Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia upele, ni njia ambazo utumiwa Ili kupunguza tatizo la upele kwenye jamii, kwa hiyo jamii inapaswa kutumia njia hizi Ili kuweza kupambana na ugonjwa huu ambao unatibika.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kuoga mara kwa mara walau mara mbili kwa siku kwa wale ambao hawajapata ila kwa waliopata wanapaswa kuoga zaidi ya mara mbili au wakioga hata mara tatu sio mbaya na pia kila wanapooga wanapaswa kubadilisha nguo chafu na kuvaa nguo safi Ili kuweza kuepuka kuendelea kuwepo kwa maambukizi.
2. Pia tunapaswa kuwatafuta watu ambao Wana dalili za ugonjwa huu na kuwapatia matibabu muhimu Ili waweze kuwa vizuri Pia kuzunguka kwenye vijiji mbalimbali Ili kuwatafuta wagonjwa wote hasa hasa wale wasiopenda kwenda hospital wapewe elimu Ili waone umuhimu wa kwenda hospital.
3. Watu wanapaswa kupewa elimu kuhusu namna ya kufanya usafi kwa sababu kwa wale wanaozingatia usafi ni vigumu sana kupata ugonjwa huu kwa hiyo ni vizuri kuwajulisha njia na namna ugonjwa huu unavyosambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na jinsi ya kutibu ugonjwa huu.
4. Vile vile na mifumo ya maji inapaswa kuboreshwa Ili watu waweze kupata maji ya kutosha kwenye familia na nyumba baada ya nyumba kwa kufanya hivyo watu wataweza kufua na kuoga na maambukizi yataisha au kupunguza kwa kiasi.
5. Pia wahudumu wa afya na viongozi wanapaswa kwenda mashuleni kutoa elimu kwa watoto kuhusu namna ya kujikuna kwa sababu watoto wengi wanapata kwa kuambukizana kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine na tatizo kama lipo watibiwe kwa wale walioambukizwa Ili kuepuka maambukizi kuendelea.
6. Vile vile wahudumu wa afya wanapaswa kuzunguka kutoka kwenye nyumba Moja na nyingine Ili kutibu wale wenye ugonjwa tayari.kwa hiyo jamii inapaswa kuelekezwa kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni uchafu na dawa kuu ni usafi kwa kujua hivyo hali itaweza kutulia na watu watapona.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1582
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Ugonjwa wa mfumo wa kinga ya mwili inavyoshambulia ini.
Ugonjwa huu hupelekea kuvimba kwenye ini yako ambayo hutokea wakati mfumo wa kinga ya mwili wako unaposhambulia ini lako. Soma Zaidi...
Maajabu ya damu na mzunguuko wake mwilini.
Ukistaajabu ya Musa utastaajabu ya Firauni. Haya ni maneno ya wahenga. Sasa hebu njoo u staajabu ya damu Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ukoma, ni Ugonjwa unaosababishwa na mdudu anayeitwa mycobacterium leprae, mdudu huyu kwa kawaida uathiri sana sehemu za ngozi na sehemu za Neva mbalimbali za mwili Soma Zaidi...
Ugonjwa wa coma
Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la Kichwa, Kiharusi, Uvimbe kwenye ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, Soma Zaidi...
Madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, ni madhara ambayo yanaweza kutokea iwapo maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo hayatatibiwa kwa wakati. Soma Zaidi...
Dalili za ugonjwa wa kipindupindu
Post hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa kipindupindu.Ni dalili zinzojitokeza kwa magonjwa wa kipindupindu. Soma Zaidi...
Dalili za vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo no tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda,hutokea baada ya ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaitwa mucus kuharibika.
Vidonda vya tumbo (peptic ulcers) imegawanyika katika ma Soma Zaidi...
Ugonjwa wa kisonono
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kisonono, ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu ambaye kwa kitaalamu huitwa Neisseria gonococcal. Soma Zaidi...
Matatizo ya unene kwa watoto (childhood obesity)
post Ina onyesha madhara na matatizo ya Unene Utoto ni hali mbaya ya kiafya inayoathiri watoto na vijana. Inatokea wakati mtoto yuko juu ya uzito wa kawaida kwa umri na urefu wake Soma Zaidi...
Njia za kupambana na saratani
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na saratani Soma Zaidi...
Vidonda vya tumbo husababishwa na nini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu visababishi vya vidonda vya tumbo Soma Zaidi...
Dalili za maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo,ni dalili ambazo ujionesha kwa mtu akiwa na shida kwenye utumbo mdogo na tumbo la kawaida. Soma Zaidi...