Mgawanyo wa Elimu katika Faradh βAin na Faradh Kifaya
Faradh ya elimu inaweza kugawanywa kwenye faradhi βAin na faradh Kifaya. Faradh βAin ni faradh inayomhusu kila mtu binafsi isiyo na uwakilishi. Mfano, kusimamisha swala, kutoa Zakat, kufunga, n.k. ni katika faradh βain.
Faradh Kifaya ni faradh inayoweza kufanywa kwa uwakilishi. Ni faradhi ya kijamii. Wachache wanaweza kuitekeleza kwa niaba ya jamii. Kwa mfano swala ya maiti na yale yote ya faradh anayostahiki kufanyiwa maiti wa Kiislamu ni katika faradh kifaya.
Elimu ya Maarifa ya Uislamu, itakayompelekea mja kumtambua, Mola wake, vilivyo na kumuabudu inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha ni faradh βAin.
Kwa maana nyingine ni faradh kwa kila Muislamu kuujua Uislamu vilivyo na kujitahidi kuutekeleza kwa kadiri ya uwezo wake katika kila kipengele cha maisha.
Elimu juu ya fani mbalimbali zinazohitajika katika maisha ya jamii ni faradhi kifaya kwa jamii ya Kiislamu. Kwa mfano ni faradhi kwa jamii ya Kiislamu kuwa na madaktari, wahandisi, wanasheria, wanasiasa, wanauchumi, waalimu na wataalamu wengineo katika kila fani ya maisha ya jamii wa kutosha kukidhi mahitajio ya jamii katika kuendea nyanja zote za maisha.
Ikitokezea Waislamu wamezembea kiasi cha kushindwa kutoa wataalamu wanaohitajika kuendesha kila fani ya maisha ya jamii mpaka inapelekea Waislamu kushindwa kumuabudu Mola wao ipasavyo katika kila kipengele cha maisha, jamii yote ya Waislamu itakuwa katika lawama (itapata dhambi) na itaathirika kutokana na dhambi hii.
Hivyo ili Waislamu waweze kusimamisha Uislamu (Ukhalifa wa Allah) katika jamii, kila Muislamu hanabudi kuufahamu Uislamu vilivyo na pawekwe mazingira ya makusudi yatakayomuwezesha kila Muislamu kujielimisha katika fani maalumu ya maisha inayohitajika katika jamii kwa kadiri ya vipaji alivyoruzukiwa na Mola wake.
Kwa maana nyingine kila Muislamu mwenye vipaji vya kuwa Daktari au Mhandisi au Mwanasheria au Mchumi au Mwalimu au β¦. ajizatiti kuiendea taaluma hiyo na jamii ijizatiti kumuwezesha. Endapo, kwa mfano Muislamu mwenye kipaji cha kuwa Daktari, akazembea asiwe Daktari atakuwa mas-uli mbele ya Allah (s.w). Pia endapo jamii ya Waislamu itazembea isitoe Madaktari wanaohitajika itakuwa mas-uli mbele ya Allah (s.w).
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.
Soma Zaidi...βNa wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti.
Soma Zaidi...