ZIPI KAZI ZAKE MWILINI?

VITAMIN NA KAZI ZAKE
NINI MAANA YA VITAMINI?
Vitamini ni kampaudi ogania ambazo zinahitajika na mwili kwa ajili ya ukuaji wa mwili na utendaji wa michakato ya kibaiolojia ndani ya miili (metabolism), na ni viruubisho ambavyo havitengenezwi ndani ya miili yetu. Vitamini vipo katika makundi makuu mawili ambayo ni fat soluble na water soluble. Pia makundi ya vitamini ni A, B, C, D na K.


Fat soluble ni titamini ambavyo mwili unaweza kuvihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye vitamini hivi ni kama A, D, E na K. Hii ina maana hatuhitaji tule vyakula vyenye vitamin hivi kila siku. Watwer soluble ni vitamini ambavyo mwili hauwezi kuvihifadhi mwilini hivyo baada ya kula chakula mwili hufyonza kiasi cha vitamini hivi na kuvitumia. Hivyo tunahitajika tule vyakula vyenye vitamini hivi kila siku. Vitamini hivi ni kama D na C.


VITAMINI A
Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene. Vitamini A ni moja kati ya vitamini vingi. Vitamini vingine ni viamini b, C, D, E, K. unaweza kupata vitamini A sana kwenye mboga za majani za kijani, maini, mayai, maziwa, karoti na spinach. Katika makala hii tutakwenda kuona mengi kuhusu vitamini A, kazi zake, vyakula vya vitamini A pamoja na athari za upungufu wake mwilini:


Yaliyomo:
1.Maana ya vitamini A
2.Kazi za vitamini A
3.Vyakula vya vitamini A
4.Upungufu wa vitamini A
5.Athari za kuzidi kwa vitamini A


Maana ya vitamini A
Vitamini ni aina ya fat soluble vitamini ambayo ni kampaind ogania (organic compound) inayopatikana katika makundi kama retinol, retinal, retinoic acid na provitamin ambazo ni beta-carotene. Vitamini A ni muhimu katika ukuaji, uboreshwaji wa mfumo wa kinga na kuboresha afya ya macho.


Ugunduzi wa vitamini A umeanza toka miaya ya 1816 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Francois Magendie alipokuwa akimfanyia uchunguzi mbwa mgonjwa. Baada ya hapo tafiti mbalimbali zikafata mwaka 1912, 1913, 1918, 1920 na 1939 na 1947. vitamini A vimepewa jina hili katika tafiti za mwaka 1920.


Kazi za vitamini A
1.Husaidia katika afya ya macho yaani kuona
2.Husaidia katika ukuaji
3.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
4.Husaiia katika ukuaji wa mimba na mtoto aliye tumboni
5.Husaidia katika afya ya mifupa
6.Husaidia katika afya ya ngozi
7.Husaidia katika afya ya meno
8.Husaidia katika utengenezwaji wa uteute mwilini.


Vyakula vya vitamini A
1.Maini
2.Karoti
3.Viazi vitamu
4.Spinachi
5.Maboga
6.Pilipili
7.Maembe
8.Njegere
9.Maziwa
10.Mayai
11.Mboga za majani za rangi ya kijani



Upungufu wa vitamini A
Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini A huathiri watoto wanaokadiriwa kufikia 670,000 waliochini ya umri wa miaka mitano kila mwaka. Pia inakadiriwa kuwa watoto katika ya 250,000 na 500,000 wanakuwa vipofu katika nchi zinazoendelea kila mwaka. Tafiti zinathibitisha kuwa chanzo kikuu cha upofu kwa watoto ni upungufu wa vitamini A.


Athari za vitamini A kupitiliza
Endapo mtu atakuwa na vitamini A vingi ndani ya mwili hata vikapitiliza kiwango ambacho mwili unaweza kudhibiti, athari zifuatazo zinaweza kutokea:-
1.Mkusanyiko wa sumu mwilini
2.Kichefuchefu
3.Kuwshwa
4.Kukosa hamu ya kula
5.Kutapika
6.Kuona maluelue
7.Maumivu ya kichwa
8.Kupotea kwa nywele na misuli
9.Maumivu ya tumbo na uchovu



VYAKULA VYA VITAMINI B
Vitamini B ni katika water soluble vitamin ambavyo vina kazi ya kuhakikisha kuwa michakato yote ya kikemikali mwilini inakwenda vizuri. Na hapa tunazungumzia kitaalamu metabolism. vitamini B vipo katika makundi mengi kma B1, B2, B3, B5, B6, B7 na B12. katika makala hii nitakwenda kukueleza maana ya vitamini hivi, nini kazi zake hasa mwilini, wapi nitapata vitamini B na je ni zipi dalili za upungufu wa vitamini hivi.


Yaliyomo
1.Maana ya vitamini B
2.Makundi ya vitamini B
3.Kazi za vitamini B
4.Vyakula vya vitamini B
5.Upungufu wa vitamini B
6.Athari za kuwa na vitamini B kupitiliza


Vitamini B ni nini?
Vitamini B ni katika kundi la vitamini vinavyofahamika kama water soluble vitamin. vitamini B ni kundi la vitamini ambavyo vinafanana sifa lakini vina utofauti kidogo. Vitamini B ndani ya miili yetu vinafanya kazi ya kuhakikisha kuwa michakato ya kikemikali inafanyika, michakato hiyo kitaalamu inafahamika kama metabolism.


Metabolism hii ni michakato ya kikemikali inayofanyika ndani ya seli kwa ajili ya mambo makuu matatu nayo ni:-
A.Kubadili chakula kuwa nishati (nguvu)
B.Kubadili chakula ama nishati kkuwa protein, carbohydrate, lipids na nucleic acid.
C.Kuondoa uchafu na sumu mwilini (nitrogen waste)
Hivyobasi michakato hii yote ili ifanyike kwa ufasaha na ufanisi vitamini B vinahitajika katika miili yetu. Endelea kusoma makala hii ukaone kazi za vitamini B.


Makundi ya vitamini B
Makundi hayo ya vitamini B ni:
1.B1 kitaalamu huitwa thiamine, hivi vimegunduliwa mwaka 1910 na mwanasayansi iliyeitwa Umetaro Suzuki. Pia mwaka 1912 mwanasayansi aliyeitwa Casimir Funk aligundua thiamine.


2.B2 kitaalamu huitwa riboflavinhivi navyo vimegunduliwa mwaka 1926 na wanasayansi wawili wanaokwenda kwa majina D.T Smith na E.G Hendrick.


3.B3 pia hutambulika kama niacin au nicotinic acid kundi hili limegunduliwa mwaka 1937 na mwanasayansi anayekwenda kwa jina la Conrad Elvehjem.


4.B5 na yo pia huitwa pantothenic acid, kundi hili limegunduliwa mwaka 1933 na Roger J. Williams


5.B6 pia huitwa pyridoxine, pyridoxal, au pyridoxamine imegunduliwa na Paul Gyorgy mwaka 1934.


6.B7 pia hufahamika kama biotin mwanasayansi aitwaye Margaret Averil Boas aliigundua vitamini hii miaka ya 1900


7.B9 pia hujulikana kama folic acid Mwanasayansi kwa jina la Lucy Wills aliigundua mwaka 1983


8.B12 ama cobalamins hii imegunduliwa na jopo wanasayansi mbalimbali.


Kazi za vitamini B N upungufu wa vitamini B mwilini
Kama tulivyoona kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-


B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.


B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.


B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo



B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.


B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.



B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.


Vyakula vya vitamini B
Tunaweza kupata vitamini B kwenye vyakula vifuatavyo:-
1.Nyama
2.Nafaka kama mchele, mtama, mahindi n.k
3.Mimea jamii ya maharagwe kama kunde
4.Viazi
5.Ndizi
6.Pilipili
7.Mayai
8.Mimea jamii ya karanga na alizeti
9.Mboga za majani zenye kijani iliyowiviana na kutia weusi kama spinachi
10.Matunda kama palachichi na ndizi


Dalili za upungufu wa vitamini B
1.Kupata ugonjwa wa Anaemia huu ni upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini
2.Matatizo kwenye ngozi
3.Kupata vidonda kwenye mdomo, ma kupasuka kwa mdomo
4.Misongo ya mawazo ama kuchanganyikiwa
5.Kuharisha
6.Kupotesa kumbukumbu kwa urahisi
7.Misuli kupoteza ujazo
8.Kubadilika badilika kwa mood (fikra na hisia) yaani mara umekasirika mara umefurahi


Athari za kuwa na vitamini b kupitiliza
1.Kichefuchefu
2.Kuona maluelue
3.Kutapika
4.Kuharisha
5.Maumivu ya tumbo
6.Shida kwenye ngozi
7.Kuzidi kwa kiu


Makala nyingine kwa ajili yako:
1.Vyakula vya protini
2.Vyakula vya vitamin K
3.Vyakula vya vitamini C
4.Afya ya uzazi
5.Afya na magonjwa




VYAKULA VYA VITAMINI C
Vitamini C ni katika vitamini muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Vitamini hivi vina sifa ya antioxidant. Antioxidant zenyewe ndani ya mwili ndizo ambazo husaidia kuupa mwili nguvu na kinga ya kupamba na na sumu, na vijidudu shambulizi. Vvitamini C ina pendelewa kuwepo ndani ya miili yetu kwa wingi muda wowote. Wapo wataalamu wa afya wanapendekeza kutumia vitamini C kwa ajili ya kupunguza uwezekeno wa kupata mafua na homa ya mafua mara lkwa mara. Katika makala hii nimekuandalia somo zima kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.


Yaliyomo
1.Maana ya vitamini C
2.Vyakula vya vitamini C
3.Kazi zake mwilini
4.Dalili za upungufu wa vitamini C
5.Maradhi yaletwayo na upungufu wa vitamini c
6.Athari za kuwa na vitamini C kupitiliza


Maana na Historia ya vitamini C
Vitamini C kitaalamu pia hufahamika kama “ascobic acid” ama ascorbate. Vitamini C ni katika water soluble vitamini ambayo husaidia kukinga mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeyee au kitaalamu scurvy. Ni maradhi hatari sana yanayodhurua afya. Kwa maelezo zaidi ya maradhi haya enelea kusoma makala hii.


Vitamini C vimegunduliwa miaka ya 1920 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Albert von Szent Györgyi. Pia itambulike kuwa hapo mwanzo mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Kazimierz Funk yeye alieleza kuwa kuna maradhi yanasababishwa na upungufu wa virutubisho mwilini. Katika maradhi hayo aliyoyataja ugonjwa uitwao scurvy yaani kisehehe aliupa virutubicho kwa herufi C.


Baada ya ugunduzi wa Albert von Szent na haworth wakaipa herufi C kemikali iitwayo ascobic acid. Na hii ndiyo vitamini C. hivyo herufi C kwenye vitamini C ina maana ascobic acid hii ni tindikali. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa wanyama katu hawawezi kuishi bila ya vitamini C mwilini mwao.Vitamini C ndio vitamini vya kwanza kuweza kutengenezwa na binadamu kikemikali.


VYAKULA VYA VITAMINI C
Kwa kuwa tumeshajuwa sasa maana na historia ya vitamini C hapa nitakwenda kukueleza chanzo cha vitamini C na je ni katika vyakula vipi tunapata vitamini C. kwa ufupi wa somo ni kuwa vitamini C unaweza kuvipata kwenye matunda yenye ladha ya uchachu uchachu (citrus) na matunda vyenye rangi ya njano na kwenye mboga za majani


Vyakula vya vitamini c
1.Pera
2.Pilipili
3.Papai
4.Chungwa
5.Limao/ndimu
6.Zabibu
7.Pensheni
8.Kabichi
9.Embe
10.Nyanya
11.Tunguja
12.Palachichi
13.Kitunguu
14.Karoti
15.Epo


Tofauti na mboga za majani na matunda ya uchachu na yenye rangi ya njano pia tunaweza kupata vitamini C kwa kula maini, maziwa na mayai. Pia unaweza kupata vitamini C kwa kumezaa vidonge vya vitamini C.


KAZI ZA VITAMINI C MWALINI
Kama tulivyowkisha kuona kuwa vitamini C hulunda mwili dhidi ya mashambulizi na sumu za vyakula. Pia basi vitamini C husaidia katika kulinda mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali kma kiseyeye, magonjwa ya ngozi, mifupa na moyo. Katika kipengele hiki utakwenda kuona kwa undani zaidi kuhusu kazi hizi za vitamini c mwilini:


Kazi kuu tatuza vitamini C
1.Husaidia katika utengenezwaji wa collagen hizi ni protini ambazo huhusika katika utengenezwaji wa tishu kitaalamu zinazotambulika kama connective tissue na pia husaidia katika uponaji wa vidonda na majeraha. Mtu mwenye upungufu wa vitamini C vidonda vyake vitachelewa sana kupona ukilinganisha na mwenye vitamini C vya kuatosha.


Tishu hizi ndizo ambazo zilitupa umbo letu, kwa lugha nyepesi hizi nyama zinazoonekana kwenye miili yetu, zilizofunika mbavu, mifupa, magoti, kichwa na maeneo yote ya mwili. Tishu hizi pia zinapatikana kwenye viungio vya miili yetu. Mifupa laini ya kwenye viungio vyetu pia ni katika tishu hizi. Hivyo protini huhusika katika utengenezwaji wa hizi tishu.


2.Vitamini C ni antioxidant katika miili yetu antioxidanti hufanyakazi ya kulinda miili dhidi ya mipambano ya kikemikali ya melecule ndani ya miili yetu.. Antioxidant ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika uuguzwaji wa oksijeni mwilini. Husaidia kuzui antioxidant hupunguza sumu za vyakula wilini. Miili yetu inahitaji antioxidant ili iweze kujilinda na kuwa madhubuti. Zipo antioxidant nyingia mbazo tunaweza kuzipata kwa vyakula. Mifano hiyo ni:-
?Caroteese ambayo tunaweza kuipata kwenye karot.
?Vitamini E
?Vitamini C
?Uric acid


3.Husaidia katika uupa mfumo wa kinga nguvu na uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi na uvamizi dhidi ya maradhi.


Kazi nyingine za vitamini C
1.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye (scurvy):
Ugonjwa wa kiseyeye husababishwa na upungufu wa vitamini C na kutibiwa kwa kupata vitamini C aidha kwa kutumia vyakula ama vidonge vya vitamini C. dalili za ugonjwa huu huanza kutokea mwezi mmoja toka upungufu wa vitamini C uanze kutokea mwilini.


Dalili za ugonjwa wa kiseyeye:
1.Kushindwa kuhema vizuri
2.Maumivu ya mifupa
3.Mafinzi kutoka damu
4.Uponaji ulio hafifu wa vidonda
5.Homa
6.Mwili kukosa nguvu
7.Maumivu ya misuli na viungio
8.Kifo



2.Kulinda mwili zidi ya maambukizi na mashambulizi:
Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.


Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.


3.Kulinda miili yetu dhidi ya saratani (cancer):
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:
A.Vitamini C husaidia kuborsha afya na kuishi vyema kwa wagonjwa wa saratani
B.Vitamini C inaweza kuuwa seli zinazotengeneza uvimbe wa saratani


4.Husaidia kulind miili yetu dhidi ya maradhi yanayohusu mishipa ya damu na moyo (cardiovascular)
5.Husaidia kulinda miili yetu dhidi ya maradhi ya ubongo na kusahasahau


UPUNGUFU WA VITAMINI C
Endapo kutatokea upungufu wa vitamini C mwilini kuna athari kubwa itakayotokea mwilini ikiwemo:
?Kupata ugonjwa wa kiseyeye
?Kuchelewa kupona kwa vidonda
?Kutokwa na damu kwenye mafinzi
?Maumivu ya mifupa
?Maumivu ya misuli na viungio


ATHARI ZA KULA VITAMINI C KUPITILIZA
Kila kirutibisho kinahitajika ndani ya miili yetu kwa kiwango maalumu. Endapo kirutubisho kitakuwa kingi kupitiliza athari zinaweza kutokea katika afya ya mtu. Miongoni mwa athari za kuwa na vitamini C kupitiliza ni kama zifuatazo:-
?Kichefuchefu
?Maumivu ya tumbo
?Kuharisha
?Kufanyika kwa vijiwe ndani ya figo
?Kujaa kwa tumbo


Mwisho
Kwakuwa sasa unatambua umuhimu wa vitamini C ndani ya mwili wako. Hakikisha kula vyakula vyema ili kusaidia katika kuboresha afya yako. Endelea kuwa pamoja na si kwa makala nyingine za Afya.





VITAMINI D NA FAIDA ZAKE MWILINI


Vitamini D ni vitamini inayosaidia miili yetu iweze kuvyonza madini ya calcium, magnesium na phosphate. Vitamini D hutengenezwa chini ya ngozi kwa kutumia mwanga wa jua. Vitamini D ipo katika makundi makuu mawili nayo ni vitamini D2 na vitamini D3. katika makala hii tutakwenda kuona zaidi kuhusu vitamini D, namna ambavyo vitamini D hutengenezwa mwilini, Je ni zipi kazi za vitamini D, na upungufu wake unasababisha athari gani mwilini?.


YALIYOMO:
1.Maana ya vitamini D
2.Makundi ya vitamini D
3.Kazi za vitamini D
4.Chanzo cha votamini D
5.Upungufu wa vitamini D


Maana ya Vitamini D
Vitamini D ni matika fat soluble vitamin ambayo imetokana compound za cholesterol. Vitamini D vimegunduliwa mwaka 1922 na Mwanasayansi anayefahamika kwa jina Elmer McCollum. Historia ya uchunguzi huu wa vitamini D ulianzia toka mwaka 1914 wakati Elmer McCollum na Marguerite Davis walipogundua vitamini A


Vitamini hivi vimeitwa D kwa sababu ndio vitamini vya nne kugundulika toka A, B, C na sasa ni vitamini D. ugunduzi wa vitamini D ulianzia kwenye mbwa mgonjwa ambaye alikuwa ana matege. Baadaye ikajulikana kuwa mbwa aliweza kupona matege kwa sababu ya chembechembe amazo baadaye ndiyo zikaitwa vitamini D.


Makundi ya vitamini D
Kama ilivyokuwa vitamini K na vitamini B zina makundi mengi. Basi hata hivyo vitamini D vimegawanyika katika makundi kadhaa, makuu katika kundi hilo ni vitamini D2 na bitamini D3. makundi haya mawili kwa pamoja ndiyo hufahamka kama vitamini D.


Vitamini D1 na vitamini D2 kwa pamoja pia huitwa calciferol. Vitamini D2 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwa ka 1931 na vitamini D3 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwaka 1935.


Kazi za vitamini D
Katika miili yetu vitamini D ina kazi kuu ya kufanya metabolism ya madini ya calcium. Kwa lugha nyepesi ni kuhakikisha kuwa unyonzwaji wa madini ya chumvi ambayo ni calcium, magnesium na phosphate unafanyika vyema ndani ya utumbo mdogo.


Faida za vitamini D:
1.Husaidia kufyonza mwili kufuonza madini ya calcium
2.Husaidia kuboresha afya ya mifupa
3.Husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani
4.Husaidia kuboresha mfumo wa faya
5.Kupunguza uzito na kitambi


Chanzo cha vitamini D
Chanzo kikuu cha vitamini D ni mwanga wa jua ambao husaidia katika utengenezwaji wa vitamini D chini ya ngozi. Kama mtu hataweza kupata mwangaza wa jua vyema kuna uwezekano wa kupata upungufu wa vitamini D.


Pia tunaweza kupata vitamini D kutoka katika vyakula na mboga, kama vile:-
1.Uyoga
2.Yai lililopikwa
3.Maini
4.Samaki


Upungufu wa vitamini D
Upungufu wa vitamini D unaweza kusababisha athari kubwa kwenye afya. Miongoni mwa athari hizo ni:-
1.Matege
2.Udhaifu wa mifupa
3.Mifupa kuvunjika kwa urahisi



VITAMINI E NI NINI
Vitamini E ni moja kati aya vitamini ambavyo vinapatikana kwenye vyakula, matunda na mboga. Pia unaweza kuvipata kwa njia ya vidonge kutoka kwenye maduka ya madawa. Kama vilivyo vitamini A, B, C, D na K vitamini E navyo endapo vitapungua mwilini kutakuwepo na madhara kiafya. Ijapokuwa upungufu wa vitamini hivi ni aghalabu sana kutokea. Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake.


Mnamo mwaka 1922 wanasayansi wawili kwa majina ya Herbert Mclean Evans na mwenzie Katharine Scott Bishop waligundua vitamini E. baada ya ugunduzi wa vitamini E tafiti mbalimbali ziilifanywa katika kuonyesha ni zipi kazi za vitaini E mwilini. Kwa mfano Mwaka 1946 wanasayansi walikuwa wakifanya tafiti juu ya nadharia inayodai kuwa vtamini E husaidia dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu (coronary heart diseases). mwaka 1949 tafiti zilifanywa kuhusu nadharia ya kuwa vitamini E huweza kusaidia watoto njiti kuwakinga na maradhi kadhaa.


Kazi za vitamini E mwilini
Vitamini E katika miili yetu zina kazi kuu zifuatazo:
1.Vitamini E bi antioxidant, ndani ya miili yetu husaidia katika kuzuia athari za kemikali mbaya zifiharibu miiliyetu.
2.Husaidia katika utengenezwaji wa utando wa seli,na kulinda seli dhidi ya uharibifu wa kemikali.
3.Husaidia katika ukuaji mzuri wa misuli.
4.Husaidia katika utengenezwaji wa utando maeneo mbalimbali ya mwili kama kwenye neva, mapafu, na maeneo mengine


Upungufu wa vitamini E
Upungufu wa vitamini E hutokea nadra sana lakini tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E vikipungua mwilini vinaweza kusababisha matatizo kwenye mfumo wa fahamu., ukuaji mzuri wa misuli na udhaifu wa misuli. Pia upungufu wa vitamini E unaweza kuathiri macho na hivyo kupelekea mtu kutoona vizuri.


Vyakula vya vitamini E
1.Nyama ya kuku, ngo’ombe
2.Maini
3.Mayai
4.Alizeti
5.Karanga
6.Spinach
7.Korosho
8.Mchele
9.Viazi vitamu
10.Siagi
11.Samaki
12.Maziwa
13.palachichi


Tafiti mbalimbali kuhusu vitamini E
Tafiti hizi zilifanya lakini zinahitaji kuendelea zaidi maana bado majibu ya uhakika hayajapatikana juu ya matokeo ya tafiti hizo. Ijapokuwa maneno ni kama hivyo lakini ukweli ni kuwa vitamini E vina faida katika afya zetu:-
1.Mwaka 2017 tafiti zilifanya na kuonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kupunguza udhaifu wa misuli wakati wa kuzeheka
2.Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kulinda mtu dhidi ya maradhi ya ubongo kama kusahausahau na kuchanganyikiwa.
3.Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E mwilini husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya figo, kibofu, mapafu na korodani.
4.Husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu
5.Husaidia kwa wajawazito





VITAMIN K NA FAIDA ZAKE MWILINI
Vitamini K ni moja kati ya vitamini ambavyo miili yetu inavihitaji kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Endapo upungufu wa vitamini hivi utatokea basi madhara makubwa ya kiafya yatamkumba mtu. Katika makala hii nimekuandalia somo hili ambalo litakwenda kuangalia zaidi kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake.


YALIYOMO:
1.Nini maana ya vitamini
2.Vitamini K ni nini?
3.Wapi nitapata vitamini K
4.Ni zipi kazi za vitamin K
5.Ni zipi athari za upungufu wa vitamini K
6.Ni zipi athari za kuzidi kwa vitamin K


NINI MAANA YA VITAMINI?
Vitamini ni kampaudi ogania ambazo zinahitajika na mwili kwa ajili ya ukuaji wa mwili na utendaji wa michakato ya kibaiolojia ndani ya miili (metabolism), na ni viruubisho ambavyo havitengenezwi ndani ya miili yetu. Vitamini vipo katika makundi makuu mawili ambayo ni fat soluble na water soluble. Pia makundi ya vitamini ni A, B, C, D na K.


Fat soluble ni titamini ambavyo mwili unaweza kuvihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye vitamini hivi ni kama A, D, E na K. Hii ina maana hatuhitaji tule vyakula vyenye vitamin hivi kila siku. Watwer soluble ni vitamini ambavyo mwili hauwezi kuvihifadhi mwilini hivyo baada ya kula chakula mwili hufyonza kiasi cha vitamini hivi na kuvitumia. Hivyo tunahitajika tule vyakula vyenye vitamini hivi kila siku. Vitamini hivi ni kama D na C.


VITAMIN K NI NINI?
Hivi ni vitamini katika kundi la fat soluble ambavyo vimetokana na kampaundi za naphthoquinone. Vitamin hivi vimeitwa K, hii K asili yake ni neno la lugha ya Danish kutoka neno koagulation neno hili ukilileta kwenye lugha ya kiingereza unapata coagulation yaani kuganda. Hasa hapa kunazungumziwa kuganda kwa damu. Kwani vitamin K huhitajika mwilini katika kusaidia mchakato wa kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.


Kwa mara ya kwanza vitamin K vimeanza kuletwa kwenye maandishi na mwanasayansi wa Danish mwaka 1929 Bwana Henrik Dam pindi alipokuwa akifanya tafiti juu ya kazi za Cholesterol kwenye mwili. Wataalamu wa lishe wameigawa vitamin K katika makundi ya K1 na K2. hivi vya K1 kitaalamu huitwa phytonadione huweza kupatikana kwenye mboga za majani na hivi vya K2 kitaalamu huitwa menaquinone hupatikana kwenye nyama, mayai na maziwa.



VYAKULA VYA VITAMIN K
Kama ulivyosoma hapo juu kuwa vitani K vipo katika makundi kma Vitamin K1 na vitamin K2 na pia umeona kwa ufupi vyanzo vya kila vitamini K. sasa hapa nitakuorodheshea tena vyanzo vya vitamin K
Vitamin K1:
Vitamini hivi unaweza kuvipata kwenye mboga za majani za rangi ya kijani kama
1.Mchicha
2.Kabichi
3.Spinach
4.Kisamvu
5.Mboga nyinginezo za majani
6.Mapalachichi
7.Zabibu
8.Na matunda mengineyo


Vitamin K2
Hivi unaweza kuvipata kwenye;-
1.Nyama
2.Mayai
3.Siagi
4.Maziwa
5.Na vyakula vinginevyo vya mfanano na hivi


KAZI ZA VITAMIN K MWILINI
Kama tulivyokwisha kuona maana ya K kweye vitamini K, sasa hebu tuone baadhi tu ya kazi za Vitamin hivi.
1.Husaidia katika kuganda kwa damu
2.Husaidia katika afya ya ubongo
3.Husaidia katika kulinda afya ya mifupa
4.Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo
5.Husaidia katika uthibiti wa matumizi ya madini ya calcium (chumvi) mwilini


1.Kuganda kwa damu:
Hii ndiyo kazi kuu ya vitamin K, ni kuwa pindi unapopata jeraha lolote ambalo litapelekea damu kutoka, basi ili kuhakikisha damu haitoki zaidi katika jeraha lile,na hatimaye damu hukata, kazi hii yote hufanya na vitamin K hasahasa hapa tunazungumzia K1. vitamini K hutumika katika kutengeneza prothrombin, factors VII, IX, pamoja na X, kwa pamoja huitwa cloting factor na ndizo ambazo huhusika katika kusimamisha damu isiendelee kutoka kwenye jeraha. Upungufu wa vitamin K unaweza kusababisha damu kutokuganda ama utoka hata kama hakuna jeraha.


2.Husaidia katika Afya ya Mifupa
Kuna ugonjwa unatambulika kama osteoporosis haya ni maradhi ya mifupa kuwa midhaifu, kuuma na kuweza kupasuka kwa urahisi sana. Mara nyingi maradhi haya yanawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 50, lakini pia unaweza kuwapata watu wenye chini ya hapo.
Wataalamu wa afya wanahusianisha upungufu wa vitamin K na kupata maradhi haya. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamin K husaidia katika kuboresha afya ya mifupa, kuthibiti ujazo na tungamo la mifupa pia kuzuia mipasuko kwenye mifupa. Hatahivyo tafiti zaidi zinahitajika kuthibitisha zaidi.


3.Afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu;
Tafiti zinahusisha uwezo wa kukumbuka na vitamin k. baadhi ya tafiti zilizofanywa zinaonyesha kuwa watu wenye umri wa zaidi ya 70 huwa uwezo wao wa kukumbuka unapungua, ila kwa wale ambao wana vitami K vya kutosha kwenye damu zao uwezo wao wa kukumbuka unakuwa mkubwa. Na hapa pia tunazungumzia sana vitamin K1.


4.Kuboresha na kulinda afya ya moyo
Vitamin K husaidia katika kushusha presha ya damu kwa kuzuia kuganda kwa madini ndani ya mishipa ya damu. Hali hii huweza kusaidia moyo uweze kusukuma damu bila ya matatizo yeyote. Tafiti zinaonyesha kuwa kuwa na vitami K vya kutosha huzuia ama kupunguza athari za kupata stroke yaani kupalalaizi.


5.Hulinda mwili dhidi ya kukuwa kwa seli za sartani.
Baadhi ya waandishi wanaeleza kuwa vitamin K huweza kusaidia kuondosha ama kulinda mwili zidi ya kupata vimbe za saratani. Lakini bado hakuna ushahidi wa kisayansi wa kutosheleza kuthibitisha madai haya.


ATHARI ZA VITAMIN K
Ijapokuwa vitamin K vinafida kubwa ndani ya miili yetu kama tulivyoona hapo juu. Basi pia itambulike kuwa vitamin K vikizidi zaidi ndani ya miili yetu vinaweza kusababisha madhara ya kiafya kama;-


Kama vitamin K itakuwa ni nyingi ndani ya mwili inaweza kupelekea athari kwenye figo. Pia inaweza kuhatarisha afya ya ini kama itatumika kwa kiwango kikubwa zaidi. Inaweza kuhatarisha ugandaji wa damu kwenye ini. Ni K vinaweza kushusha kiwango cha sukari hivyo kwa wenye kisukari itakuwa ni vyema akiwa chini ya uangalizi wa daktari kama anatumia dozi ya vitamin K.


UPUNGUFU WA VITAMIN K
Kama tulivyoona kazi za vitamin K katika miili yetu sasa hebu tuone ni zipi Athari za upungufu wa vitamin hivi ndani ya miili yetu
1.Kuchelewa kuganda ama kusimama kwa damu katika jeraha ama kidonda
2.Kutokwa na damu hata kama hakuna jeraha
3.Ni rahisi kupata maradhi ya saratani (cancer)
4.Ni rahisi kupata maradhi ya moyo
5.Kupunguza hadira na misongo ya mawazo
6.Kutoweza kuthibiti kumbukumbu

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 2381


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Dua Sehemu ya 02
Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa. Soma Zaidi...

kitabu cha matunda
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Fahamu mtindo mzuri wa maisha
Postei hizi inahusu zaidi mtindo mzuri wa maisha, yaani mtu ale ki vipi au afanyeni nini ili kuweza kuboresha afya yake. Soma Zaidi...

kitabu cha matunda
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Kitabu Cha Afya na Lishe
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

NJIA AMBAZO MARADHI HUAMBUKIZWA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

YANAYOATHIRI AFYA KATIKA SHUGHULI ZA KILA SIKU
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Nini hutokea unapokuwa kwenye ndoto ukiwa usingizini umelala
Ndoto ni moja ya mamba ambayo yanatokea mwanadamu na sayansi haina uelewa hasa nini hutokea. Hata hivyo yapo machache tafiti za kisayansi zinatueleza. Soma Zaidi...

KAULI ZA WATU MASHUHURI KUHUSU AFYA
Soma Zaidi...

FAIDA ZA MATUNDA MBALIMBALI
1. Soma Zaidi...