Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.
Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.w).
Ahadi kubwa wanayotoa Waislamu mbele ya Allah (s.w) ni shahada; pale wanapo ahidi kuwa hawatamshirikisha Allah (s.w) na chochote na kwamba wataishi maisha yao yote kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mtume wake, Muhammad (s.a.w). Rejea (6: 162 -163)Katika Suratul-Fur-qaan sifa za Waumini zinabainishwa tena kama ifuatavyo:
โNa waja wa Rahmaan; Ni wale wanaokwenda ulimwenguni kwa unyenyekevu; na wajinga wakisema nao (maneno mabaya) huwajibu (maneno ya) salama. (25:63).
Na wale wanaopitisha baadhi ya saa za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama. Na wale wanaosema:โMola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam, bila shaka adhabu yake ni yenye kuendelea(25 :64-65).
Hakika hiyo (Jahannamu) ni kituo kibaya na mahali (pabaya kabisa) pa kukaa โ.Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo. (25:66-6 7)
Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Allah, wala hawaui nafsi aliyoiharamisha Allah ila kwa haki, wala hawazini; na atakayefanya hayo atapata madhara (papa hapa ulimwenguni).(25:68).
Na atazidishiwa adhabu siku ya Kiyama na atakaa humo kwa kufedheheka milele (25:69).
Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri, basi hao ndio Mwenyezi Mungu atawabadilishia maovu yao kuwa mema; na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa ku reh em u. (25:70).
Na aliyetubia na kufanya wema, basi kwa hakika yeye anatubu kw eli kw eli kw a Mwenyezi Mungu.(25:71)
Na wale ambao hawashuhudii shahada za uwongo, na wanapopita penye upuuzi, hupita kwa hishima (yao). (25:72)
Na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao haw aziangukii kw a uziw i na upofu.(25:73)
Na wale wanaosema: โMola wetu! Tupe katika wake zetu na wototo wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao (Mungu). (25:74).
Hao ndio watakaolipwa ghorofa (za Peponi) kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo hishima na am ani(25 :75).
Wakae humo milele; kituo kizuri na mahali pazuri (kabisa pa kukaa.) (25:76)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa sifa za Waumini ambao hapa wameitwa โWaja wa Rahmanโ ni pamoja na:
Umeionaje Makala hii.. ?
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah.
Soma Zaidi...Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.
Soma Zaidi...