picha

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran

Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki.

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran


Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Nao waliambiwa: "Njooni mpigane katika njia ya Mwenyezi Mungu au mzuie (maadui pamoja na sisi)" Wakasema: "Tungejua kuwa kuna kupigana bila ya shaka tungelikufuateni." Wao siku ile walikuwa karibu na ukafiri kuliko na Uislamu (japokuwa siku zote wakidhihirisha Uislamu wa uwongo). Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema (yote) wanayoyaficha. (3:167)


Wale waliosema juu ya ndugu zao - na (wao wenyewe) wamekataa kwenda (hawakwenda) vitani: "Wangalitutii wasingeuawa." Sema: "Jiondoleeni mauti (nyinyi) wenyewe msife maisha ikiwa mnasema kweli." (3:168)



"Wala usiwadhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu (maiti). Bali wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao." (3:169).
Kutokana na aya hizi tunapata sifa za wanafiki zifuatazo:



(i)Hawako tayari kujitoa muhanga kupigania dini ya Allah (s.w) isimame katika jamii au kuihami isiangushwe baada ya kusimama kwake.



(ii)Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Baada ya mapambano dhidi ya maadui wa Dini ya Allah (s.w) kwisha, wanafiki hujikosha kwa kusema uwongo kuwa hawakuwa na taarifa juu ya mapambano ya Waislamu dhidi ya maadui zao, vinginevyo wangelikuwa Pamoja katika vita hivyo hali ya kuwa walijificha wasiende vitani kwa kuogopa kufa.



(iii)Huwabeza na kuwalaumu wale wanaouliwa au kupata misuko suko katika kuupigania Uislamu.
Katika aya ya 168 na 169 (3:168-1 69), Allah (s.w) anawasuta wanafiki na kuwakatisha tamaa kuwa mtu hafi kwa kuwa amepigania dini ya Allah (s.w), bali kila mtu atakufa kwa ajali yake aliyopangiwa:



“… Sema: (uwaambia wanafiki): "Jiondosheeni mauti (nyinyi wenyewe msife milele) ikiwa mnasema kweli."



Pia Allah (s.w) anawakatisha tamaa wanafiki na kuwatumainisha waumini kuwa hapana jambo lililozuri na bora kwa mtu kuliko kufa katika njia ya Allah (s.w) (kufa shahidi).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 1118

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 web hosting     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

MAADILI MEMA KATIKA UISLAMU

Yajuwe maadili mema yaliyotajwa katika quran

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Dua 120

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa maswahaba wa mtume (s.a.w)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa tabiina (wafuasi wa maswahaba)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa tabii tabiina

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...