picha

Faida za kula ukwaju

Uchachu wa ukwaju, ndio ubora wake, kuna virutubisho vingi kwa kula ukwaju, soma makala hii

Faida za kula ukwaju

22. Faida za ukwaju (Tamarind)
Ukwajju ni katika mimea ambayo matunda yake yanatumika katika kutengenezea madawa ya hospitali. Kinywaji cha ukwaju hutumika katika kutibu kuharisha, kukosa choo, homa na aina za vidonda vya tumbo. Tofauti na matunda pia majani na maganda ya mti huu pia hutumika katika kutibu vidonda. Wataalamu wa afya bado wanaendelea kuuchunguza mti huu kwa ajili ya kupata tiba zaidi.

Antioxidant ambayo ipo kwenye ukwaju husaidia katika kudhibiti na kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo, saratani na kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa ukwaju husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Pia kwa watu wenye kutaka kupunguza uzito, ukwaju pia husaidia.

Ukwaju una virutubisho vingi sana kama vile:- madini ya magnesium, potassium, chuma, calcium na phosphorous. Pia kuna vitamin B1 (thiamin), vitamin B2 (riboflavin), vitamin B3 (niacin). pia kuna vitamin C, k na B6 na B5. kwa ufupi ukwaju ni katika matunda ya asili yalotumiwa na watu toka zamani sana.

Katika ukwaju kuna polyphenols kama vile flavonoids ambayo husaidia katika kudhibiti kiwango cha cholesterol na triglycerides. Antioxidant zilizomo kwenye tunda hili husaidia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo. Pia ukwaju husaidia katika kutengeneza dawa za malaria.

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa ukwaju husaidia katika kupunguza uzito. Itambulike kuwa kuzidi uzito mwilini kunahusianishwa sana na maradhi ya moyo, ini, na figo. Hivyo ukwaju husaidia katika kupunguza choloesterol mbaya (LDL) na husaidia katika kuongeza cholesterol nzuri (HDL).

Ukwaju una potassium bitartipate ambayo hii husaidia katika upatikanaji wa choo na kuzuia kuganda kwa choo. Mizizi na maganda ya mkwaju husaidia sana kwa maumivu ya tumbo. Uw.epo wa procyanidins kwenye ukwaju husaidia katika kulinda ini dhidi ya uharibifu. Pia ukwaju hutumika katika kutibu along’atwa na nyoka.


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 6455

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰2 web hosting     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰5 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Faida za kiafya za parachichi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula parachichi

Soma Zaidi...
Vyakula muhimu kwa kulinda afya ya macho - Epuka upofu kwa kula vyakula hivi

Matatizo ya macho yanaweza kuruthiwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto. hata hivyo shughuli zetu na vyakula tunavyokula vinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa matatizo haya. Hapa nitakuletea vyakula muhimu kwa afya ya macho yako.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula pera

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pera

Soma Zaidi...
Faida za kula Palachichi

Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula uyoga

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula uyoga

Soma Zaidi...
Nyanya (tomato)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyanya

Soma Zaidi...